Siungi mkono watu Kumchukia Diamond kisa aliipigia kampeni CCM

Tukubaliane tu CHADEMA ni chama ambacho kama kitakuja kutawala hii nchi basi watakuwa hawana tofauti na utawala wa mwendazake kama hutaki mwingine ashabikie au akupinge hiyo demoklasia tunayoihubili ipo wapi sasa
Hii hali inashangaza na kutia mashaka sana juu ya mustakabali wa taifa hili.......
 
Wako huru kumsapoti yeyote kama wewe ulivyo huru kumsapoti diamond, halafu kama ni wanaharakati wa kisiasa wako sahihi kwanini unataka wamsapoti aliyeungana na watesi wao CCM kuwateka, kuwaua, kuwanyanyasa na kuwabeza kwa nyimbo zake?
Wamsapoti burnaboy Ila wasimcondemn diamond kisa anaipenda ccm

Kama walivyo na Uhuru wa kumpigia burnaboy hvyo ndivyo diamond ana Uhuru wa kuipenda ccm

Siipendi ccm hili lipo wazi

Diamond ahukumiwe kwa kazi zake sio kwa sababu ya kuipenda ccm

Uliberali uanze na hili
 
Huu ndio ukweli Kuna Agenda nyingine, hata hoja inayotumika ni dhaifu na haina mashiko, maana wasanii wengi walipigia kampeni ccm, tena cha kushangaza mwengine alijirecord live akilia kipindi JPM amekufa.
 
 
Uislamu unanasibishwa na ugaidi dunia nzima...je inafaa kuwaita waumini wote kuwa ni magaidi kwa kuwa wamechagua kuwa waislamu........??
Nimesema wazi kabisa kaungana na wauaji, ukishirikiana na gaidi lazima utaunganishwa tu cha muhimu jitenge nao.
 
Nimesema wazi kabisa kaungana na wauaji, ukishirikiana na gaidi lazima utaunganishwa tu cha muhimu jitenge nao.
Uuaji umeainishwa kwenye katiba ya CCM au ni utashi wa mtu binafsi ndani ya CCM.....??
 
Ahahaha umeona hoja zilivyo nyepesi, halafu wanataka Uhuru wa kutoa maoni, wakati Uhuru huo Ata wao umewashinda
Inaonekana hata hujui maana ya wimbo huo ‘Nakaa kimya’ ungeelewa maana yake wala usingechekelea, it means he doesn’t care about others pains.
 
Unaposhabikia chama Cha siasa au hata mpira. Kumbuka wapinzani wako hawatakaa kimya.

Juzi tu tumeona Kaiser Chiefs vs Simba, wanayanga walijitenga na Simba na walifurahia kupigwa kwao 4:0 kule SA.

Rule of thumb is ukiona Kuna Jambo limefanyika ndivyo sivyo kemea chama chake ili kujitenga na uovu huo.

Wengi mtakumbuka alichofanya Trump January 6, Mwaka huu Republicans wengi walijitenga na matendo Yale na kusema si ya chama Bali yake Kama Trump.

Sasa Kama Diamond aliamua kujiunga na CCM sio kosa na sidhani Kama anahukumiwa kwa Hilo. Bali matendo maovu ya CCM Diamond hajaonesha kuchukizwa nayo hivyo kumfanya yeye kuwa sehemu ya uovu iliyofanywa dhidi ya wapinzani wake na Sasa wanaonyesha hasira zao maana ndio sehemu pekee wanaweza kumbana Diamond.

Hivyo tukumbuke "Usimtendee mwenzako usichopenda kutendewa"

Wakati wa uchaguzi wakisema "....baba lao..... Kupambana Nasi ..... Chama lao...." Upande wapi nao wamejibu Burnaboy chama lao.

Wazee wa sauti ya Simbilisi
 
Inaonekana hata hujui maana ya wimbo huo ‘Nakaa kimya’ ungeelewa maana yake wala usingechekelea, it means he doesn’t care about others pains.
Nimekwambia yeye kakaa kimya maana anaogopa vita na watawala, ebu niambie Nani akukaa kimya Katika hao wasanii wakubwa?
 
Kwahiyo Diamond kukosa tuzo ndio mateso yao yataisha?
 
Thanks, Diamond hahukumiwi kwa yeye kuwa CCM bali kutokemea matendo maovu yaliyotendwa na chama chake.
 
Ukiwapinga wanatokwa na povu kubwa sana
Nimewafatilia sana hawataki kupingwa kabisa, ukiwapinga sana unachezea block, mimi nilimshangaa Kigogo badala ya kupambana na Niki wa pili, anamshambulia mke wa Niki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…