Siyo lazima kila alama ya mvuka kwa miguu (zebra) dereva wa gari asimame, Sheria ifumuliwe imepitwa na wakati

Tatizo hata wavuka barabara nao hwajitambui, gari inasimama mtu anaendelea ongea na simu, wanapita wachache akiona wamevuka na yeye ndo anataka vuka
Wengine huwekwa chambo na askari ili kukuchomesha then wanakawiwa ganji,
Yaani jaamaa anakuwa anamtayme dereva na kuchomeka mguu, au kuingia wakati gari ikipita ili mbele trafiki anakwambia mbona unataka kugonga watu kwenye zebra,
 
Basi kama haujui trafiki wengi wamepata matatizo kwa hilo unalolizungumza brother...
 
Usilete hisia kwenye mambo yanayohitaji sheria, hakuna dereva asiyepisha LA sivyo kila siku tungesikia vifo vya watembea mguu,

Tunachosema hapa, hizo zebra hata kama hakuna MTU wa kuvuka, ukipita trafiki anakukamata ,
Traffic wa wapi wanaokukamata hata kama hakuna watu?
 
Tena inatakiwa iongezewe mkazo na faini yake iwe juu zaidi, kwenye zebra unatakiwa usimame hakuna namna ,sehem ya wavuka kwa miguu siku zote inatakiwa iheshimiwe
 
Una hoja.. Kwenye zebra hakuna mtu anaetaka kuvuka, ukipita bila kusimama, li askari linakwambia mbona hukusimama kwenye zebra, ni upuuzi tu.
Angekuwepo mtu anataka kuvuka sawa, sasa hakuna mtu bado nisimame tu, haileti mantiki.
 
Inawezekana una hoja ila hueleweki kwa sababu ya uandishi wako mbovu!
 
Tena inatakiwa iongezewe mkazo na faini yake iwe juu zaidi, kwenye zebra unatakiwa usimame hakuna namna ,sehem ya wavuka kwa miguu siku zote inatakiwa iheshimiwe
Ndugu yangu kuna barabara zinabebra nyingi kuliko watu, ebu waza hakuna watu wavukaji theni dereva asimame kila sehem!

Hata watembea kwa miguu haohao wakipanda daladala linalosimama kila kituo huanza kulalamika hii inaonesha jinsigani siyo kila sehem lazima kusimama hata kama hakuna watu!

Lakini sheria IPO kimya ndiyo maana askari anaweza kumuandikia dereva akiamua na hakuna kitu atamfanya maana sheria inamlinda askari kufanya hayo hata kubambika makosa
 
Ni kweli lakini na madereva pia mnazipuuza sana hizo sheria.
Kivipi lete hoja ..ingekuwa madereva wanapuuza hivi huko barabarani si kila siku watu wangegongwa?
Kwanini utazame kosa moja la miaka mitano na usione ibora wa madereva kila siku?
 
Kwenye zebra azima usimame utaki kanunue ndege fullstop, maana usiposimama au kupunguza mwendo na wa nyuma yako nae ataosha vile vile sasa watu watavuka saa ngapi , slow down unapokaribia zebra cheki kushoto kulia ukivuka osha
 
Wewe ni dereva au abiria?
Ninaendesha gari kwa zaidi ya miaka 20 na nimezunguka Tanzania nzima sijashuhudia hicho ulichoandika. Wewe kwa vyo vyote vile una-over speed (unaendesha kasi zaidi ya speed inayoruhusiwa) mjini.
 
Rules are rules! Without rules we are all savages.
 
Kuna zebra zilizochorewa Horizontal solid line ukifika pale unatakiwa usimame kuwe na mtembea kwa miguu au kusiwepo , ni lazima usimame, na kuna zile zebra ambazo zimechorwa tu pale unatakiwa upunguze mwendo hata kama hamna mtu hutakiwi kupita na speed 80kph unatakiwa upunguze mwendo pita na speed ambayo ikitokea chochote unaweza kusimama mara moja vinginevyo unatakiwa kupigwa faini kwa kosa la reckless driving

Trafiki kapewa hayo mamlaka ya kukuandikia faini ikiwa utaendesha bila tahadhari.
 
Kwenye zebra azima usimame utaki kanunue ndege fullstop, maana usiposimama au kupunguza mwendo na wa nyuma yako nae ataosha vile vile sasa watu watavuka saa ngapi , slow down unapokaribia zebra cheki kushoto kulia ukivuka osha
Slows down ndicho madereva hufanya speed ya 10kmh pasipo na watembea kwa miguu lakini bado askari anakamata na kusema kwanini hujasimama? Swali sheria inamteteaje dereva hapo akiandikiwa faini?
 
Maeneo yote yenye zebra ni makazi ya watu na speed inayoruhusiwa si zaidi ya 50Kph, sasa hiyo 80kph ni wapi?
 
Slows down ndicho madereva hufanya speed ya 10kmh pasipo na watembea kwa miguu lakini bado askari anakamata na kusema kwanini hujasimama? Swali sheria inamteteaje dereva hapo akiandikiwa faini?
Uongo tena wa mwaka!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…