Siwezi kusahau siku niliyofukuzwa kazi nikiwa baa

Siwezi kusahau siku niliyofukuzwa kazi nikiwa baa

DALALI MKUU

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2022
Posts
2,011
Reaction score
4,705
Hello wazee na mashangazi,

Kuna tukio lilinitokea Mwaka 2021 mwishon tarehe kama ya Leo sitokaa niisahau.

Nilikuwa nimekaa zangu Bar nakunywa castle zangu lite na embassy nimekaa na mhudumu tunapiga story za hapa na kule.

Mara ghafla nikasikia SMS imeingia Kwa Simu nikasema siisomi Kwanza itakuwa ni ya wife ama mchepuko.
Ila Roho ikaniambia ni SMS muhimu kaisome nikaamka nikaenda washroom nikafungua nikakupa sms inasema "Kuanzia kesho usiingie kazini nenda HQ Utapata maelekezo mengine"

Nikarudi nikachukue Konyagi ndogo nikaibwia kama maji madogo ya Kilimanjaro au Juice Kisha nikampigia Boss nikamwambia sijaelewa sms Yako, akanijibu Kwa kifupi umefukizwa kazi kachukue barua Yako HQ kesho na kama unadai ama unadaiwa utalipwa stahiki zako zote.

Nikavuta pumzi nikamuuliza kwanini? Akajibu Kwa kifupi una tuhuma nzito sana za kuchukua Hela kwa supplier zaidi ya million 14 Ili umpe tender tumeona tusiende mahakamani ila utupishe tu.

Tuhuma haikuwa ya kweli kabisa ila supplier aliwahi kuniambia nimfanyie namna nimpe hiyo tender atanipa dau Nene nikamwambia mimi sisi hatufanyi kazi za namna hiyo maana tender zote zinafanyiwa evaluation na wakubwa namimi ni mtu tu wa IT hivyo sihusiki.

Basi nilibwiya pombe siku hiyo nilikuwa na 1.2M nikanywa Kila aina ya pombe lakin silewi. Sijui Nini kilifuata asubuh nilijikuta nipo lodge na mhudumu wa Ile Bar.

Kesho yake nikafuata barua yangu Kisha nikaandika barua ya utetezi na ushahid wa Whatsapp chat na Hadi Leo sijajibiwa. Nikaamua kujichanganya Hadi Leo Nipo kwenye company nyingine nakula Bata tu.

Ila mhudumu wa pale bar aliniambia Ile siku nilikunywa konyag ndogo tatu kvant kubwa Moja na castle kumi na Moja.
 
Dah! Hiyo kesi nimeitamani hatari! Shida kubwa watanzania wengi walioajiriwa sekta binafsi au serikalini,ni woga wa kudai haki zao wakati wangethubutu wangeweza kuvuna pesa nyingi ikiwa taratibu za kazi hazikufuatwa katika kukuachisha kazi. Pole sana mkuu ila shukuru Mola ulipata kwingine.
 
Sisi watu wa IT sio waongeaji sana na tunaziogopa kweli mahakama
 
Dah! Hiyo kesi nimeitamani hatari! Shida kubwa watanzania wengi walioajiriwa sekta binafsi au serikalini,ni woga wa kudai haki zao wakati wangethubutu wangeweza kuvuna pesa nyingi ikiwa taratibu za kazi hazikufuatwa katika kukuachisha kazi. Pole sana mkuu ila shukuru Mola ulipata kwingine.
Huenda wakati huo ninheliweka jukwan ningepata msaada
 
Pole sana mkuu, babu yangu aliwahi kufutwa kazi ya u RC mkoa wa Kilimanjaro na JK Nyerere kwa style inafanana na hiyo.

Kipindi hicho alinisimulia kulikua na Bar za viongozi, sasa usiku alienda kupiga mitungi kwenye hiyo bar/club ya serikari Moshi.

Saa 2 usiku hua walikua wanazima mziki inawekwa taarifa ya habari kutoka RTD ndipo akasikia kua Rais amemtema kazi , kabla ya kupata barua wala kupigiwa simu.
 
Back
Top Bottom