Unaposhabikia chama Cha siasa au hata mpira. Kumbuka wapinzani wako hawatakaa kimya.
Juzi tu tumeona Kaiser Chiefs vs Simba, wanayanga walijitenga na Simba na walifurahia kupigwa kwao 4:0 kule SA.
Rule of thumb is ukiona Kuna Jambo limefanyika ndivyo sivyo kemea chama chake ili kujitenga na uovu huo.
Wengi mtakumbuka alichofanya Trump January 6, Mwaka huu Republicans wengi walijitenga na matendo Yale na kusema si ya chama Bali yake Kama Trump.
Sasa Kama Diamond aliamua kujiunga na CCM sio kosa na sidhani Kama anahukumiwa kwa Hilo. Bali matendo maovu ya CCM Diamond hajaonesha kuchukizwa nayo hivyo kumfanya yeye kuwa sehemu ya uovu iliyofanywa dhidi ya wapinzani wake na Sasa wanaonyesha hasira zao maana ndio sehemu pekee wanaweza kumbana Diamond.
Hivyo tukumbuke "Usimtendee mwenzako usichopenda kutendewa"
Wakati wa uchaguzi wakisema "....baba lao..... Kupambana Nasi ..... Chama lao...." Upande wapi nao wamejibu Burnaboy chama lao.
Wazee wa sauti ya Simbilisi