Siwezi kusahau haya manyanyaso ya mama wa kambo

Binafsi nimekuwa na kulelewa na baba kwani mama yangu alifariki nikiwa nipo mdogo, nilipofika darasa la 6 baba alipata mwanamke wa kuishi nae, huyu nilitambulishwa kuwa atakuwa akiishi nasi.

Huyu mwanamke wa baba alikuwa mkarimu, mchapakazi, msafi, mchangamfu na ana stori nyingi sana, kabila lake alikuwa mngoni. Baada ya kuanza kuishi naye mwanzoni mambo yalikuwa mazuri tu, lakini baadae baada ya kufika secondary na kipindi hiki ndiyo kilikuwa kipindi cha ukuaji, kwahiyo vitabia vya ujeuri jeuri nilikuwa navyo hapo ndiyo tukaanza kukosana sasa.

Nakumbuka nilikuwa nikikosea mama huyu alikuwa ananipiga sana kama anataka kuua mtu, kama hakuna mtu wa kukugombelezea hapo naona anaweza hata kukuvunja kiungo, maana alikuwa akikasirika mishipa inamtoka na anakuwa na nguvu za ajabu, ikafika kipindi akaanza kuninenea maneno mabaya sana huyu mama, nikikumbuka hayo maneno sitamani hata kuonana nae.

Wakati haya yote yanatendeka baba angu alikuwa anaona lakini ni vile mapenzi yana nguvu kwahiyo aliacha mimi niteseke ili wasikosane na mkewe, ilifika kipindi tulikuwa hatuongei kabisa zaidi ya mwaka kipindi hiki nilikuwa nimeshamaliza kidato cha 4, kwahiyo nilikuwa naenda kwa ndugu nakaa alafu narudi nyumbani, sasa kuna siku tulipishana kauli na huyu mama akaanza kusema maneno mabaya mpaka kunitukana na kusema natembea na baba angu😭😭 hili alikuwa analiongea kama kitu cha kawaida sana, hakika aliniumiza sana, akaniambia nimeathirika mimi, akaniambia anaweza hata kuninyonga nisimchukulie poa😭😭 sasa sijui ni lini alinipima, kiukweli sikuweza kumvumilia tulijibishana hapo, na mzee alikuwepo akawa anaamualia maana huyu mama alitaka kunipiga.

Sasa mzee akaniambia niende kumuita mjumbe, nikaenda nikarudi mjumbe alikuwa bize nikaenda kumuita jirani yetu mama mmoja hivi ambaye pia ni shosti yake na mama, basi kufika pale akawa anasuluhisha lakini huyu mama alikuwa anasema hawezi kunisamehe, hasemi kikubwa nilichomkosea ila ndiyo hivyo tu anasema.

Mwisho wa siku, akaniambia amenisamehe basi tukashikana mikono ila mimi nikamuona usoni kama ameridhia kinafki tu, sikutaka mambo mengi nikawa sawa tu na mimi nikafurahia pale.

Sasa mimi nilikaa nyumbani kama siku mbili tatu nikaondoka nikaenda kwa ndugu zangu, nilivyokuwa huko mzee akanipigia simu akaniambia wamegombana na mkewe ameongea maneno ya hovyo, yeye mwenyewe anasema kamchoka mkewe, akaniambia walivyogombana akawa anasema hajanisamehe pale aliona aibu tu sababu ya yule mama jirani, aisee mimi nikamwambia watajua wenyewe, wamalizane wenyewe maana kugombana wamezoea wanashikianaga hadi mapanga na kesho unawakuta wako wanacheka kama hakuna kilichotokea.

Ikapita muda nikarudigi home, maisha mengine yakaendelea kama kawa japo hivyo hivyo kiunafki nafki tu, lakini hadi hii leo tunaongea tu, nilimsamehe kweli lakini moja kwa moja lakini sina amani na furaha ya kupafurahia nyumbani ndiyo maana huwa siendi mara kwa mara hadi nipigiwe simu waniulize mbona kimya siendi kuwasalimia ndiyo ntaenda.

Hivi, sisi wanawake tuna shida gani kwanini hatuwezi kuishi kwa upendo na watoto wa wanawake wenzetu, sasa nilichogundua japo sijafanya uchunguzi wa kina sana ila nimegundua huyu mama ana shida kidogo kwenye afya ya akili au kuna ugonjwa unamsumbua ndiyo unampelekea kupenda ukorofi na fujo hivyo maana alikuwa akitaka kunipiga anakuwa anataka kama kuning"ata sasa sijui kwanini, kingine ni chuki na roho mbaya pia.

Haya matukio na maisha niliyopitia hapo yameniachia alama na makovu makubwa nashindwa kupona kabisa kuna muda huwa nakaa namuuliza Mungu hivi kwanini umeruhusu nipitie maisha ya namna hii, kwanini umeruhusu mama angu aondoke mapema naimani angekuwepo mama angu nisingepitiaga yote haya na pengine ningekuwa na furahia background yangu.

Kiukweli nilikuwa nikimchukia baba yangu, lakini sioni faida ya kufanya, nimeamua tu niache hayo maana kuna leo na kesho, nyie single faza jaribuni kuoa au kuishi na wanawake watakaowapenda watoto wenu, siyo unaishi na mwanamke unajua kabisa hampendi mwanao ila kwasababu wewe anakupenda unaganda nae hii siyo sawa.

Mimi sina la zaidi ndugu zangu, asanteni kwa kusoma japo mimi siyo mwandishi mzuri, nadhani sijaandika kama inavyopaswa lakini atleast imeeleweka.
Chai
 
Ni ugonjwa unaitwa bipolar hata mimi nilikosea kuoa nikao mke wa ugonjwa huo nasubiria mambo yakae sawa nitoke nduki bila kuathiri watoto maana naona mambo yangu hayaendi kila siku mikosi kafunga baraka zangu.
Ana nyota ya kaa asili yake ni maji mimi simba asili ni moto so unakuta moto unazimwa na maji.So hatumatch siku hii elewa hii elimu kabla ya kuoa.
Inatakiwa nioe mke mwenye nyota za upepo.
Upepo unapuliza moto ningekuwa mbali sana.Ana maneno makali akikutamkia lazima mabaya yakupate
Huyo ni kama huyu mama akikutamkia maneno hayo utaumia kila ukimuona na yeye hana hata habari anajifanya kasahau
 
The same way!! Tumepitia kweny moto
Mungu atutie nguvu
Mtoto wa kambo akirekebishwa na kuchapwa anaona amefanyiwa kitendo cha ajabu kuwahi kutokea duniani, ila mama zao wakiwachapa hadi wanawachoma mikono aahhh ni sawa tu! Kama unajua kuna mahalu ulibadilika kwa sababu ya kuona umeanza kukua huyo mama alikuwa sawa, na inaonekana ukaanza kumuona sio mama tena na wala hana haki ya kukuchapa kwenye upuuzi unaoufanya.
Na ujue pia alikuepusha na ndoa za utotoni na kubakwa pia maana naamini kupitia bakora zake kuna mahali ulipata kauoga.
Na vile vile angekuacha na makuzi yako ukazaa ukiwa darasa la 7 ungekujaga kulalamika mama wa kambo hakukupa malezi mazuri na kukuongoza hadi ukabakwa ukazaa utotoni!
Mjifunzege kuwa na shukrani
Ni vile siwezi kusema yote lakini Asante kwa ushauri
 
Uzi ufungwe
 
Huyo ni kama huyu mama akikutamkia maneno hayo utaumia kila ukimuona na yeye hana hata habari anajifanya kasahau
Unayacrush yamrudie mwenyewe Hapo Hapo.
Hawa wengi wanakuwaga ni wachawi nishafanya utafiti.
Mwanamke yeyeto mshari,mgomvi, mtukanaji, mkali jeuri mjuaji mwenye dharau huyu ni lazima anakuwa ni members wa vyama vyetu vile vya kupaa usiku.
 
Binafsi nimekuwa na kulelewa na baba kwani mama yangu alifariki nikiwa nipo mdogo, nilipofika darasa la 6 baba alipata mwanamke wa kuishi nae, huyu nilitambulishwa kuwa atakuwa akiishi nasi.

Huyu mwanamke wa baba alikuwa mkarimu, mchapakazi, msafi, mchangamfu na ana stori nyingi sana, kabila lake alikuwa mngoni. Baada ya kuanza kuishi naye mwanzoni mambo yalikuwa mazuri tu, lakini baadae baada ya kufika secondary na kipindi hiki ndiyo kilikuwa kipindi cha ukuaji, kwahiyo vitabia vya ujeuri jeuri nilikuwa navyo hapo ndiyo tukaanza kukosana sasa.

Nakumbuka nilikuwa nikikosea mama huyu alikuwa ananipiga sana kama anataka kuua mtu, kama hakuna mtu wa kukugombelezea hapo naona anaweza hata kukuvunja kiungo, maana alikuwa akikasirika mishipa inamtoka na anakuwa na nguvu za ajabu, ikafika kipindi akaanza kuninenea maneno mabaya sana huyu mama, nikikumbuka hayo maneno sitamani hata kuonana nae.

Wakati haya yote yanatendeka baba angu alikuwa anaona lakini ni vile mapenzi yana nguvu kwahiyo aliacha mimi niteseke ili wasikosane na mkewe, ilifika kipindi tulikuwa hatuongei kabisa zaidi ya mwaka kipindi hiki nilikuwa nimeshamaliza kidato cha 4, kwahiyo nilikuwa naenda kwa ndugu nakaa alafu narudi nyumbani, sasa kuna siku tulipishana kauli na huyu mama akaanza kusema maneno mabaya mpaka kunitukana na kusema natembea na baba angu😭😭 hili alikuwa analiongea kama kitu cha kawaida sana, hakika aliniumiza sana, akaniambia nimeathirika mimi, akaniambia anaweza hata kuninyonga nisimchukulie poa😭😭 sasa sijui ni lini alinipima, kiukweli sikuweza kumvumilia tulijibishana hapo, na mzee alikuwepo akawa anaamualia maana huyu mama alitaka kunipiga.

Sasa mzee akaniambia niende kumuita mjumbe, nikaenda nikarudi mjumbe alikuwa bize nikaenda kumuita jirani yetu mama mmoja hivi ambaye pia ni shosti yake na mama, basi kufika pale akawa anasuluhisha lakini huyu mama alikuwa anasema hawezi kunisamehe, hasemi kikubwa nilichomkosea ila ndiyo hivyo tu anasema.

Mwisho wa siku, akaniambia amenisamehe basi tukashikana mikono ila mimi nikamuona usoni kama ameridhia kinafki tu, sikutaka mambo mengi nikawa sawa tu na mimi nikafurahia pale.

Sasa mimi nilikaa nyumbani kama siku mbili tatu nikaondoka nikaenda kwa ndugu zangu, nilivyokuwa huko mzee akanipigia simu akaniambia wamegombana na mkewe ameongea maneno ya hovyo, yeye mwenyewe anasema kamchoka mkewe, akaniambia walivyogombana akawa anasema hajanisamehe pale aliona aibu tu sababu ya yule mama jirani, aisee mimi nikamwambia watajua wenyewe, wamalizane wenyewe maana kugombana wamezoea wanashikianaga hadi mapanga na kesho unawakuta wako wanacheka kama hakuna kilichotokea.

Ikapita muda nikarudigi home, maisha mengine yakaendelea kama kawa japo hivyo hivyo kiunafki nafki tu, lakini hadi hii leo tunaongea tu, nilimsamehe kweli lakini moja kwa moja lakini sina amani na furaha ya kupafurahia nyumbani ndiyo maana huwa siendi mara kwa mara hadi nipigiwe simu waniulize mbona kimya siendi kuwasalimia ndiyo ntaenda.

Hivi, sisi wanawake tuna shida gani kwanini hatuwezi kuishi kwa upendo na watoto wa wanawake wenzetu, sasa nilichogundua japo sijafanya uchunguzi wa kina sana ila nimegundua huyu mama ana shida kidogo kwenye afya ya akili au kuna ugonjwa unamsumbua ndiyo unampelekea kupenda ukorofi na fujo hivyo maana alikuwa akitaka kunipiga anakuwa anataka kama kuning"ata sasa sijui kwanini, kingine ni chuki na roho mbaya pia.

Haya matukio na maisha niliyopitia hapo yameniachia alama na makovu makubwa nashindwa kupona kabisa kuna muda huwa nakaa namuuliza Mungu hivi kwanini umeruhusu nipitie maisha ya namna hii, kwanini umeruhusu mama angu aondoke mapema naimani angekuwepo mama angu nisingepitiaga yote haya na pengine ningekuwa na furahia background yangu.

Kiukweli nilikuwa nikimchukia baba yangu, lakini sioni faida ya kufanya, nimeamua tu niache hayo maana kuna leo na kesho, nyie single faza jaribuni kuoa au kuishi na wanawake watakaowapenda watoto wenu, siyo unaishi na mwanamke unajua kabisa hampendi mwanao ila kwasababu wewe anakupenda unaganda nae hii siyo sawa.

Mimi sina la zaidi ndugu zangu, asanteni kwa kusoma japo mimi siyo mwandishi mzuri, nadhani sijaandika kama inavyopaswa lakini atleast imeeleweka.
Noma sana!
 
Aliwahi kunipiga mbwa yule........yani kama mti mbichi aliutendea vile sijui kwa mti mkavu ingekuwaje
Baba mwenyew akajifia kwaio tumekosa wote nayeye ana mayatima zake wawili
 
Pole sana Bint Sayuni! Katika yote Mungu anabaki kuwa Mwaminifu alikuachia upitie hayo kwa kusudi lake ingawa siyo mapenzi yake!
Kila mtu humu ameeleza kama ambavyo angefanya!
Kwa upande wangu huyo Mama alipitiliza mno!
Mimi kwangu huyo Mama tungekuwa tuliachana muda!
Mimi huwa katika maisha yangu WATOTO KWANZA! Wengine baadaye.
 
Pole sana mkuu Mungu akutie nguvu
 
Pole sana Bint Sayuni! Katika yote Mungu anabaki kuwa Mwaminifu alikuachia upitie hayo kwa kusudi lake ingawa siyo mapenzi yake!
Kila mtu humu ameeleza kama ambavyo angefanya!
Kwa upande wangu huyo Mama alipitiliza mno!
Mimi kwangu huyo Mama tungekuwa tuliachana muda!
Mimi huwa katika maisha yangu WATOTO KWANZA! Wengine baadaye.
Asante sana mkuu, Mungu ni mwema nimeshamsamehe sasa hivi anaona haya kwa yale aliyokuwa akinifanyia
 
Unayacrush yamrudie mwenyewe Hapo Hapo.
Hawa wengi wanakuwaga ni wachawi nishafanya utafiti.
Mwanamke yeyeto mshari,mgomvi, mtukanaji, mkali jeuri mjuaji mwenye dharau huyu ni lazima anakuwa ni members wa vyama vyetu vile vya kupaa usiku.
Sasa hivi tukikutana anaona haya kwa yale aliyokuwa ananifanyia, hakuna faida yoyote aliyopata
 
Back
Top Bottom