Sitosahau yaliyonipata kijijini Kwamsisi

Mijitu kama hii niyakupigwa ban ya maisha sijui hawa mods hawaonagi haya malalamiko.
 
Umequote kutoka wapi hii?
 
Wewe ni tapeli na tunakuchukulia hatua uondolewe humu ndani... unataka kujifaidisha na kazi za watu wengine. Hii aikubaliki .
Umekosa kazi, na rafiki yako chizi maarifa. I am reputable and known writer of JF.
 
Hiyo dawa ya ndele nilishawahi kuitumia ni noma aisee niliipata bumbuli huko, nilihadithiwa sikuamini nikaamua kwenda kuijaribu yaani wanawake wanakuwa kama mazezeta ukimtamani tu anakufata na kujichekea chekea unaweza kumpeleka popote...
 
SEHEMU YA 10

"Haiwezi kuwa kirahisi huyu kijana ametuingilia vya kutosha sasa haina budi tumfanyizie!" Mzee Samasimba na vijana wake Mbwana na Jumanne waliketi kwenye kikao kizito wakinijadili mimi. Hao vijana walikuwa wakiogopwa sana pale kijijini, mabingwa wa kuroga kuanzia zongo mpaka kutupiana mashakizi. Mashakizi ni majini yanayotumwa kukusababishia kifo kisichotarajiwa, mfano unaweza kupata ajali ya basi ukafa kumbe sababu ni za kichawi na hii inatokana na mashakizi utakayo tumiwa.

Taarifa za vikao vyao nilizipata kwakuwa nilikuwa nikioteshwa kila kitu walichokifanya niliona mchezo mzima na hapo nikapanga namna ya kujiokoa. Siku hii usiku niliota ndoto ya kutisha, nimesafiri kwenda mjini Tanga kikazi wakati wa chakula watu wengi tulikuwa tumekaa pembezoni ya maegesho ya magari ya mizigo, lilikuwepo lori la mizigo lililokuwa limepaki hapo kwahiyo sisi tulikuwa tumekaa kwa pembeni yake kufumba na kufumbua niliona lile kontena likichomoka na kutuangukia na kutufunika watu wote tuliokuwepo mahali pale, nilishtuka kutoka ndotoni.

Ni ndoto ambayo ilinisumbua sana ingawa sikumwambia mtu yeyote na baada ya wiki nilipokea barua ya mwaliko wa kuhudhuria semina ya walimu wa masomo ya sayansi katika jiji la Tanga na kweli nilipofika niliyaona mazingira kama yale niliona lori la mizigo likiwa limeegeshwa sehemu ambayo waalimu walikuwa wakigawiwa chakula, nilihisi kitu hakiko sawa nami sikusogelea kabisa eneo hilo mara baada ya kuchukua chakula nilikaa mbali ya eneo hilo huku nikishuhudia jambo litakaloweza kutokea.

Kufumba na kufumbua niliona lile kontena likianguka kwa haraka na kuwafunika walimu wote waliokuwapo pale kwa chini wengi walijeruhiwa na baadhi yao kupoteza maisha niliogopa sana nikamshukuru Mungu kwa kuniepusha na jambo hilo. Baada ya tukio hilo nilishangaa nilipopigiwa simu na watu ninaowafahamu kutoka kule kijijini wakiniambia kwamba taarifa zimesambaa kuwa mimi ni mmoja wa walimu waliofariki kwenye ajali hiyo, nilishangaa! Baada ya kufanya uchunguzi niliambiwa watu waliokuwa wakisambaza taarifa hiyo hawakuwa wengine bali ni wale vijana wa mzee Samasimba Jumanne na Mbwana.

Nilirudi nikafika kijijini usiku. Sitti alikuwa na kawaida ya kuja kunipokea pindi nitokapo nje ya mji na siku hii nilimletea zawadi aliyokuwa akiipenda, lotion ya Swetheart pamoja na perfume ya Kulthum. Nilitembea mpaka nyumbani kwangu na kuingia ndani, nilisikia miguno ya kimapenzi ikitokea ndani ya nyumba yangu."Kuna nini tena humu?!" Nilishtuka kwasababu funguo za nyumba yangu nilimkabidhi Sitti nilivyo ondoka kwenda mjini Tanga. Niliporudi sikuona umuhimu wa kumjulisha kwamba ninarudi nilitembea taratibu mpaka nyumbani kwangu na baada ya kusikia sauti hizo nilichungulia kupitia dirishani, kuna mambo ya kiutu uzima yalikuwa yakiendelea chumbani kwangu.

Sitaki kuamini kile nilicho kishuhudia usiku ule, ilikuwa ni kweli na wala haikuwa ndoto kama nilivyotaraji iwe. Sitti alikuwa akivunja amri ya sitta na Mbwana tena mbaya zaidi alikuwa akifanya kitendo hicho ndani ya nyumba yangu kwenye kitanda changu. Niligonga mlango kwa nguvu wala hawakufungua, nikaufungua kwa funguo za akiba nilizokuwa nazo. "Lahaula lakwata!" Niliwakuta wakiwa kama walivyo zaliwa wakivunja amri ya sita juu ya kitanda changu. "Sitti ni wewe ama ninaota!" Walishtuka, "Hee Soka, ni wewe ama ni mzimu wako?!" wote wakawa wakinitazama.

"Nilijua umesha fariki kwenye ajali kumbe bado u mzima!" Walikukuruka wakashindwa kuachiana nilichukua fimbo nikawatandika haswa nilimtandika zaidi Mbwana kwasababu nilikuwa na hasira naye lakini alijaribu kukukuruka hakuweza kutoka kwani nilikuwa nimezindika kichawi. Baada ya kuwapa kipigo hevi na kuridhika ndipo nilichomoa kisu kwenye ala niliyokuwa nimeificha kwenye kona ya chumba changu basi wakaachiana. Sikutaka kuwaona kabisa mbele ya macho yangu, niliwafukuza. Pamoja na uchawi wake wote, Mbwana alikuwa mdogo kama piritoni kwasababu ukifumaniwa huwezi kuwa na nguvu zozote, hata kama ukiwa na nguvu za kichawi unashindwa kuzitumia ili kujitetea.

Japo nilimpenda Sitti na kujitesa kwa ajili yake lakini nilikuja kuamini kwamba wanawake sio watu wa kuwawekea mdhamana. "Sitti nilimuamini mpaka kudiriki kumuachia funguo ya nyumba yangu lakini leo hii ameamua kunifanyia usaliti wa wazi kabisa," nilijisemea mwenyewe kwani niliumia sana moyoni. Sikutaka kumwambia mtu yeyote juu ya jambo hili nilijua itakuwa aibu kubwa ila akilini niliapa kulipa kisasi.

Siku hiyo sikulala kitandani nilikuwa nimekaa pale nje kwenye kizingiti nikiwaza sana mpaka usingizi uliponipitia na cha ajabu nilishtuka usingizini nikiwa nimelala kitandani kwangu milango yote ikiwa imefungwa. Nilishtuka kusikia harufu kali ya marashi ikiwa imesambaa kwenye kile chumba na hapo nikamuona mwanamke mrembo mweupe pe' na mwenye nywele ndefu zilizofika mpaka kwenye kiuno chake na alikuwa na macho maangavu yaliyoingia ndani.

Alikuwa amesimama mbele yangu akinitazama huku yupo uchi wa mnyama. "Ondoka kwangu kaa mbali na mimi, kwani wewe ni nani nilimhoji!" "Naitwa Maimuna nimetoka kwenye kina kirefu cha bahari nimekupenda sana jinsi ulivyo na pia nimependa ujasiri wako, nilimtazama mwanamke yule kuanzia juu mpaka chini nilistaajabu nilipoziona kwato zake mithili ya farasi zikiwa zimechomoka kwenye miguu yake nikapatwa na kigugumizi.

Yule kiumbe akaondoka, nilimtazama akitembea vishindo vya viatu virefu vilisikika vikipotelea mbali ya upeo wa akili yangu na sauti ya mlango ukafungwa kwa kishindo kikuu! Nilishtuka kwenye ndoto ile na jasho jingi lilikuwa limenitoka mpaka kulowesha mashuka, nikweli nilikuwa nimelala kitandani kwangu na milango yote ikiwa imefungwa sikuelewa kivipi yule kiumbe alipita mpaka kuweza kuingia na kutoka ndani ya nyumba yangu. Baadaye nilikuja kutambua kuwa majini ni viumbe wenye uwezo mkubwa wa kuweza kupenya ama kupita kwenye maeneo yenye vizuizi vya kila aina kwa sababu kikawaida viumbe hawa hawana mwili wa kibinadamu na huweza kuvaa umbo na mwili wa kiumbe chochote kile wakitakacho.

ITAENDELEA...

Sitosahau yaliyonipata kijijini Kwamsisi-11
 
Mambo mazito
 
Hili jamaa kichwa ngumu
 
Usinifundishe uandishi, wewe kama unajua kukosoa si uandike story yako hata moja tuione, mimi ni mwandishi wa vitabu, sio hizi episode za JF. Kwa wanaojua umuhimu wa uandishi wamesha nifuata PM, watu kama wewe hawanisumbui, ushauri peleka angaza.
Kuandika vitabu kusikuvimbishe kichwa sababu vitabu sio ishu tena kila popoma anajiandikia na kuchapa tu. So, unaweza kuwa na kitabu na ukawa popoma tu
 
Unatapatapa sana dogo reputable writer
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…