Siwezi kusahau haya manyanyaso ya mama wa kambo

Siwezi kusahau haya manyanyaso ya mama wa kambo

Si ninavyo kuelezea bali jinsi ulivyo jielezea ww, au sio ww uliye leta mada ya kujutia maisha yako ya nyuma?
Na kwenye maelezo yako sio ww ulie sema kuwa mama yako wa kambo alikuwa vizuri mpaka pale ulipo anza tabia za ajabu?
Hata ww una upande wa pili iwapo mtu atavuka mipaka yako ya uvumilivu.

Kama ww unavyo jutia makosa yako ya nyuma na hutaki kuhukumiwa kwa uliyo yafanya huko nyuma, hivyo hivyo huna haki ya kumuhukumu mama yako wa kambo kwa mama yako wa kambo kwa mambo ya nyuma msamehe maisha yaende mbele.
Kusamehe mtu aliyetengeneza donda moyoni si kazi ya muda mfupi ndugu yangu.

Anahitaji mtu sahihi wa kumweleza na mengine mengi aliyoyapitia.ninaimani siku akijaribu kufanya hivyo atalia sana basi na hapo ndio utakuwa wakati wake sahihi kwa kulia sana bila kubembelezwa anyamaze kulia,taratibu ataanza kupata ahueni mazungumzo ya kusamehe yataanzia hapo na kidogo kidogo atajikuta anaachilia vitu.

Hakika Mungu amtie nguvu aise vinginevyo itaathiri baadhi ya vitu😌
 
Sote tulifundishwa mada ya uandishi wa barua za kikazi. Hebu leo kamata graduate ye yote mwambie aandike barua siriazi ya kuomba kazi uone majanga yake. CV ndiyo kabisaaa!

Anyway. Binti Sayuni03 ana maumivu bado; na childhood trauma ni mbaya maana inaweza kuathiri mahusiano yake yote maishani yakiwemo yake na watoto pamoja na wenza wake. Kutokujithamini, kuhisi anaonewa katika kila jambo (inferiority complex), hasira na chuki zisizo na sababu, kutokuridhika na upendo hata apendwe vipi, kupenda kuhusiana na watu wa hovyo (bad boys), moyo kuwa sugu na kutojali, kutaka kupendwa na kila mtu, kuumizwa sana na maneno ya watu, hamu isiyoisha ya kutaka sana kufurahisha watu na matatizo mengine mengi.

Maumivu haya inabidi yachimbuliwe katika mizizi yake ili yaweze kung'olewa. Na hapo ndipo safari ya uponaji wa kweli itaweza kuanza. Hata kuja kuyasema tu hapa naamini huko aliko anajisikia unafuu kidogo. Inabidi sasa atafute mshauri nasaha/mwanasaikolojia mzuri ili wakae na kuchimbua mizizi ya hii trauma. Naamini atakuwa sawa; hasa ikifika mahali akawasamehe na kuwaachilia kabisa hao wazazi wake kwa tanuru la mateso walilompitisha. Mungu na Amsaidie 🙏🏿
 
Mengi ya aliyofanya hata mama yako mzazi angefanya. Bond ya binti na baba yake huwa inakuwa kubwa kiasi cha kuanza kutiliwa shaka na mama. Wanawake wengi wanakuwa na wivu na huu uhusiano wa binti na baba yake.

Kama umeolewa na una mtoto wa kike hili utalishuhudia wazi. Akivunja ungo na kuota vimatiti uhusiano wa karibu haufi. Na binti anaongeza kiburi zaidi. Utaomba chochote utapewa na kupewa muda zaidi kuliko yeye. Hapo ndio utaanza kuona wivu wa mama kuelekea binti yake na kuanza kukuhisi unaliwa. Sio mama wa kambo tu hata mama mzazi
Hii sikubaliani nayo kwa maana mimi sikuwa na huo ukaribu wa kutisha mzee
 
Kusamehe mtu aliyetengeneza donda moyo si kazi ya muda mfupi ndugu yangu.

Anahitaji mtu sahihi wa kumweleza na mengine mengi aliyoyapitia.ninaimani siku akijaribu kufanya hivyo atalia sana basi na hapo ndio utakuwa wakati wake sahihi kwa kulia sana bila kubembelezwa anyamaze kulia,taratibu ataanza kupata ahueni mazungumzo ya kusamehe sasa yataanzia hapo na kidogo kidogo atajikuta anaachilia vitu.

Hakika Mungu amtie nguvu aise vinginevyo itaathiri baadhi ya vitu😌
Asante sana mkuu ngoja nianze kutafuta mwanasaikolojia
 
Mimi huyu baba angu alikuwa kashikwa akili na mkewe kabisa, yaani unamwambia anasikitika tu na hafanyi kitu, anaona kabisa matusi kama hayo tunatukanwa lakini hafnyi kitu
Katika viumbe ambavyo tunapaswa kuviombea sana basi ni Mwanaume.Awe baba,kaka,mtoto,mjomba..hawa viumbe wanapitaga kwenye mambo mengi na magumu na kwa bahati mbaya sana si viumbe rahisi wa kusema yanayowasibu💔.

Mwanaume yeyote akitekwa ufahamu amekwisha.msamehe baba yako.Tuwaombee mno
 
Mwanzoni umesema mambo yalienda sawa ila yalikuja kubadilika ulipobalehe na kuanza kuwa na tabia za ukaidi kwahy tatizo ni wewe
Mwanadamu kwa asili ni mbinafsi sana.hakuna mtu asiyejua kuwa wakati wa balehe kuna vitabia huwa vinaibuka ninauhakika angekuwa mwanae kuna adhabu na maneno makali asingemtamkia mwanae.

Kwa upande wako Binti Sayuni03 hii stori unayotupa leo ipo siku itakufikisha sehemu ambayo ilikuwa ni lazima upitie hayo mateso ili ufike ulipokusudiwa.

Praise the Lord..
 
Huyu mwanamke wa baba alikuwa mkarimu, mchapakazi, msafi, mchangamfu na ana stori nyingi sana, kabila lake alikuwa mngoni. Baada ya kuanza kuishi naye mwanzoni mambo yalikuwa mazuri tu, lakini baadae baada ya kufika secondary na kipindi hiki ndiyo kilikuwa kipindi cha ukuaji, kwahiyo vitabia vya ujeuri jeuri nilikuwa navyo hapo ndiyo tukaanza kukosana sasa.
Nadhani wewe ndio umeanza hizo shida, angalia sifa ulizomwaga hapo juu, kwahiyo tabia zako ndio zilimbadilisha mama wa watu, akaona akicheka na nyani atavuna mabua. Na hakuna mahali umesema kuwa wewe ulikuwa mtoto mtiifu, bali kiburi, jeuri mbavyo mpaka leo unavyo
 
Nadhani wewe ndio umeanza hizo shida, angalia sifa ulizomwaga hapo juu, kwahiyo tabia zako ndio zilimbadilisha mama wa watu, akaona akicheka na nyani atavuna mabua. Na hakuna mahali umesema kuwa wewe ulikuwa mtoto mtiifu, bali kiburi, jeuri mbavyo mpaka leo unavyo
Siyo kweli mkuu, mimi siyo muandishi mzuri hivyo mengine sijaandika
 
Back
Top Bottom