Siyo lazima kila alama ya mvuka kwa miguu (zebra) dereva wa gari asimame, Sheria ifumuliwe imepitwa na wakati

Maeneo yote yenye zebra ni makazi ya watu na speed inayoruhusiwa si zaidi ya 50Kph, sasa hiyo 80kph ni wapi?
Maeneo mengi tu yanazebra na unaweza kupita na hiyo speed 80kph siyo kila dereva anafata sheria ndo hao wanaopigwa faini
 
Wewe ni traffic, dereva au abiria?
Nimekuuliza ni wapi huko traffic police anakupiga fine unapopita zebra wakati hakuna watembea kwa miguu, hutaki kusema! Hivyo wewe ni muongo!

Mimi siyo traffic ila mimi ni dereva na mtembea kwa miguu!
 
Sasa ukikiuka sheria fine ni halali yako!
Ndiyo ni halali yako na ndo nasema kwenye zebra inatakiwa iongezwe sheria kali na siyo kulegezwa watu kibao wamegongwa wakiwa wanavuka kwenye zebra kwaajili ya hayahaya mambo ya kusema wakati napita na gari sikuona mtu, ameshasahu anatakiwa eneo hilo asimame au apunguze mwendo ikiwezekana 15kph ili kujiridhisha
 
Maeneo mengi tu yanazebra na unaweza kupita na hiyo speed 80kph siyo kila dereva anafata sheria ndo hao wanaopigwa faini
Mjini speed ya 80 unaipatia wapi matuta kila hatua?
Madereva wanavuka na 20kmh lakini mbele trafiki anaeaandikia faini?
Swali wanatumia kipimo gani zaidi ya kutaka kuona wanasimama hata kama hakuna watu?
 
Nimekuuliza ni wapi huko traffic police anakupiga fine unapopita zebra wakati hakuna watembea kwa miguu, hutaki kusema! Hivyo wewe ni muongo!

Mimi siyo traffic ila mimi ni dereva na mtembea kwa miguu!
Tuambie kama dereva hakubaliani na kosa, je ni utaratibu gani hufuatwa pasipo kumharibia safari na ratiba ya dereva?
 
Mjini speed ya 80 unaipatia wapi matuta kila hatua?
Madereva wanavuka na 20kmh lakini mbele trafiki anaeaandikia faini?
Swali wanatumia kipimo gani zaidi ya kutaka kuona wanasimama hata kama hakuna watu?
Kwahiyo dereva ni wa mjini tu? We kama unaendesha gari yako safari ya kwenda kazini na kurudi nyumbani tu unatakiwa ujue kuna madereva wanaoenda safari ndefu pia na huko wanapopita kuna miji midogo ambayo kuna hivyo vivuko na asipobanwa na sheria anapita na 80kph+ bila kujali hata akiona watu wamesimama pemben wanataka wavuke.

Suala la zebra ni sensitive haitakiwi itafutiwe dharura yoyote zaidi ya kusimama au kupunguza mwendo ambao unakaribia na kusimama ili kujiridhisha na ndo upite, vinginevyo ukipita na speed uliyotoka nayo huko ulipotoka bila kujali unatakiwa upigwe faini na kama hujaridhika na faini au ukionewa unatakiwa ukatae kulipa hiyo faini uende mahakamani ukapate haki yako ambayo traffic ametaka kukudhulumu.
 
Hebu soma kipengele kinachohusu zebra crosing na kile kinachohusu railway crosing kwenye sheria ya usalama barabarani. Utakua na nguvu ya kuwaelimisha hao trafiki wanapotaka kukuzingua
 
Hebu soma kipengele kinachohusu zebra crosing na kile kinachohusu railway crosing kwenye sheria ya usalama barabarani. Utakua na nguvu ya kuwaelimisha hao trafiki wanapotaka kukuzingua
Weka hapa watu wachambue
 
Nafikiri sheria iko fair ila shida iko kwa wanaosimamia hizi sheria huko barabarani, napendekeza

1. Itolewe elimu ya mara kwa mara juu ya usimamizi wa sheria hizi kwa pande zote mbili madereva na askari

2. Madereva au wamiliki wa vyombo waelekezwe pahala maalum kwajili ya kutoa malalamiko pale inapotokea askari wamekiuka sheria na kuonea watu

3. Adhabu zifuatie kwa atakaebainika kakiuka sheria ilivyoelekeza
 
Makazi ya watu sheria iko wazi speed ni 50kmh, tena pamoja hilo kuna matuta, sijui wewe unapata wapi speed ya 80kmh.

Lakini pamoja na hayo hoja yangu ya kuwekwa zebra na vibao vya mistari miekundu na alama ya stop kwenye zebra za lazima itaondoa utofauti wa matumizi ya zebra za highway na huko mjini ambapo zipo kila mita mia hivyo ni nyingi sana ambazo dereva kusimama kila sehem pasipo kuwa na watu wa kuvuka ni kero, pia kwa usiku ni hatari hata kuvamiwa kwa kusimama sima kila hatua 100
 
Kwenye zebra muwe mnavuka kwa kukimbia. Unakuta mtu kisa ni zebra anaburuza miguu kama konokono, hajui kama watu wana haraka
 
Ilikuwa hivyo kabla, madhara Kwa watembea Kwa miguu yalikuwa ni makubwa hasa kwenye vivuko
 
Kwenye zebra muwe mnavuka kwa kukimbia. Unakuta mtu kisa ni zebra anaburuza miguu kama konokono, hajui kama watu wana haraka
Nimemuuliza jamaa atuambie sheria inasemaje kama dereva hakubaliani na kosa pasipo kuathiri safari yake?

Kasema sheria IPO kimya! Swali takukuru hawaoni sasa ni wakati kupunguza rushwa kwa kushinikiza kurekebishwa kwa sheria mbovu?
 
Tuambie kama dereva hakubaliani na kosa, je ni utaratibu gani hufuatwa pasipo kumharibia safari na ratiba ya dereva?
Haki ina gharama! Nenda kwa kiongozi wake ukate rufaa na ikishindikana nenda mahakamani, hakimu atahitaji ushahidi!
 
Hapo haijabadilishwa watu wanagongwa kwa zebra!! Na ikibadilishwa itakuwq je?
 
Haki ina gharama! Nenda kwa kiongozi wake ukate rufaa na ikishindikana nenda mahakamani, hakimu atahitaji ushahidi!
Kwani ukimkamata mtu ugoni huwa unawashikilia wabakie wamekumbatiana hadi mahakamani kuonesha ushahidi?

Mtu anasafari ya mkoa ukimbambikia kosa ambalo hakubaliani nalo unaposhikilia chombo hapo siyo sheria Bali ni kumkomoa, akija kushinda sheria inasemaje kumlipia muda wake na usumbufu huyo dereva?

Ndiyo maana nasisitiza sheria ya usalama ina mapungufu mengi tansy on mandamus a dereva
 
Kwanza nimekuambia kuwa maelezo yako kuwa ukipita sehemu ya zebra unakamatwa hata kama hakuna mtembea kwa miguu siyo kweli labda kama ume-over speed. Pili kesi ya kubambikiwa utajitetea kadri itakavyoendesha na ukishinda unaweza kudai fidia kwa taratibu zilizopo. Hivyo ni kweli safari yako itakuwa imevurugwa na hakuna namna.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…