Sitosahau UKIMWI ulichofanya mtaani kwetu. Nyie watu wa mapenzi kuweni makini

Kuna mmoja alikuwa anaumwa yaani ukikalia kitandani pia anaumia ile ngoma sio mchezo aliondoka yule dada yeye na mume wake sio mchezo.
 
Asante sana kwa kutukumbusha na kutupatia msisitizo. Kesho Nina game na katoto flani hv, acha nisiuze mechi.
 
Kilichozungumziwa apo mateso ya ukimwi ni ukijumlisha viugonjwa vyote ulivyovitaja apo uweke na kipindupindu juu yake ndo unafikia ngwengwe key word #mateso
 
Una ujinga (siyo tusi) mwingi sana.
 
Ni mpumbavuuu huyoo anajua ukweli ila unaupindishaaa ilo aonekane ana akilii kumbe zero brain...!! HIV is really aiseee hatari sana hiyo kituuuu yani mtu anaedhani ukimwi haupo ana matatizo ya akili..
Kunawatu wanautetea sana ukimwi [emoji1787][emoji1787][emoji1787] kwamba ni ugonjwa mdogo, kunakitu sio bure [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Watu wanasema UKIMWI ni kama mafua, ila usiombe kumwona mgonjwa wa UKIMWI anayekaribia kufa. Tuendelee kujilinda na kuepuka ngono zembe

Ni kweli ni hatari ,nilimuona sister mmoja hivi aisee ni noma kaisha balaa madonda mdomoni puani kibao ,uzuri ARV zilikuwa tayari zishaanza hiyo ilikuwa around 2008 ,mpaka sasa yupo amenenepa sana ,ukimuona hauwezi mjua kama Tayari kaumia.
 
Kunawatu wanautetea sana ukimwi [emoji1787][emoji1787][emoji1787] kwamba ni ugonjwa mdogo, kunakitu sio bure [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Ugonjwa usio na dawa ya kutibia hauwezi kuwa mdogo au wa kawaida. Hizi gono, syphilis yalikuwa magonjwa hatari kabla ya kugundulika dawa za kutibia ziliuwa hadi wafalme miaka iyo dawa hakuna lakini saivi yanaonekana ni magonjwa ya kawaida kwa saabu unapata dawa zipo kibao tena unazipata apoapo kwenye famasi ya mtaani kwako tu. tuendelee kuomba dawa ya kutibu ipatikane.
 

Duuuh hatari ,na pedicure na manicure ,wanasugua miguu na mikono kwa brush si ndiyo muambukizana tu ni kama kutumia mswaki mmoja.
 
Issue siyo Tohara. Mafinga wanatiana sana sababu ya hali ya hewa na pia magari makubwa mengi yanapiga kambi pale. Sisi wengine tumefanya research ni mji unaokua sana. Na una mchanganyiko mkubwa kama mleta mada alivyosema. Hali ya baridi na vyakula pale watu wanatiana masaa 24.
 
Duuuh hatari ,na pedicure na manicure ,wanasugua miguu na mikono kwa brush si ndiyo muambukizana tu ni kama kutumia mswaki mmoja.
Brush sio shida sana kuna vile vya kutoa uchafu kwenye kucha ninavyo lakn siwezi kutembea navyo muda wote, japo ingekuwa hivyo nadhani maambukizi yangekuwa juu sana ni km saluni na kunyoa,. Kuna mdau kasema virusi vya ukimwi haviwezi kuishi nje ya mfumo wa damu hata kwa dakika 1,, sielewi kwakweli
 

Yes HIV wanakuwa inactive wwakiwa nje ya damu na ndiyo maana % kubwa ya maambukizi inatokana na NGONO ZEMBE.
 
Kwa mujibu wa baiolojia ya kidato cha pili che; virusi (vikiwemo vya UKIMWI) vina sifa zote za viumbe hai na visivyo hai.

Kwahiyo; kinapokuwa nje ya seli hai kinakuwa inactive (dormant) punde tu kinapopata access ya kuwa kwenye seli hai kinaanza kuishi.

Haya mambo magumu sana kuyaelewa! 😁
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…