Sitosahau yaliyonipata kijijini Kwamsisi

Sitosahau yaliyonipata kijijini Kwamsisi

Story yenyewe ni ya kuunga unga hata haieleweki cjui ni anasimulia Bongo Movie😂😂😂😂
"I want to die judge" tumeisoma mwanzo mwisho humu humu Jf na bado isidingo ya "nilimdhani kahaba kumbe ni bikra" hatujaombwa chochote sembuse iwe hii wasakatonge😂😂😂😂😂😂
 
Jina langu ninaitwa Soka (sio jina halisi) na kwetu ni huko Moshi uchagani. Nilisoma kwa shida na kufanikiwa kupata elimu ya Sekondari na kisha kujiunga na mafunzo ya ualimu katika chuo cha Marangu na kuhitimu kwa kutunukiwa Daraja A. Baada ya kuhitimu nilipangiwa kituo cha kazi ni huko Kwamsisi mkoani Tanga katika shule ya msingi Kwamsisi.

Nilivyofika nilishangazwa sana na mazingira ya shule na kijiji kwa ujumla. Kwanza nilipokelewa na wazee wa kijiji walio nionya sana kuhusu kile kijiji, wakaniambia niwe makini. Mzee mmoja aliyejitambulisha kama mzee Kingalu akanipatia kipande cha mfupa na kuniambia kuwa ni lazima nilale nacho ili niweze kuwa salama.

Niliogopa sana, nilipelekwa kwenye nyumba ya walimu ilikuwa ni nyumba ya bati iliyojengwa kwa kuta za miti na kusilibwa vizuri kwa udongo pia iliezekwa kwa bati. ilikuwa ni nyumba yenye hadhi kwa eneo hilo kwani asilimia kubwa ya nyumba za pale kijijini zilikuwa ni nyumba za udongo na kuezekwa na nyasi.

Siku ya kwanza nilipoingia shuleni ili niweze kutambulishwa nilishangazwa sana na mazingira yalivyokuwepo. Wanafunzi walikuwa ni wengi mno na walimu tulikuwa watano tu, ilikuwa ni mimi na mwenzangu wa kike tulioripoti ndani ya wiki hiyo pamoja na walimu wengine watatu akiwemo mzee mmoja mstaafu aliyeombwa kuhudumu hapo shuleni.

Siku niliyoripoti walimu wenzangu walinishangaa na kunionya kuwa kama sikuwa na kinga yoyote basi hapo kijijini sito paweza. Mimi niliwajibu kuwa siamini kabisa kwenye nguvu za giza na ninaimani kwa Mwenyezi Mungu kuwa ndiye atakaye nisaidia kwani mimi ni mkristo Mkatoliki. Nikatambulishwa mbele ya wanafunzi na mimi nikajitambulisha.

Siku hiyo nilifanya maandalizi kadhaa kwa ajili ya kipindi na kisha kuanza kazi yangu ya kufundisha. Siku za mwanzo nilishangazwa na umakini wa wanafunzi darasani, wengi walikuwa wakinitazama kwa makini na wengine walikuwa hawaongei wala kujibu chochote hata ukiwauliza maswali wakati wa kipindi, nilikuja kugundua kumbe walikuwa ni kama wamelala huku wakiniangalia kwa sababu ilikuwa hata nikiwashtua kwa kuwatingisha walibaki wakinitazama tu!

Nyumba yangu niliyopewa na uongozi wa Kijiji ilikuwa pembezoni kidogo na eneo la shule, na kama mnavyojua mazingira ya kijijini, nyumba ilikuwa pembezoni mwa kijiji. Siku moja nilivyokuwa nikirudi kutoka kazini, mtaani wakazi wengi walikuwa wakinitolea macho ya mshangao kama vile walikuwa wakinitamani sikuelewa hawakuniongelesha kwa lolote na nilivyo wasalimia wengi wao hawakunijibu walibaki tu wakinitazama! Niliwaona baadhi yao wakininyooshea vidole kama vile wanaelekezana kitu, mimi nilitembea haraka haraka kuelekea yalipo makazi yangu.

Nilifika nyumbani kwangu, vile naufungua tu mlango nilishangazwa kuona mnyama kama panya akitoka ndani ya nyumba yangu kwa kasi kubwa sana kupitia mlango mkuu wa kuingilia sebuleni, alikuwa amebeba mfupa! Nilishtuka sana baada ya kuingia chumbani kwangu na kuukosa ule mfupa niliopewa na mzee Kingalu, nikatambua kwamba uliondoka na yule panya niliyepishana naye pale mlangoni.

Nilivyofika ndani kwangu nikafanya utaratibu wa kuandaa chakula na baada ya kula nikajipumzisha kitandani na kupitiwa na usingizi totoro. Nilishtuka niliposikia jina langu likiitwa, "Soka! Soka!" hapo kijasho chembamba kikanitoka na nilipotazama mlangoni ulikuwa ni mwanga mkali sana na sikuweza kuona kitu chochote nikafikiria ni nani huyo aliyekuwa akiniita kisha nikaisikia tena ile sauti, na mara hii kwa mtetemo.

"Wewe ni mgeni hapa kijijini Kwamsisi, ila umewakasirisha wavyele(wazee wa kimila) kwani ulijiwekea zindiko la mfupa bila ruhusa ya wavyele. kwa hiyo mambo yatakayo kupata ni makubwa mno!"

Mimi nikawajibu kuwa ule mfupa nilipewa tu na mzee Kingalu na wala yeye hakuniambia kama ni zindiko hata hivyo jana nilivyo rudi kutoka kazini sikuukuta ule mfupa kwa hiyo kama ni zindiko mimi sina. Yule mtu akacheka sana na kuniambia kuwa yule panya niliyemuona sio panya wa kawaida bali ni mtaalamu wa kutegua mabomu ya kichawi, kisha ile sauti ikapotea na hapo mimi nikashtuka kutoka usingizini. Nilihisi kuwa huwenda ikawa ni ndoto tu iliyokuwa ikinisumbua japokuwa nilikuwa naogopa sana nilichukua biblia yangu nikalala nayo huku nikisali rozali.


Pia, soma: Sitosahau yaliyonipata kijijini Kwamsisi-2
Kusoma Biblia peke yake ,kusali Rosary na kuwa Mroma kusinge-kusaidia kabisa mkuu.
1.Ulipaswa kumkiri Yesu kuwa Bwana na Mwokozi was maisha yako
2.Kusoma na kuiishi Biblia,yaani Neno la MUNGU.
3.Kua na Roho Mtakatifu.Roho Mtakatifu unampata baada ya kukidhi vigezo 1 na 2 na kumuomba MUNGU akupe.
4.Kudumu katika maombi.

Hizo ndizo initial very important tools ambazo unahitaji ili kumshinda Shetani.Short of that you are an easy target for the Devil.
 
Sasa hapa wewe ndo umeonesha una stress. Hizi stories why zinawatoa imani hivyo? Sisi wengine tunakuja humu kutafuta wa kuwatoa makamasi na kuamsha stress zao tuna enjoy. Tafuteni kazi shauri lenu. Mtakuja olewa na watunzi kwa stories tu. Mwacheni mtunzi atunge kwa utulivu
Wewe kenge kiboko yako ni Omughaka tu ulimkatisha tamaa lkn mwanaume wa kikurya alisimama imara akamalizia story yake
 
Wewe kenge kiboko yako ni Omughaka tu ulimkatisha tamaa lkn mwanaume wa kikurya alisimama imara akamalizia story yake
Utakuwa ulitembea na omugaka wewe. Nyie wanawake wa humu hamtulii kabisa. Mnaliwa kipuuzi tu. Umewapenda wanaume wa kikurya? 🤣 Angalieni mtakufa kwa ukimwi.
 
Utakuwa ulitembea na omugaka wewe. Nyie wanawake wa humu hamtulii kabisa. Mnaliwa kipuuzi tu. Umewapenda wanaume wa kikurya? [emoji1787] Angalieni mtakufa kwa ukimwi.
Bora Mimi kuliko wewe ambae muda wote unawaza post za wanaume wako humu huwezi kukaa ukaja na Uzi wako kazi kuvalia shanga thread za wanaume humu[emoji23]
 
NASHAURI MWANA JF YEYOTE ASIMUUNGE HUYU MTOA HADITHI MPUUZI SANA ANATAKA MAMBO YA PM PM KAMA AMESHINDWA KUSIMULIA KIHADITHI CHAKE TUACHANE NAE AKAFIE MBELE NA STORY YAKE.

WAPO WATU HUMU KAMA AKINA "UMUGHAKA" WAMETOA STORY ZAO HALISI ZENYE EPISODES SIJUI MPAKA ZA 60 HUKO MPAKA ZINAISHA BILA HATA KUDAI AU KULETA PROMO YEYOTE SIJUI NJOO PM.
SASA HUYU MPUUZI ANALETA STORY HATA EPISODE 10 HAJAFIKA ANALETA MAMBO YA PM.

Nimeandika kwa herufi kubwa kuona huyu jamaa anataka asumbue watu hapa. Hatuhitaji story yako
Tamaaa
 
NASHAURI MWANA JF YEYOTE ASIMUUNGE HUYU MTOA HADITHI MPUUZI SANA ANATAKA MAMBO YA PM PM KAMA AMESHINDWA KUSIMULIA KIHADITHI CHAKE TUACHANE NAE AKAFIE MBELE NA STORY YAKE.

WAPO WATU HUMU KAMA AKINA "UMUGHAKA" WAMETOA STORY ZAO HALISI ZENYE EPISODES SIJUI MPAKA ZA 60 HUKO MPAKA ZINAISHA BILA HATA KUDAI AU KULETA PROMO YEYOTE SIJUI NJOO PM.
SASA HUYU MPUUZI ANALETA STORY HATA EPISODE 10 HAJAFIKA ANALETA MAMBO YA PM.

Nimeandika kwa herufi kubwa kuona huyu jamaa anataka asumbue watu hapa. Hatuhitaji story yako
Maku yake kabisa huyu
 
Wakuu, kama vipi nipeni ruhusa me niendeleze hii chai
 
Back
Top Bottom