Sitosahau yaliyonipata kijijini Kwamsisi

Sitosahau yaliyonipata kijijini Kwamsisi

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Ulisema kweli tulikupinga huwa unaona mbali

Sasa me nauliza pm tunaenda bure au na hela hajanyoosha maelezo vizuri
Pm anakuwa hajabanwa sana kama kuandika huku.... Muendelee tu kunitukana. Mi nikiona uzi mwanzoni tu najua uelekeo wake.
 
SEHEMU YA 3

Mwalimu mkuu alituita kikao kilikuwa ni kikao kizito kujadili ujumbe ulioletwa na mzazi mmoja kwenye karatasi iliyokuwa imefungwa kwenye bahasha ya khaki alionekana kuwa akitetemeka na hakuwa sawa kisaikolojia, mimi nilikuwa ndio kwanza nikisahihisha madaftari huku nikibadilishana maongezi na mwalimu huyu wa kike aliyetokea kuwa karibu sana na mimi nilishtuka kumuona mwalimu mkuu akiwa kwenye hali ile.

"Walimu habari za mchana?" Tulikuwa walimu wanne wote tulitahamaki na hakuna hata mmoja aliye jibu wote tulikaa kimya. Siti akajibu, "nzuri." Sauti yake ikasikika kwa wote nasi tukarudia tena "nzuri." "Inaweza kuwa ni nzuri kwenu au la mmejibu kwa mazowea tu lakini kuna vita kali sana inayoendelea kati yetu haswa kwa nyinyi walimu wageni, inaonekana mmeshindwa kabisa kuheshimu wazee wa kijiji hiki, mzee Sa-Masimba ameleta barua hii amemtuma mwanaye ailete barua hii imenitisha kidogo kuisoma japo sijaielewa lakini ina alama ya damu.

"Alama ya damu?!" wote tulihamaki. "Ndio ni damu ya halisi kabisa ni kidoti kimewekwa juu ya bahasha kikiwa kimechovywa kama na kidole cha mkono, inaonekana kuna mtu anawindwa hapa je ni nani anayewindwa na kwanini?" alihoji mwalimu mkuu.

Barua ilisomeka, "Ndugu mwalimu mkuu hongera kwa kupata wafanyakazi wapya lakini sidhani kama vijana hao uliwafunza juu ya mila za kwetu, kuheshimu wazee na kuto jiingiza kwa namna yoyote na mipango ya kujaribu kupambana na wazee wa kimila, kama hiyo haitoshi kutengeneza wigo na kujiona kuwa huingiliki kwetu sisi tunahesabia kwamba ni dharau. Kama wameshindwa kutuheshimu japo kwa salamu mpaka kufikia hatua ya kupambana na sisi ki chawi hakika hatuta waacha salama." ilimalizika shemu ya barua hiyo.

Nakumbuka siku hiyo tuliwaruhusu wanafunzi mapema sana ilikuwa kama mchana wa saa nane hivi. Mimi nilijua fika ndiyo mlengwa mkuu hivyo niliogopa sana tulitembea mpaka kwenye nyumba ya Mzee Samasimba tulivyo karibia tu tulipiga magoti huku tukitembea kwa magoti mpaka tulipoufikia mlango wa nyumba yake, mwalimu mkuu akiwa ametangulia mbele. Mzee mwenyewe hatuku mkuta basi wakatumwa watoto kwenda kumwita alikuja huku akiwa amevaa msuli wake kiunoni aliambatana na vijana wengine wawili mmoja alimtazama sana Siti kisha akaendelea mpaka wakaingia ndani mzee alisimama pale nje mkewe akamletea kigoda(kiti cha kukalia), akakaa kutusikiliza.

Mwalimu mkuu alikuwa ametangulia mbele aliongea naye kwa lugha ya Kizigua na mwisho aliinama sana huku akimwomba msamaha. Kwakweli nikiri wazi kwamba sikuwahi kushuhudia mchawi akiabudiwa kama siku hiyo, huyu mzee inasemekana alikuwa moja kati ya wazee wenye kauli sana pale kijijini, mambo mengi yalikwama endapo tu yeye asinge shirikishwa na kukubaliana. Ilifika zamu yangu ya kumwomba msamaha kwani tulimwendea kwa zamu, niliinama na kupiga magoti na kusema shikamoo mzee Masimba mimi ni mgeni hapa kijijini naomba unisamehe kama nilikukwaza kwa namna yoyote, sikumpa mkono kama wenzangu walivyofanya niliogopa kuchukuliwa nyota.

Tuliondoka baada ya kupakwa usembe(unga mweupe) usoni na kichwani na wale vijana wake, tulidhalilishwa sana siku hiyo hamna siku nilichukia kazi hii ya ualimu kama siku hiyo tulirudi nyumbani kila mtu akiwa kimya hamsemeshi mwenzake, nilitembea huku nikiwa na mawazo mengi macho yangu yakitazama chini huku machozi yakinilengelenga. "Kwanini binadamu anaabudiwa kama Mungu!" niliwaza moyoni ilikuwa yapata majira ya saa kumi nambili jioni ikikaribia saa moja usiku, nilishtuka kumuona Siti akiwa amenishika bega la kulia kwa nyuma niligeuka na kumtazama.

"Kwahiyo ndio unaenda nyumbani, uende salama ila uwe makini, hapa ndio Kwamsisi uache ubrazameni uheshimu watu." Kumbe ile hali yangu ya kujitengetenga na kutosalimia watu iliwaudhi wengi pia kujiweka karibu na mzee Kingalu ilikuwa ni hatari kwangu niliogopa kuiendea ile njia inayokwenda nyumbani, nilipokumbuka lile jicho alilonikata mzee Masimba nilipogoma kumpa mkono wa msamaha kwa kuwa sikutaka kushikana mkono na mchawi. Basi nikajua kuwa usiku huo lazima atanijilia nyumbani kwangu.

ITAENDELEA...

Sitosahau yaliyonipata kijijini Kwamsisi-4
Stori la uongo nimeishia kwenye tone la damu.

Byeee!
 
SEHEMU YA 9

"Soka unaenda wapi mbona unaniacha mwenyewe?!" Sitti aliniita nikiwa ndio kwanza naelekea nyumbani kwangu kujipumzisha baada ya kumfikisha pale alipokuwa akiishi. "Naenda zangu nyumbani, kwani we' si nimesha kufikisha kwenu? lala upumzike." "Tafadhali nisubiri!" alisema. Hapo mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio, sikuwa na mazowea ya kihivyo na huyu binti nilimheshimu kama mwalimu mwenzangu tu na si vinginevyo.

Alinifuata akanikumbatia na kunibusu. Nami sikuwa mnyonge nilimpokea na ndani ya muda mfupi tukawa tukibadilishana mate alining'ang'ania, nikaona isiwe kesi nikamtoa kwanguvu kifuani kwangu. "Sikiliza Sitti, nenda kalale tutaongea kesho tusije kuyazusha mengine kwa sasa." Nilimuaga na kumbusu kwenye paji la uso wake kisha nika muangalia jinsi alivyogeuka mpaka alipoingia ndani ndipo nikatoka kwa kasi kuelekea nyumbani kwangu.

Nakumbuka siku zile nilikuwa nikiwindwa sana haswa nikiwa kazini ama nyumbani, ilikuwa ni ngumu kulala nyumbani kwangu mara kwa mara nilikuwa nikilala kiwizi wizi, hata wanafunzi wengine walikuwa wakitumwa makusudi kunijaribu wakinitafutia sababu ili waende kuwaeleza wazazi wao. Nilijitahidi kuwa makini juu ya hilo nilifanya yale yanayo nihusu tu. Mapenzi yangu kwa Sitti yalizidi kushamiri ingawa nilikuwa bado nikiwindwa sana.

Mzimu wa mzee Kingalu nao haukuacha kunisumbua, lakini kuna kitu kimoja ambacho kilinishangaza kwani ilikuwa kila nikilala nyumbani kwangu nilipata amani ambayo sikuitarajia kabisa yale mauzauza niliyokuwa nikiyaona mwanzoni yaliisha kabisa, baadaye nilikuja kugundua kwamba kuichimbia ile hirizi pale ndani ndio ilikuwa sababu ya yote, wachawi walishindwa kusogelea pale ama kufanya lolote nikiwa ndani ya ile nyumba.

Wachawi wanautaratibu wao pindi wamchukuapo mtu kichawi, husubiri kwanza kwa muda wa siku 40 kuona kama kuna vita yoyote ama ufuatiliaji wowote na hapo ndipo wangeweza kufanya maamuzi ya au kumla nyama ama kumgeuza msukule moja kwa moja. Sababu nyingine iliyo wachelewesha ni kutokana na ukweli kuwa mzee Kingalu alikuwa ni mchawi mwenzao tena mwenye daraja ya juu sana, kuna tetesi walisema kuwa alikuwa akifuga majini akiyafungia kwenye chumba maalum katika moja ya nyumba zake.

Kuna siku uongozi wa kijiji akiwemo mwenyekiti, afisa mtendaji pamoja na mwalimu mkuu walifika shuleni wakatuonya sana walimu juu ya kujihusisha na mambo yaliyo kinyume na taaluma zetu, mlengwa mkubwa alikuwa ni mimi na nilipewa barua ya onyo, ingawa nilijaribu kujitetea kwamba wanakijiji hawana urafiki na walimu na wala hawatupi ushirikiano zaidi ya kutuibulia vikwazo kila uchao. Viongozi hao hawakunielewa na walinitishia kunifukuzisha kazi, ilibidi niwe mpole na kuwakubalia yote waliyo yasema.

Siku moja usiku yule mganga alinijia akaniamsha na kuniambia nimfuate, ilinibidi nivae kama yeye nilivua kila nguo na kisha kuvaa kaniki nyeusi kwa mtindo wa lubega, aliniletea vazi hilo, alitaka kunitembeza na kunionyesha maajabu ya usiku. "Vaa bangili yako," alisema, nami nikaivaa kwenye mkono wa kulia, niile bangili yenye uwezo wa kuona vitu visivyoweza kuonekana kwa macho ya kawaida. Tulitembea mpaka eneo la makaburi kisha tukakaa kimya kwa pembeni mbali kidogo ili kuweza kushuhudia yatakayo tokea.

Baada ya muda wachawi walianza kuingia hapo kila mmoja kwa usafiri wake wapo waliotua kwa ungo na wapo waliotua kwa kutumia fisi na wengine kuja mithili ya kimbunga. Niliweza kushuhudia live bila chenga, basi baada ya muda nikaona yule kiongozi wao (Mzee Samasimba) amesimama kwenye kaburi lililokuwa jipya upande wa kichwani akiwa ameshika zana zake za kazi na baadaye akatokea bibi mmoja na fimbo ndefu akapiga juu ya lile kaburi na hapo maajabu yakatokea.

Mwili wa binadamu ulipanda kutoka chini ardhini mpaka juu ya lile kaburi, waliuchukua na kisha kuugawanya na hapo kulikuwa na moto mkubwa sana waliweza kuichoma ile nyama ya binadamu na nilishuhudia yule bibi akiwalisha wachawi wenzake kwa mtindo wa kuwarushia kipande kwa kipande nao hudaka kwa kutumia mdomo wao, ni kosa kubwa unaporushiwa kipande cha nyama nawe ukashindwa kukidaka, hii ilitafsiriwa kama ni dharau kwa chama chao wanacho kiabudu. Asilimia kubwa ya wachawi ni watu wa kawaida lakini matukio wanayo yafanya ni ya aibu mno.

Tuliondoka na mganga tukatembea mpaka alipokuwa nyumba ya mzee Samasimba, tulitaka tufanye tukio la hatari, tulifika na kuukosa ulinzi kabisa kwani yule mzee alikuwa yupo kwenye sherehe za kichawi, lakini kumbe nyumbayake alisha izingira na nguvu za giza na kulikuwa na mitego aliyoitega kwamba endapo kuna mtu atakaye kuja nyumbani kwake basi yeye ni lazima angejua. Tulipita kwenye banda la uwani ni banda lililozungushwa kwa majani ya mnazi baadaye mimi nilibaki pale nje mganga alizama ndani kichawi. nilimsubiri kwa muda mrefu kidogo.

Alitoka na kabla hatujapotea ki miujiza alimwaga dawa za kuondosha ushahidi. "Nimesha muweka humu kwenye hii tunguli," akimaanisha ameuweka mzimu wa mzee Kingalu kwenye kile kibuyu, tulitoka kwa tahadhari kubwa na mara tulisikia vishindo vikubwa na kelele ya kuunguruma, ilikuwa ni kelele ya mzee Samasimba baada ya kurudi kwenye sherehe zao za kichawi, kwani huyu mzee akikasirika hutoa muungurumo kama wa mnyama Simba na hii ndio sababu walimpa jina la Samasimba. tulipotea na kukimbia kila mtu kwa njia yake.

USISITE KUANDIKA MAONI...
(NB: Kutokana na ubusy wa kazi, hadithi hii itaishia hapa ila kwa atakayetaka muendelezo wake namkaribisha PM, kwa vitabu mbalimbali vya hadithi na mikasa ya kweli na story za audiobooks.)
story lako baya unataka kutuuzia we kweli lofa hatuji kununua story lako bovu la kutunga ati mkaunganisha ndimi lol kwendaaaaa [emoji3][emoji3]
 
Hujalazimishwa na hakuna mtu nimemtoza pesa kwenye hii hadithi, hukunisaidia kuandika.
pm utakuwa unampa mtu mmoja mmoja hapa unaweka mara moja tu huoni huko pm ndio kazi? unataka kutulipisha? huu uhuni tulishapita kitambo sana [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
NILIWAAMBIA NYIE MAZUZU HADITHI YA UONGO KUNA NAMNA UKIOTENGENEZA BAADAYE UNAPATA SHIDA KUOENDELEZA.
nisamehe sana mkuu nilikupinga naomba niwe muungwanga kwa kukuomba radhi mithili ya alikamwe alivyomuomba mgunda nimekosa mimi nimekosa sana [emoji1787][emoji1787]
 
nisamehe sana mkuu nilikupinga naomba niwe muungwanga kwa kukuomba radhi mithili ya alikamwe alivyomuomba mgunda nimekosa mimi nimekosa sana [emoji1787][emoji1787]
Its just ok. Hamna shida. Mi nina miaka mingi humu JF na umri pia. Ukiacha ID hii. Ya kwanza kabisa nliifungua enzi za Jambo Forum. Ukichanganya kaumri kangu ka miaka 50 plus. Naelewa sana haya mambo. Nlishafanya sana huu utapeli. So napokosoa kitu najua huyu mtu anapita ambamo nlipita mimi miaka 10 mpaka 15 iliyopita. Mnaponitukana nacheka tu.
 
Vipo vitabu vya hadithi za kutisha kwa yeyote atakaye hitaji hadithi ni za ukweli na nyingine za kubuni, kwa stori hii nitaishia hapa hopefully mnaenjoy na kujifunza pia, napokea maoni kupitia private messages (PM).
We ni kenge tu
 
Hio Kwamsisi mzee aliacha shamba la heka 50 la michungwa na minazi pamoja na nyumba ya room 3 🤣🤣🤣 sijui nini kilimpataga bana.
Fanya mpango ukafuatilie hizo mali ukiwa na maji ya mwamposa na mafuta mkononi vitarudi amini😂😂😂
 
NASHAURI MWANA JF YEYOTE ASIMUUNGE HUYU MTOA HADITHI MPUUZI SANA ANATAKA MAMBO YA PM PM KAMA AMESHINDWA KUSIMULIA KIHADITHI CHAKE TUACHANE NAE AKAFIE MBELE NA STORY YAKE.

WAPO WATU HUMU KAMA AKINA "UMUGHAKA" WAMETOA STORY ZAO HALISI ZENYE EPISODES SIJUI MPAKA ZA 60 HUKO MPAKA ZINAISHA BILA HATA KUDAI AU KULETA PROMO YEYOTE SIJUI NJOO PM.
SASA HUYU MPUUZI ANALETA STORY HATA EPISODE 10 HAJAFIKA ANALETA MAMBO YA PM.

Nimeandika kwa herufi kubwa kuona huyu jamaa anataka asumbue watu hapa. Hatuhitaji story yako
Story yenyewe ni ya kuunga unga hata haieleweki cjui ni anasimulia Bongo Movie😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom