Sitosahau yaliyonipata kijijini Kwamsisi

Sitosahau yaliyonipata kijijini Kwamsisi

Hapana mkuu utakuta mtu swala 5 afu ni anaswalisha au anamiliki msikini ila ni mganga wakinyeji au watu wana mtuhumu kuwa ni mchawi
Kwa wakristo haiwezeka ila washirika washirikina wapo ila wanajificha sana
Ni kwamba ushirikina ni mpana mwamposa mshirikina ,lusekelo ,sijui mlima wa moto wote ni washirikina.

Maji ya upako wote washirikina ..sawa ni waganga wavaa suti wanaojiita manabii wote ni washirkina.

Wanaoabudu masanamu ni washirikina.

Ushirikina mpaka usome sana ndo utajua ukienda kukiri dhambi mbele ya binadamu mwenzio ni ushirikina pia.
 
hajui kuwa Mtu swala tano swafii na anafuga majini
Unaweza kuswali ila kwa kuwaongopea wanadamu tu ila kwa Mungu huswali kabisa ni mnafiki.

Ukisikia mtu anafuata swalah zote ina maana hizo swalah zinamkataza kutenda maovi yaani kama bado anafanya hayo maovu bado swalah zake hazikubaliki.

Ukiwa mshirikina ,mwizi ,mzinzi ,tapeli na mambo yote ya hovyo basi hauna swalah mpak uache hayo mambo.

So mshirikina hafuati swalah ila anajidanganya.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Nimesema uongo? Mapema tu mimi nlimuonya dogo kuwa anazidisha sana chumvi itakuwa ngumu huko mbeleni. Mkaanza nishukia. Mkaona mimi nawanyima nafasi ya kusoma hadithi ambayo mnaambiwa ni kweli kumbe ya kutunga. Uchawi upo ila si kwa kiwango anachosema mtunzi. Sema watunzi wengi wamejua JF wanapenda stories za Kichawi sana.
 
NB: Kutokana na ubusy wa kazi, hadithi hii itaishia hapa ila kwa atakayetaka muendelezo wake namkaribisha PM, kwa vitabu mbalimbali vya hadithi na mikasa ya kweli na story za audiobooks
Yamekuwa haya tena.🙌😂😂😂

So PM hauko busy mkuu???

Bora tu ungeendelea hapa hapa ukaweka tu na namba wenye nia ya kukuunga mkono kwa chochote tungefanya hivyo. Vinginevyo tumekuona ni mbabaishaji.
 
Wadau nipo busy kidogo mambo yamebana. Ndo maana muda unakosekana. Ila nimeweka namba ya simu. Nicheck kwa hiyo namba nitakupatia visa vingine.
 
SEHEMU YA 3

Mwalimu mkuu alituita kikao kilikuwa ni kikao kizito kujadili ujumbe ulioletwa na mzazi mmoja kwenye karatasi iliyokuwa imefungwa kwenye bahasha ya khaki alionekana kuwa akitetemeka na hakuwa sawa kisaikolojia, mimi nilikuwa ndio kwanza nikisahihisha madaftari huku nikibadilishana maongezi na mwalimu huyu wa kike aliyetokea kuwa karibu sana na mimi nilishtuka kumuona mwalimu mkuu akiwa kwenye hali ile.

"Walimu habari za mchana?" Tulikuwa walimu wanne wote tulitahamaki na hakuna hata mmoja aliye jibu wote tulikaa kimya. Siti akajibu, "nzuri." Sauti yake ikasikika kwa wote nasi tukarudia tena "nzuri." "Inaweza kuwa ni nzuri kwenu au la mmejibu kwa mazowea tu lakini kuna vita kali sana inayoendelea kati yetu haswa kwa nyinyi walimu wageni, inaonekana mmeshindwa kabisa kuheshimu wazee wa kijiji hiki, mzee Sa-Masimba ameleta barua hii amemtuma mwanaye ailete barua hii imenitisha kidogo kuisoma japo sijaielewa lakini ina alama ya damu.

"Alama ya damu?!" wote tulihamaki. "Ndio ni damu ya halisi kabisa ni kidoti kimewekwa juu ya bahasha kikiwa kimechovywa kama na kidole cha mkono, inaonekana kuna mtu anawindwa hapa je ni nani anayewindwa na kwanini?" alihoji mwalimu mkuu.

Barua ilisomeka, "Ndugu mwalimu mkuu hongera kwa kupata wafanyakazi wapya lakini sidhani kama vijana hao uliwafunza juu ya mila za kwetu, kuheshimu wazee na kuto jiingiza kwa namna yoyote na mipango ya kujaribu kupambana na wazee wa kimila, kama hiyo haitoshi kutengeneza wigo na kujiona kuwa huingiliki kwetu sisi tunahesabia kwamba ni dharau. Kama wameshindwa kutuheshimu japo kwa salamu mpaka kufikia hatua ya kupambana na sisi ki chawi hakika hatuta waacha salama." ilimalizika shemu ya barua hiyo.

Nakumbuka siku hiyo tuliwaruhusu wanafunzi mapema sana ilikuwa kama mchana wa saa nane hivi. Mimi nilijua fika ndiyo mlengwa mkuu hivyo niliogopa sana tulitembea mpaka kwenye nyumba ya Mzee Samasimba tulivyo karibia tu tulipiga magoti huku tukitembea kwa magoti mpaka tulipoufikia mlango wa nyumba yake, mwalimu mkuu akiwa ametangulia mbele. Mzee mwenyewe hatuku mkuta basi wakatumwa watoto kwenda kumwita alikuja huku akiwa amevaa msuli wake kiunoni aliambatana na vijana wengine wawili mmoja alimtazama sana Siti kisha akaendelea mpaka wakaingia ndani mzee alisimama pale nje mkewe akamletea kigoda(kiti cha kukalia), akakaa kutusikiliza.

Mwalimu mkuu alikuwa ametangulia mbele aliongea naye kwa lugha ya Kizigua na mwisho aliinama sana huku akimwomba msamaha. Kwakweli nikiri wazi kwamba sikuwahi kushuhudia mchawi akiabudiwa kama siku hiyo, huyu mzee inasemekana alikuwa moja kati ya wazee wenye kauli sana pale kijijini, mambo mengi yalikwama endapo tu yeye asinge shirikishwa na kukubaliana. Ilifika zamu yangu ya kumwomba msamaha kwani tulimwendea kwa zamu, niliinama na kupiga magoti na kusema shikamoo mzee Masimba mimi ni mgeni hapa kijijini naomba unisamehe kama nilikukwaza kwa namna yoyote, sikumpa mkono kama wenzangu walivyofanya niliogopa kuchukuliwa nyota.

Tuliondoka baada ya kupakwa usembe(unga mweupe) usoni na kichwani na wale vijana wake, tulidhalilishwa sana siku hiyo hamna siku nilichukia kazi hii ya ualimu kama siku hiyo tulirudi nyumbani kila mtu akiwa kimya hamsemeshi mwenzake, nilitembea huku nikiwa na mawazo mengi macho yangu yakitazama chini huku machozi yakinilengelenga. "Kwanini binadamu anaabudiwa kama Mungu!" niliwaza moyoni ilikuwa yapata majira ya saa kumi nambili jioni ikikaribia saa moja usiku, nilishtuka kumuona Siti akiwa amenishika bega la kulia kwa nyuma niligeuka na kumtazama.

"Kwahiyo ndio unaenda nyumbani, uende salama ila uwe makini, hapa ndio Kwamsisi uache ubrazameni uheshimu watu." Kumbe ile hali yangu ya kujitengetenga na kutosalimia watu iliwaudhi wengi pia kujiweka karibu na mzee Kingalu ilikuwa ni hatari kwangu niliogopa kuiendea ile njia inayokwenda nyumbani, nilipokumbuka lile jicho alilonikata mzee Masimba nilipogoma kumpa mkono wa msamaha kwa kuwa sikutaka kushikana mkono na mchawi. Basi nikajua kuwa usiku huo lazima atanijilia nyumbani kwangu.

ITAENDELEA...

Sitosahau yaliyonipata kijijini Kwamsisi-4
Picha lingeanza kwa kugoma kutembea kwa magoti na kugoma kuomba msamaha.
 
Nimesema uongo? Mapema tu mimi nlimuonya dogo kuwa anazidisha sana chumvi itakuwa ngumu huko mbeleni. Mkaanza nishukia. Mkaona mimi nawanyima nafasi ya kusoma hadithi ambayo mnaambiwa ni kweli kumbe ya kutunga. Uchawi upo ila si kwa kiwango anachosema mtunzi. Sema watunzi wengi wamejua JF wanapenda stories za Kichawi sana.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Ulisema kweli tulikupinga huwa unaona mbali

Sasa me nauliza pm tunaenda bure au na hela hajanyoosha maelezo vizuri
 
Vipo vitabu vya hadithi za kutisha kwa yeyote atakaye hitaji hadithi ni za ukweli na nyingine za kubuni, kwa stori hii nitaishia hapa hopefully mnaenjoy na kujifunza pia, napokea maoni kupitia private messages (PM).
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
SEHEMU YA 9

"Soka unaenda wapi mbona unaniacha mwenyewe?!" Sitti aliniita nikiwa ndio kwanza naelekea nyumbani kwangu kujipumzisha baada ya kumfikisha pale alipokuwa akiishi. "Naenda zangu nyumbani, kwani we' si nimesha kufikisha kwenu? lala upumzike." "Tafadhali nisubiri!" alisema. Hapo mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio, sikuwa na mazowea ya kihivyo na huyu binti nilimheshimu kama mwalimu mwenzangu tu na si vinginevyo.

Alinifuata akanikumbatia na kunibusu. Nami sikuwa mnyonge nilimpokea na ndani ya muda mfupi tukawa tukibadilishana mate alining'ang'ania, nikaona isiwe kesi nikamtoa kwanguvu kifuani kwangu. "Sikiliza Sitti, nenda kalale tutaongea kesho tusije kuyazusha mengine kwa sasa." Nilimuaga na kumbusu kwenye paji la uso wake kisha nika muangalia jinsi alivyogeuka mpaka alipoingia ndani ndipo nikatoka kwa kasi kuelekea nyumbani kwangu.

Nakumbuka siku zile nilikuwa nikiwindwa sana haswa nikiwa kazini ama nyumbani, ilikuwa ni ngumu kulala nyumbani kwangu mara kwa mara nilikuwa nikilala kiwizi wizi, hata wanafunzi wengine walikuwa wakitumwa makusudi kunijaribu wakinitafutia sababu ili waende kuwaeleza wazazi wao. Nilijitahidi kuwa makini juu ya hilo nilifanya yale yanayo nihusu tu. Mapenzi yangu kwa Sitti yalizidi kushamiri ingawa nilikuwa bado nikiwindwa sana.

Mzimu wa mzee Kingalu nao haukuacha kunisumbua, lakini kuna kitu kimoja ambacho kilinishangaza kwani ilikuwa kila nikilala nyumbani kwangu nilipata amani ambayo sikuitarajia kabisa yale mauzauza niliyokuwa nikiyaona mwanzoni yaliisha kabisa, baadaye nilikuja kugundua kwamba kuichimbia ile hirizi pale ndani ndio ilikuwa sababu ya yote, wachawi walishindwa kusogelea pale ama kufanya lolote nikiwa ndani ya ile nyumba.

Wachawi wanautaratibu wao pindi wamchukuapo mtu kichawi, husubiri kwanza kwa muda wa siku 40 kuona kama kuna vita yoyote ama ufuatiliaji wowote na hapo ndipo wangeweza kufanya maamuzi ya au kumla nyama ama kumgeuza msukule moja kwa moja. Sababu nyingine iliyo wachelewesha ni kutokana na ukweli kuwa mzee Kingalu alikuwa ni mchawi mwenzao tena mwenye daraja ya juu sana, kuna tetesi walisema kuwa alikuwa akifuga majini akiyafungia kwenye chumba maalum katika moja ya nyumba zake.

Kuna siku uongozi wa kijiji akiwemo mwenyekiti, afisa mtendaji pamoja na mwalimu mkuu walifika shuleni wakatuonya sana walimu juu ya kujihusisha na mambo yaliyo kinyume na taaluma zetu, mlengwa mkubwa alikuwa ni mimi na nilipewa barua ya onyo, ingawa nilijaribu kujitetea kwamba wanakijiji hawana urafiki na walimu na wala hawatupi ushirikiano zaidi ya kutuibulia vikwazo kila uchao. Viongozi hao hawakunielewa na walinitishia kunifukuzisha kazi, ilibidi niwe mpole na kuwakubalia yote waliyo yasema.

Siku moja usiku yule mganga alinijia akaniamsha na kuniambia nimfuate, ilinibidi nivae kama yeye nilivua kila nguo na kisha kuvaa kaniki nyeusi kwa mtindo wa lubega, aliniletea vazi hilo, alitaka kunitembeza na kunionyesha maajabu ya usiku. "Vaa bangili yako," alisema, nami nikaivaa kwenye mkono wa kulia, niile bangili yenye uwezo wa kuona vitu visivyoweza kuonekana kwa macho ya kawaida. Tulitembea mpaka eneo la makaburi kisha tukakaa kimya kwa pembeni mbali kidogo ili kuweza kushuhudia yatakayo tokea.

Baada ya muda wachawi walianza kuingia hapo kila mmoja kwa usafiri wake wapo waliotua kwa ungo na wapo waliotua kwa kutumia fisi na wengine kuja mithili ya kimbunga. Niliweza kushuhudia live bila chenga, basi baada ya muda nikaona yule kiongozi wao (Mzee Samasimba) amesimama kwenye kaburi lililokuwa jipya upande wa kichwani akiwa ameshika zana zake za kazi na baadaye akatokea bibi mmoja na fimbo ndefu akapiga juu ya lile kaburi na hapo maajabu yakatokea.

Mwili wa binadamu ulipanda kutoka chini ardhini mpaka juu ya lile kaburi, waliuchukua na kisha kuugawanya na hapo kulikuwa na moto mkubwa sana waliweza kuichoma ile nyama ya binadamu na nilishuhudia yule bibi akiwalisha wachawi wenzake kwa mtindo wa kuwarushia kipande kwa kipande nao hudaka kwa kutumia mdomo wao, ni kosa kubwa unaporushiwa kipande cha nyama nawe ukashindwa kukidaka, hii ilitafsiriwa kama ni dharau kwa chama chao wanacho kiabudu. Asilimia kubwa ya wachawi ni watu wa kawaida lakini matukio wanayo yafanya ni ya aibu mno.

Tuliondoka na mganga tukatembea mpaka alipokuwa nyumba ya mzee Samasimba, tulitaka tufanye tukio la hatari, tulifika na kuukosa ulinzi kabisa kwani yule mzee alikuwa yupo kwenye sherehe za kichawi, lakini kumbe nyumbayake alisha izingira na nguvu za giza na kulikuwa na mitego aliyoitega kwamba endapo kuna mtu atakaye kuja nyumbani kwake basi yeye ni lazima angejua. Tulipita kwenye banda la uwani ni banda lililozungushwa kwa majani ya mnazi baadaye mimi nilibaki pale nje mganga alizama ndani kichawi. nilimsubiri kwa muda mrefu kidogo.

Alitoka na kabla hatujapotea ki miujiza alimwaga dawa za kuondosha ushahidi. "Nimesha muweka humu kwenye hii tunguli," akimaanisha ameuweka mzimu wa mzee Kingalu kwenye kile kibuyu, tulitoka kwa tahadhari kubwa na mara tulisikia vishindo vikubwa na kelele ya kuunguruma, ilikuwa ni kelele ya mzee Samasimba baada ya kurudi kwenye sherehe zao za kichawi, kwani huyu mzee akikasirika hutoa muungurumo kama wa mnyama Simba na hii ndio sababu walimpa jina la Samasimba. tulipotea na kukimbia kila mtu kwa njia yake.

USISITE KUANDIKA MAONI...
(NB: Kutokana na ubusy wa kazi, hadithi hii itaishia hapa ila kwa atakayetaka muendelezo wake namkaribisha PM, kwa vitabu mbalimbali vya hadithi na mikasa ya kweli na story za audiobooks.)
Uzuri nilishajua unawarushia watu mahindi ili wajae kapuni uwavune.
Uzuri zaidi members wa JF nao wana uzoefu mkubwa wa kuishia njiani kwenye hadithi nyingi. Hapo walipo ukute wameshangaa hata kufika hadi hiyo sehemu ya 10 wakati walijiandaa kuishia sehemu ya 3.
 
Sina stori niliyowahi kuimaliza JF nikiona Itaendelea naishia hapo.
Ukiamua kuleta stori iandike kabisa yote iishe ukija unakimbiza mwanzo mwisho kama Deepond. Mambo ya kutuambia watu wazima itaendelea ni ukahaba
 
Ni kwamba ushirikina ni mpana mwamposa mshirikina ,lusekelo ,sijui mlima wa moto wote ni washirikina.

Maji ya upako wote washirikina ..sawa ni waganga wavaa suti wanaojiita manabii wote ni washirkina.

Wanaoabudu masanamu ni washirikina.

Ushirikina mpaka usome sana ndo utajua ukienda kukiri dhambi mbele ya binadamu mwenzio ni ushirikina pia.
Nilijua tu lazima uje kutetea tanga yako ndo maana nimesema sisi wakristo kama unafanya utafanya kwa sili sana kwa sababu dini yetu inakataza

Ila salama leko na ushirikina hauwezi tofautisha, mtu unaswali swala 5 afu unamganga wako au mganga wa familia
Kwetu sisi ni mwiko
 
Nilijua tu lazima uje kutetea tanga yako ndo maana nimesema sisi wakristo kama unafanya utafanya kwa sili sana kwa sababu dini yetu inakataza

Ila salama leko na ushirikina hauwezi tofautisha, mtu unaswali swala 5 afu unamganga wako au mganga wa familia
Kwetu sisi ni mwiko
Wakristo wa maji ya upako na ushirikina huwezi kutenganisha.

Kutubu dhambi kwa mchungaji ni ushirikina.

Kuita yesu ni Mungu badala ya Mungu mmoja ni ushirikina.

Ukristo kwa ujumla ukiamini tu ni mshirikina.🤣🤣
 
Back
Top Bottom