Siwezi kusahau haya manyanyaso ya mama wa kambo

Means binti alimbadilisha mama au mama alificha makucha ili apate ndoa?
 
Hata kama ana ugonjwa wa akili makofi mawili matatu huwa yanasaidia kureset mfumo.

Huwezi ukaniambia natembea na mzazi wangu nikae nakukodolea macho tu. Mungu aniepushe na hizi kesi asee.
Shida alikuwa na nguvu kuliko mimi na mimi nina kamwili kadogo kwahiyo kuwez kumpiga siyo rahisi
 
 
Kiukweli nilikuwa nikimchukia baba yangu, lakini sioni faida ya kufanya, nimeamua tu niache hayo maana kuna leo na kesho, nyie single faza jaribuni kuoa au kuishi na wanawake watakaowapenda watoto wenu, siyo unaishi na mwanamke unajua kabisa hampendi mwanao ila kwasababu wewe anakupenda unaganda nae hii siyo sawa.😪😪😪

 
Means binti alimbadilisha mama au mama alificha makucha ili apate ndoa?
Mama alificha makucha maana hata kuna mtoto wake alikuja mwanzoni walikuwa vizuri ila baadae anakuwa na mambo ya ajabu unaweza kumsalimia asiitikie au atafanya kitu uongee ili akuanzishie ugomvi
 
Wewe Dada mbona hadithi ya maisha yko inataka kufanana na yangu? Sema Mimi niliachwa na miezi 4😭 wanaume hakika angalieni wanawake wa kuoa hasa ukiwa umeachiwa mtoto/watoto wadogo...... Mungu bariki kila Mama aweze kulea mwenyewe uzao wake.
 
Miaka nasoma ukifika kidato Cha nne SoMo la kiswahili mada ya kwanza inaitwa UFAHAMU NA UFUPISHO, vp ulibahatika kusoma hiyo mada?
Sote tulifundishwa mada ya uandishi wa barua za kikazi. Hebu leo kamata graduate ye yote mwambie aandike barua siriazi ya kuomba kazi uone majanga yake. CV ndiyo kabisaaa!

➡️➡️➡️ Anyway. Binti Sayuni03 ana maumivu bado; na childhood trauma ni mbaya maana inaweza kuathiri mahusiano yake yote maishani yakiwemo yake na watoto pamoja na wenza wake. Kutokujithamini, kuhisi anaonewa katika kila jambo (inferiority complex), hasira na chuki zisizo na sababu, kutokuridhika na upendo hata apendwe vipi, kupenda kuhusiana na watu wa hovyo (bad boys), moyo kuwa sugu na kutojali, kutaka kupendwa na kila mtu, kuumizwa sana na maneno ya watu, hamu isiyoisha ya kutaka sana kufurahisha watu na matatizo mengine mengi.

Maumivu haya inabidi yachimbuliwe katika mizizi yake ili yaweze kung'olewa. Na hapo ndipo safari ya uponaji wa kweli itaweza kuanza. Hata kuja kuyasema tu hapa naamini huko aliko anajisikia unafuu kidogo. Inabidi sasa atafute mshauri nasaha/mwanasaikolojia mzuri ili wakae na kuchimbua mizizi ya hii trauma. Naamini atakuwa sawa; hasa ikifika mahali akawasamehe na kuwaachilia kabisa hao wazazi wake kwa tanuru la mateso walilompitisha. Mungu na Amsaidie 🙏🏿
 
Mama alificha makucha maana hata kuna mtoto wake alikuja mwanzoni walikuwa vizuri ila baadae anakuwa na mambo ya ajabu unaweza kumsalimia asiitikie au atafanya kitu uongee ili akuanzishie ugomvi
Sad,sahau....usiwe Kama Mimi niliweka kinyongo na kikaja kunitesa mwenyewe...Kupitia njia ngumu ni sehemu ya maisha
 
Wewe Dada mbona hadithi ya maisha yko inataka kufanana na yangu? Sema Mimi niliachwa na miezi 4😭 wanaume hakika angalieni wanawake wa kuona hasa ukiwa umeachiwa mtoto/watoto wadogo...... Mungu bariki kila Mama aweze kulea mwenyewe uzao wake.
Pole sana japo mimi niliachwa nikiwa chekechea, Mungu atutie nguvu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…