Siwezi kusahau haya manyanyaso ya mama wa kambo

Siwezi kusahau haya manyanyaso ya mama wa kambo

Binafsi nimekuwa na kulelewa na baba kwani mama yangu alifariki nikiwa nipo mdogo, nilipofika darasa la 6 baba alipata mwanamke wa kuishi nae, huyu nilitambulishwa kuwa atakuwa akiishi nasi.

Huyu mwanamke wa baba alikuwa mkarimu, mchapakazi, msafi, mchangamfu na ana stori nyingi sana, kabila lake alikuwa mngoni. Baada ya kuanza kuishi naye mwanzoni mambo yalikuwa mazuri tu, lakini baadae baada ya kufika secondary na kipindi hiki ndiyo kilikuwa kipindi cha ukuaji, kwahiyo vitabia vya ujeuri jeuri nilikuwa navyo hapo ndiyo tukaanza kukosana sasa.

Nakumbuka nilikuwa nikikosea mama huyu alikuwa ananipiga sana kama anataka kuua mtu, kama hakuna mtu wa kukugombelezea hapo naona anaweza hata kukuvunja kiungo, maana alikuwa akikasirika mishipa inamtoka na anakuwa na nguvu za ajabu, ikafika kipindi akaanza kuninenea maneno mabaya sana huyu mama, nikikumbuka hayo maneno sitamani hata kuonana nae.

Wakati haya yote yanatendeka baba angu alikuwa anaona lakini ni vile mapenzi yana nguvu kwahiyo aliacha mimi niteseke ili wasikosane na mkewe, ilifika kipindi tulikuwa hatuongei kabisa zaidi ya mwaka kipindi hiki nilikuwa nimeshamaliza kidato cha 4, kwahiyo nilikuwa naenda kwa ndugu nakaa alafu narudi nyumbani, sasa kuna siku tulipishana kauli na huyu mama akaanza kusema maneno mabaya mpaka kunitukana na kusema natembea na baba angu😭😭 hili alikuwa analiongea kama kitu cha kawaida sana, hakika aliniumiza sana, akaniambia nimeathirika mimi, akaniambia anaweza hata kuninyonga nisimchukulie poa😭😭 sasa sijui ni lini alinipima, kiukweli sikuweza kumvumilia tulijibishana hapo, na mzee alikuwepo akawa anaamualia maana huyu mama alitaka kunipiga.

Sasa mzee akaniambia niende kumuita mjumbe, nikaenda nikarudi mjumbe alikuwa bize nikaenda kumuita jirani yetu mama mmoja hivi ambaye pia ni shosti yake na mama, basi kufika pale akawa anasuluhisha lakini huyu mama alikuwa anasema hawezi kunisamehe, hasemi kikubwa nilichomkosea ila ndiyo hivyo tu anasema.

Mwisho wa siku, akaniambia amenisamehe basi tukashikana mikono ila mimi nikamuona usoni kama ameridhia kinafki tu, sikutaka mambo mengi nikawa sawa tu na mimi nikafurahia pale.

Sasa mimi nilikaa nyumbani kama siku mbili tatu nikaondoka nikaenda kwa ndugu zangu, nilivyokuwa huko mzee akanipigia simu akaniambia wamegombana na mkewe ameongea maneno ya hovyo, yeye mwenyewe anasema kamchoka mkewe, akaniambia walivyogombana akawa anasema hajanisamehe pale aliona aibu tu sababu ya yule mama jirani, aisee mimi nikamwambia watajua wenyewe, wamalizane wenyewe maana kugombana wamezoea wanashikianaga hadi mapanga na kesho unawakuta wako wanacheka kama hakuna kilichotokea.

Ikapita muda nikarudigi home, maisha mengine yakaendelea kama kawa japo hivyo hivyo kiunafki nafki tu, lakini hadi hii leo tunaongea tu, nilimsamehe kweli lakini moja kwa moja lakini sina amani na furaha ya kupafurahia nyumbani ndiyo maana huwa siendi mara kwa mara hadi nipigiwe simu waniulize mbona kimya siendi kuwasalimia ndiyo ntaenda.

Hivi, sisi wanawake tuna shida gani kwanini hatuwezi kuishi kwa upendo na watoto wa wanawake wenzetu, sasa nilichogundua japo sijafanya uchunguzi wa kina sana ila nimegundua huyu mama ana shida kidogo kwenye afya ya akili au kuna ugonjwa unamsumbua ndiyo unampelekea kupenda ukorofi na fujo hivyo maana alikuwa akitaka kunipiga anakuwa anataka kama kuning"ata sasa sijui kwanini, kingine ni chuki na roho mbaya pia.

Haya matukio na maisha niliyopitia hapo yameniachia alama na makovu makubwa nashindwa kupona kabisa kuna muda huwa nakaa namuuliza Mungu hivi kwanini umeruhusu nipitie maisha ya namna hii, kwanini umeruhusu mama angu aondoke mapema naimani angekuwepo mama angu nisingepitiaga yote haya na pengine ningekuwa na furahia background yangu.

Kiukweli nilikuwa nikimchukia baba yangu, lakini sioni faida ya kufanya, nimeamua tu niache hayo maana kuna leo na kesho, nyie single faza jaribuni kuoa au kuishi na wanawake watakaowapenda watoto wenu, siyo unaishi na mwanamke unajua kabisa hampendi mwanao ila kwasababu wewe anakupenda unaganda nae hii siyo sawa.

Mimi sina la zaidi ndugu zangu, asanteni kwa kusoma japo mimi siyo mwandishi mzuri, nadhani sijaandika kama inavyopaswa lakini atleast imeeleweka.
Kwa mujibu wa maelezo yako shida ilikuwa kwako na si mama wa kambo.
 
Itakuwa una pepo la kudundwa wewe. Si ndio wewe ulichezea kichapo cha msukuma?

Anyways kiuhalisia inaonekana chimbuko la chuki kwa mama yako wa kambo ni kupevuka kwako na kuanza jeuri.

Kuendelea kuumia ikiwa muhisika anaishi maisha yake kwa amani ni wewe kujitesa mwenyewe.
 
Foolish age haikwepeki...mama alihitaji busara sana namna ya kuishi na mwanae
Hakuna kitu kama hicho inatokana na malezi na huruka ya mtoto tu, maana hata sisi hizo hatua tumezipitia lakini hatukuwahi kuleta dharau na jeuri mbele wa walezi na wazazi wetu.
Huyu mleta mada kuna kipindi alisha andika mada humu jf kujutia historia ya maisha yake ya nyuma hii inaonesha alikuwa ni mtu mwenye tabia mbovu sana.
 
Itakuwa una pepo la kudundwa wewe. Si ndio wewe ulichezea kichapo cha msukuma?

Anyways kiuhalisia inaonekana chimbuko la chuki kwa mama yako wa kambo ni kupevuka kwako na kuanza jeuri.

Kuendelea kuumia ikiwa muhisika anaishi maisha yake kwa amani ni wewe kujitesa mwenyewe.
Hana amani yoyote kwasasa, alafu mimi siumii wala nini lakini nashindwa kusahau hayo
 
Hakuna kitu kama hicho inatokana na malezi na huruka ya mtoto tu, maana hata sisi hizo hatua tumezipitia lakini hatukuwahi kuleta dharau na jeuri mbele wa walezi na wazazi wetu.
Huyu mleta mada kuna kipindi alisha andika mada humu jf kujutia historia ya maisha yake ya nyuma hii inaonesha alikuwa ni mtu mwenye tabia mbovu sana.
Unavyoongea hivyo ni kama tumekuwa wote, aya endelea kunielezea
 
Sote tulifundishwa mada ya uandishi wa barua za kikazi. Hebu leo kamata graduate ye yote mwambie aandike barua siriazi ya kuomba kazi uone majanga yake. CV ndiyo kabisaaa!

➡️➡️➡️ Anyway. Binti Sayuni03 ana maumivu bado; na childhood trauma ni mbaya maana inaweza kuathiri mahusiano yake yote maishani yakiwemo yake na watoto pamoja na wenza wake. Kutokujithamini, kuhisi anaonewa katika kila jambo (inferiority complex), hasira na chuki zisizo na sababu, kutokuridhika na upendo hata apendwe vipi, kupenda kuhusiana na watu wa hovyo (bad boys), moyo kuwa sugu na kutojali, kutaka kupendwa na kila mtu, kuumizwa sana na maneno ya watu, hamu isiyoisha ya kutaka sana kufurahisha watu na matatizo mengine mengi.

Maumivu haya inabidi yachimbuliwe katika mizizi yake ili yaweze kung'olewa. Na hapo ndipo safari ya uponaji wa kweli itaweza kuanza. Hata kuja kuyasema tu hapa naamini huko aliko anajisikia unafuu kidogo. Inabidi sasa atafute mshauri nasaha/mwanasaikolojia mzuri ili wakae na kuchimbua mizizi ya hii trauma. Naamini atakuwa sawa; hasa ikifika mahali akawasamehe na kuwaachilia kabisa hao wazazi wake kwa tanuru la mateso walilompitisha. Mungu na Amsaidie 🙏🏿
Hapo kwa graduate umenichekesha ila kwa sababu basics wanayo ni rahis kuelekezwa!

Turudi Kwa binti sayuni:
Nimekuelewa vizuri sana, katika maisha ya kawaiida unapotaka kumsaidia mtu unaweza kusaidia msaada wa 'hali na mali' Kwa ww ulivoainisha huyu anahitaji msaada wa hali kwenye hilo first defense line ya kujisaidia ni yeye mwenyewe ila kwenye msaada wa Mali ndo wengine wanaweza kua first defense line ya kukushika Mkono maana unaweza usiwe na chochote!
 
Back
Top Bottom