Siungi mkono watu Kumchukia Diamond kisa aliipigia kampeni CCM

Ndugu yangu kwani kuna ubaya gani wanaharakati wa CCM nao wakaanzisha harakati za kupigia debe achukue hiyo tuzo? Si kila mtu na maamuzi yake?
 
Ni tabia moja mbaya sana kurithi adui wa mtu - J.M. Kikwete
 
Mkuu hata wakimchukia haimpunguzii chochote Domo, hizi ni kelele za vyura hazimzuii tembo kunywa maji. Kura hazipatikani au hazikosekani sababu ya eti Domo kuuinga mkono CCM, Roma yeye anashabikia Chadema na sijasikia kuwa kwa kushabikia kwake basi Roma asusiwe na wana CCM. SACCOSS ya Kaskazini hawana la kufanya sasa wamebidi waanze kumwandama Domo badala ya kutangaza sera zao ,siku hizi kuna suluhu na uhuru waliokuwa wanadai haupo sasa upo sasa hawana cha kusingizia wamebaki kumlaumu Domo, hovyo sana hawa wana SACCOSS
 
Good point ni kwamba atakae mpigia apige na ambae hatompigia akapiga kwa mtu mwingine apige.kutulazimisha tuwe na umoja kwenye Mambo ya kijinga ya tuzo alafu kwenye Mambo ya msingi hatuwi wamoja sio issue
 
Unasema CDM hawahusiki kwa hilo ila ni ukweli hao wanatumia nguvu waliyoipata CDM kishawishi watu
 
Mahaba ni demokrasia 100%.
Hoja inaweza isiwe demokrasia kwani inaweza kuwa ni "hoja ya nguvu (mabavu/dola)".
Ewaaaaaaaaaahhh hapa ndio ninapo pataka mahaba yasemwe kuwa ni mahaba kama ni hoja isemwe hoja yenye mashiko, sio sehemu ya mahaba uje utudanganye kuwa hapo Pana hoja, lazima tukubane mbavu
 
Haya ndio matokeo ya kushabikia chama na kuwa kimbelembele. Aende Lumumba kuwaomba wampigie kura.
Kwani umelazimishwa kumpigia? kama hutaki mpigie umtakae, ila Diamond kampeni hawezi kuacha kupiga kisa nyumbu wananuna
 
Wanaomchukia Diamond ni masikini wa kipato kama hao kina HILDA NA JACOB wanaamini umasikini wao ni sababu ya mtu tajiri
 
Ata mimi naamini hivyo kwa hoja hii kuwa eti ni ccm sio kweli, maana kwenye kampeni Ata Alikiba alivalishwa kofia na JPM, hawa jamaa waseme wanachokitaka kwa Diamond
Ni umasikini mkuu.. Tz ukiwa na hela unachukiwa sana
 
Diamond toka zamani yuko ccm!

Kama ndio hivyo angekuwa ameshashuka zamani
 
Ewaaaaaaaaaahhh hapa ndio ninapo pataka mahaba yasemwe kuwa ni mahaba kama ni hoja isemwe hoja yenye mashiko, sio sehemu ya mahaba uje utudanganye kuwa hapo Pana hoja, lazima tukubane mbavu
Penye hoja ya nguvu (dola/mabavu) upande wa kwanza, weka mahaba upande wa pili. Inaitwa kulipa ubaya kwa wema!
 
Wewe kwa akili yako unafikri diamond hata asiposhinda atakuwa masikini kama wewe?

Ashinde asishinde atajijua yeye na familia yake ila akale alipoleka mboga,wewe na nzi wa kijani wenzako mpigieni kura kuanzia 7 June 2021,sisi tunaenda na BUNABOI.

Ndio kwanza Forbes imeweka historia ya kuwa na Bilionea anyeishi nyumba ya KUPANGA..... πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€
 
Mleta mada ni mpuuzi kama alivyo huyo kada mwenziwe wa CCM. Msanii yoyote anaeyejihusisha na ushenzi wa CCM ni mpuuzi
 
Ni kama vile wao, ukiwa mpenzi wa Konde Boy unaonekana msaliti...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…