Binti Sayuni03
JF-Expert Member
- Jan 21, 2025
- 1,075
- 1,913
- Thread starter
- #101
Hakika mkuu nitafanya hivyoSonga mbele safari ni ndefu na usikumbuke ya nyuma yatakuumiza sana na kukurudisha nyuma.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hakika mkuu nitafanya hivyoSonga mbele safari ni ndefu na usikumbuke ya nyuma yatakuumiza sana na kukurudisha nyuma.
Amen 🙏Mwanadamu kwa asili ni mbinafsi sana.hakuna mtu asiyejua kuwa wakati wa balehe kuna vitabia huwa vinaibuka ninauhakika angekuwa mwanae kuna adhabu na maneno makali asingemtamkia mwanae.
Kwa upande wako Binti Sayuni03 hii stori unayotupa leo ipo siku itakufikisha sehemu ambayo ilikuwa ni lazima upitie hayo mateso ili ufike ulipokusudiwa.
Praise the Lord..
Huyu ukorofi ni asili yakeWatu wa nyota ya nge hao wao kujaa upepo dk sifuri moto baridi
Ndiyo maana nilimuacha tuUnampigaje kichaa sasa
Hakika mkuu yote hayo ni makosa yakeUlikua na baba wa hovyo, asie jielewa na asie tambua nafasi yake ndani ya nyumba yake kama baba.
'Siyo mwandishi mzuri' ...huku unamwaga madini tena vizuri kabisa!Binafsi nimekuwa na kulelewa na baba kwani mama yangu alifariki nikiwa nipo mdogo, nilipofika darasa la 6 baba alipata mwanamke wa kuishi nae, huyu nilitambulishwa kuwa atakuwa akiishi nasi.
Huyu mwanamke wa baba alikuwa mkarimu, mchapakazi, msafi, mchangamfu na ana stori nyingi sana, kabila lake alikuwa mngoni. Baada ya kuanza kuishi naye mwanzoni mambo yalikuwa mazuri tu, lakini baadae baada ya kufika secondary na kipindi hiki ndiyo kilikuwa kipindi cha ukuaji, kwahiyo vitabia vya ujeuri jeuri nilikuwa navyo hapo ndiyo tukaanza kukosana sasa.
Nakumbuka nilikuwa nikikosea mama huyu alikuwa ananipiga sana kama anataka kuua mtu, kama hakuna mtu wa kukugombelezea hapo naona anaweza hata kukuvunja kiungo, maana alikuwa akikasirika mishipa inamtoka na anakuwa na nguvu za ajabu, ikafika kipindi akaanza kuninenea maneno mabaya sana huyu mama, nikikumbuka hayo maneno sitamani hata kuonana nae.
Wakati haya yote yanatendeka baba angu alikuwa anaona lakini ni vile mapenzi yana nguvu kwahiyo aliacha mimi niteseke ili wasikosane na mkewe, ilifika kipindi tulikuwa hatuongei kabisa zaidi ya mwaka kipindi hiki nilikuwa nimeshamaliza kidato cha 4, kwahiyo nilikuwa naenda kwa ndugu nakaa alafu narudi nyumbani, sasa kuna siku tulipishana kauli na huyu mama akaanza kusema maneno mabaya mpaka kunitukana na kusema natembea na baba angu😭😭 hili alikuwa analiongea kama kitu cha kawaida sana, hakika aliniumiza sana, akaniambia nimeathirika mimi, akaniambia anaweza hata kuninyonga nisimchukulie poa😭😭 sasa sijui ni lini alinipima, kiukweli sikuweza kumvumilia tulijibishana hapo, na mzee alikuwepo akawa anaamualia maana huyu mama alitaka kunipiga.
Sasa mzee akaniambia niende kumuita mjumbe, nikaenda nikarudi mjumbe alikuwa bize nikaenda kumuita jirani yetu mama mmoja hivi ambaye pia ni shosti yake na mama, basi kufika pale akawa anasuluhisha lakini huyu mama alikuwa anasema hawezi kunisamehe, hasemi kikubwa nilichomkosea ila ndiyo hivyo tu anasema.
Mwisho wa siku, akaniambia amenisamehe basi tukashikana mikono ila mimi nikamuona usoni kama ameridhia kinafki tu, sikutaka mambo mengi nikawa sawa tu na mimi nikafurahia pale.
Sasa mimi nilikaa nyumbani kama siku mbili tatu nikaondoka nikaenda kwa ndugu zangu, nilivyokuwa huko mzee akanipigia simu akaniambia wamegombana na mkewe ameongea maneno ya hovyo, yeye mwenyewe anasema kamchoka mkewe, akaniambia walivyogombana akawa anasema hajanisamehe pale aliona aibu tu sababu ya yule mama jirani, aisee mimi nikamwambia watajua wenyewe, wamalizane wenyewe maana kugombana wamezoea wanashikianaga hadi mapanga na kesho unawakuta wako wanacheka kama hakuna kilichotokea.
Ikapita muda nikarudigi home, maisha mengine yakaendelea kama kawa japo hivyo hivyo kiunafki nafki tu, lakini hadi hii leo tunaongea tu, nilimsamehe kweli lakini moja kwa moja lakini sina amani na furaha ya kupafurahia nyumbani ndiyo maana huwa siendi mara kwa mara hadi nipigiwe simu waniulize mbona kimya siendi kuwasalimia ndiyo ntaenda.
Hivi, sisi wanawake tuna shida gani kwanini hatuwezi kuishi kwa upendo na watoto wa wanawake wenzetu, sasa nilichogundua japo sijafanya uchunguzi wa kina sana ila nimegundua huyu mama ana shida kidogo kwenye afya ya akili au kuna ugonjwa unamsumbua ndiyo unampelekea kupenda ukorofi na fujo hivyo maana alikuwa akitaka kunipiga anakuwa anataka kama kuning"ata sasa sijui kwanini, kingine ni chuki na roho mbaya pia.
Haya matukio na maisha niliyopitia hapo yameniachia alama na makovu makubwa nashindwa kupona kabisa kuna muda huwa nakaa namuuliza Mungu hivi kwanini umeruhusu nipitie maisha ya namna hii, kwanini umeruhusu mama angu aondoke mapema naimani angekuwepo mama angu nisingepitiaga yote haya na pengine ningekuwa na furahia background yangu.
Kiukweli nilikuwa nikimchukia baba yangu, lakini sioni faida ya kufanya, nimeamua tu niache hayo maana kuna leo na kesho, nyie single faza jaribuni kuoa au kuishi na wanawake watakaowapenda watoto wenu, siyo unaishi na mwanamke unajua kabisa hampendi mwanao ila kwasababu wewe anakupenda unaganda nae hii siyo sawa.
Mimi sina la zaidi ndugu zangu, asanteni kwa kusoma japo mimi siyo mwandishi mzuri, nadhani sijaandika kama inavyopaswa lakini atleast imeeleweka.
Namuomba Mungu nisije kuwa hivyoSi ajabu wewe ukaja kuwa mmbaya zaidi na mtesaji wa watoto wa watu zaidi yake
Pole sana Binti Sayuni03 ila mpaka mwaka uishe nitakuwa nakujua na kukufahamu kila kitu isipokuwa hapo kati ,fanya mpango na hapo nipaone ili mambo mengine yaendeleeBinafsi nimekuwa na kulelewa na baba kwani mama yangu alifariki nikiwa nipo mdogo, nilipofika darasa la 6 baba alipata mwanamke wa kuishi nae, huyu nilitambulishwa kuwa atakuwa akiishi nasi.
Huyu mwanamke wa baba alikuwa mkarimu, mchapakazi, msafi, mchangamfu na ana stori nyingi sana, kabila lake alikuwa mngoni. Baada ya kuanza kuishi naye mwanzoni mambo yalikuwa mazuri tu, lakini baadae baada ya kufika secondary na kipindi hiki ndiyo kilikuwa kipindi cha ukuaji, kwahiyo vitabia vya ujeuri jeuri nilikuwa navyo hapo ndiyo tukaanza kukosana sasa.
Nakumbuka nilikuwa nikikosea mama huyu alikuwa ananipiga sana kama anataka kuua mtu, kama hakuna mtu wa kukugombelezea hapo naona anaweza hata kukuvunja kiungo, maana alikuwa akikasirika mishipa inamtoka na anakuwa na nguvu za ajabu, ikafika kipindi akaanza kuninenea maneno mabaya sana huyu mama, nikikumbuka hayo maneno sitamani hata kuonana nae.
Wakati haya yote yanatendeka baba angu alikuwa anaona lakini ni vile mapenzi yana nguvu kwahiyo aliacha mimi niteseke ili wasikosane na mkewe, ilifika kipindi tulikuwa hatuongei kabisa zaidi ya mwaka kipindi hiki nilikuwa nimeshamaliza kidato cha 4, kwahiyo nilikuwa naenda kwa ndugu nakaa alafu narudi nyumbani, sasa kuna siku tulipishana kauli na huyu mama akaanza kusema maneno mabaya mpaka kunitukana na kusema natembea na baba angu😭😭 hili alikuwa analiongea kama kitu cha kawaida sana, hakika aliniumiza sana, akaniambia nimeathirika mimi, akaniambia anaweza hata kuninyonga nisimchukulie poa😭😭 sasa sijui ni lini alinipima, kiukweli sikuweza kumvumilia tulijibishana hapo, na mzee alikuwepo akawa anaamualia maana huyu mama alitaka kunipiga.
Sasa mzee akaniambia niende kumuita mjumbe, nikaenda nikarudi mjumbe alikuwa bize nikaenda kumuita jirani yetu mama mmoja hivi ambaye pia ni shosti yake na mama, basi kufika pale akawa anasuluhisha lakini huyu mama alikuwa anasema hawezi kunisamehe, hasemi kikubwa nilichomkosea ila ndiyo hivyo tu anasema.
Mwisho wa siku, akaniambia amenisamehe basi tukashikana mikono ila mimi nikamuona usoni kama ameridhia kinafki tu, sikutaka mambo mengi nikawa sawa tu na mimi nikafurahia pale.
Sasa mimi nilikaa nyumbani kama siku mbili tatu nikaondoka nikaenda kwa ndugu zangu, nilivyokuwa huko mzee akanipigia simu akaniambia wamegombana na mkewe ameongea maneno ya hovyo, yeye mwenyewe anasema kamchoka mkewe, akaniambia walivyogombana akawa anasema hajanisamehe pale aliona aibu tu sababu ya yule mama jirani, aisee mimi nikamwambia watajua wenyewe, wamalizane wenyewe maana kugombana wamezoea wanashikianaga hadi mapanga na kesho unawakuta wako wanacheka kama hakuna kilichotokea.
Ikapita muda nikarudigi home, maisha mengine yakaendelea kama kawa japo hivyo hivyo kiunafki nafki tu, lakini hadi hii leo tunaongea tu, nilimsamehe kweli lakini moja kwa moja lakini sina amani na furaha ya kupafurahia nyumbani ndiyo maana huwa siendi mara kwa mara hadi nipigiwe simu waniulize mbona kimya siendi kuwasalimia ndiyo ntaenda.
Hivi, sisi wanawake tuna shida gani kwanini hatuwezi kuishi kwa upendo na watoto wa wanawake wenzetu, sasa nilichogundua japo sijafanya uchunguzi wa kina sana ila nimegundua huyu mama ana shida kidogo kwenye afya ya akili au kuna ugonjwa unamsumbua ndiyo unampelekea kupenda ukorofi na fujo hivyo maana alikuwa akitaka kunipiga anakuwa anataka kama kuning"ata sasa sijui kwanini, kingine ni chuki na roho mbaya pia.
Haya matukio na maisha niliyopitia hapo yameniachia alama na makovu makubwa nashindwa kupona kabisa kuna muda huwa nakaa namuuliza Mungu hivi kwanini umeruhusu nipitie maisha ya namna hii, kwanini umeruhusu mama angu aondoke mapema naimani angekuwepo mama angu nisingepitiaga yote haya na pengine ningekuwa na furahia background yangu.
Kiukweli nilikuwa nikimchukia baba yangu, lakini sioni faida ya kufanya, nimeamua tu niache hayo maana kuna leo na kesho, nyie single faza jaribuni kuoa au kuishi na wanawake watakaowapenda watoto wenu, siyo unaishi na mwanamke unajua kabisa hampendi mwanao ila kwasababu wewe anakupenda unaganda nae hii siyo sawa.
Mimi sina la zaidi ndugu zangu, asanteni kwa kusoma japo mimi siyo mwandishi mzuri, nadhani sijaandika kama inavyopaswa lakini atleast imeeleweka.
Nilicho jifunza kupitia haya niliyopitia ni kuishi vizuri na watu maisha yanabadilika muda wowote unaweza kumfanyia roho mbaya mtu kesho ndiyo akawa msaada wako, kama wao walipo sasa mimi ndiyo wananisumbua wakiumwa au wakikwama hela ya chakula ninawapa ninapojisikia, wangekuwa walinjtendea vizuri nadhani ningekuwa na ratiba nzuri kabisa ya kuhakikisha kila baada ya muda flani nahakikisha wanapata matumizi, sifanyi hivyo na sitaweza ninafanya kwa kiasi kidogo tu kwasababu ni wazazi'Siyo mwandishi mzuri' ...huku unamwaga madini tena vizuri kabisa!
Ndiyo nyie mnachanganyaga watu kusema: 'Sina'ela' huku unaporomosha bonge ka jumba!
Kwenye mada yako umetoa kama darasa.
Wanawake(binadamu) ni wanyama kama walivyo wanyama wengine, tofauti ya binadamu ni kwamba tumepewa utashi.
Kama ushafuga kuku, unaonaje majike yakitotoa vifaranga namna yanavyobehave?
Koo huyu, hataki kuoviona ama kusogelewa na vifaranga vya mwenzake na vikimsogelea anaviadhibu kwa uchungu bila sababu.
Hisia za chuki za namna hiyo hata kwa binadamu tumeumbiwa, ila kwa sababu sisi tumepewa akili ya kujitambua na kutafakari mambo, yatupasa kuchambua na kuvidhibiti vitendo vyetu vya ovyo na kufuata njia iliyosahihi kutendea wengine.
Mama yako huyo wa kambo ana tatizo la kiakili na hawezi kujidhibiti hisia zake ovu.
Hapo wa kulaumiwa ni babako mzazi ambaye ni guardian wa familia kushindwa kuingilia na kukomesha uonevu huo mapema kabisa kabla haujaota mizizi.
Wasichoelewa kina mama wa kambo walio wengi ni kwamba malezi ya mtoto huwa ni ya muda mfupi na baadaye huishia kujitegemea na kufuata maisha yake.
Kama ulimlea vizuri, lazima mtoto huyo atarudisha upendo na fadhila kama zile ambazo angelizitoa kwa mamake mzazi.
Hicho ndiyo uwazacho, Mungu akusaidiePole sana Binti Sayuni03 ila mpaka mwaka uishe nitakuwa nakujua na kukufahamu kila kitu isipokuwa hapo kati ,fanya mpango na hapo nipaone ili mambo mengine yaendelee
Alikuwa anasema akimuacha ikitokea kaumwa nani atakuwa anamuogesha, ndiyo maana akabaki kumg'ang'aniaKatika viumbe ambavyo tunapaswa kuviombea sana basi ni Mwanaume.Awe baba,kaka,mtoto,mjomba..hawa viumbe wanapitaga kwenye mambo mengi na magumu na kwa bahati mbaya sana si viumbe rahisi wa kusema yanayowasibu💔.
Mwanaume yeyote akitekwa ufahamu amekwisha.msamehe baba yako.Tuwaombee mno
Hapana mkuu hii siyo sababu ya yeye kuanza kuwa na roho mbayaMwanzoni umesema mambo yalienda sawa ila yalikuja kubadilika ulipobalehe na kuanza kuwa na tabia za ukaidi kwahy tatizo ni wewe
Sawa mkuu kwahiyo mama huyu aliyekuwa hadi anapigana na baba anamshikia na panga ni mwanamke bora kabisa mimi ndiye niliyembadilishaBint ulianza ujeuri mwenyewe,labda kama hukusoma hiyo story ukaimaliza ijapo Mshana Jr kakuletea tena urejee hayo maelezo.
Asante sana mkuuPole sana Binti.
Nipo sawa nae japo hatuna huo ukaribuBasi kama umeamuwa kusamehe acha kukaa na mambo moyoni yasahau tu na rudisha uhusiano yako na mama yako mlezi.
Kama sio sababu kwa nini ubaya ulianzia paleHapana mkuu hii siyo sababu ya yeye kuanza kuwa na roho mbaya
wewe mtoto akiwa mjeuri,akawa na kiburi halafu unaishi naye wewe utaelewana naye?Siyo kweli mkuu, mimi siyo muandishi mzuri hivyo mengine sijaandika
Nitamudhibu na kumrekebisha kwa busara na siyo kumnenea maneno mabayawewe mtoto akiwa mjeuri,akawa na kiburi halafu unaishi naye wewe utaelewana naye?