Siyo lazima kila alama ya mvuka kwa miguu (zebra) dereva wa gari asimame, Sheria ifumuliwe imepitwa na wakati

Sasa tunataka sheria isimame ili dereva asivurugiwe ratiba kwa kutunga sheria mpya
 
Sasa tunataka sheria isimame ili dereva asivurugiwe ratiba kwa kutunga sheria mpya
Hakuna kesi yo yote duniani iwe ya madai au jinai ambayo haivurugi ratiba ya mtu. Jambo la msingi tujiepushe na hizo kesi na lingine walinda Sheria waelimishwe na wasisitizwe watende haki!
 
Ukiona zebra crossing ina askari basi jua hilo eneo liko bussy na wavuka kwa miguu ni wengi simama kama unaona unachelewa basi toka nusu saa kabla ya muda ulio plan kutoka
 
Hakuna kesi yo yote duniani iwe ya madai au jinai ambayo haivurugi ratiba ya mtu. Jambo la msingi tujiepushe na hizo kesi na lingine walinda Sheria waelimishwe na wasisitizwe watende haki!
Sijui kama unaelewa! Mtu anasafari mkoani, anakutana na trafiki anambambikia kosa ambalo hakubaliani na nalo, ...chombo chake kinashikiliwa! Anashindwa kusafiri ...wewe unaona sheria hapo iko sasa kabisaa kumharibia mtu safari kusudi tu kizembe
 
Siku hizi watanzania tunazidi kuwa wajinga kwenye sheria za barabarani. Mtu anavuka kivuko huku taa ya wavuka kwa miguu ikiwa inawaka nyekundu, na wanavuka kundi huku taa za magari zimeruhusiwa. Ukiwauliza wanasema kwani huoni zebra. Yaani wanadhani kukiwa na zebra yeye ni halal kuvuka hata kama taa haimruhusu.
 
Ndiyo nikasema sheria bado inamapungufu sana
 
Sijui kama unaelewa! Mtu anasafari mkoani, anakutana na trafiki anambambikia kosa ambalo hakubaliani na nalo, ...chombo chake kinashikiliwa! Anashindwa kusafiri ...wewe unaona sheria hapo iko sasa kabisaa kumharibia mtu safari kusudi tu kizembe
Nimekuambia kwa madereva wasiozingatia sheria za barabarani ni sawa kabisa, tena wanatakiwa wawekwe rumande!

Kwa maelezo yako wewe haukubambikiwa kosa bali uli- over speed kwenye zebra kwa hiyo ulistahili adhabu kali ikiwa na pamoja na kuwekwa rumande! Madereva wazembe kama wewe ndio mnaoua watu kwenye zebra!
 
Shida inaanza na watumia barabara, traffic officer yeye ana take advantage tu kujipatia chochote.

Ila swala la msingi kuhusu zebra ni kwamba makosa huwa yanakuwa pande zote kwa nyakati tofauti si kwamba madereva wapo sahihi au waenda kwa miguu wapo sahihi muda wote.

Kwa mfano, Madereva wengi wengi hawafahamu speed ya kupita nayo kwenye Zebra. Mtu anapita na 80 kwenye zebra unategemea traffic akuache hata kama hakuna mtu anayevuka, hii inaonyesha umakini wako katika kuzingatia sheria upo chini sana, traffic anachofanya ni kukumbushana tu kuwa unatakiwa ukipita zebra basi mshale wa speed uwe below 25KM/H sio above.

Mazoea ya kupita na speed yakijengeka hautakuwa na akili ya kusimama hata kama wavukaji wapo.

Pia watumia vivuko vya Zebra mnatakiwa kujua kuwa sio kila sehemu unatakiwa uvuke kama ng'ombe anakwenda zizini. Unakuta mtu anapita mataa ya ubungo, au mwenge, au lugalo kule au popote pale kwenye taa na anaona taa zimewaka nyekundu na yeye huyo kama ng'ombe anavuka akidhania kiwa zebra ni sehemu ambayo unaweza pita muda wowote.

Wewe mwenda kwa miguu, unapotumia zebra zilizopo barabara kubwa zenye mataa chukua tahadhari kwanza kwa kutazama taa zinaelekeza nini maana zamani kulikuwa hakuna taa za waenda kwa miguu ila kwa sasa zipo utaona zinakuelekeza kuwa taa za kuongoza magari ziliwasha nyekundu then kuna upande wa watembea kwa mikuu zebra itawasha kijani ya kuashiria mvuke.

Ila hata kama hakuna taa za waenda kwa miguu kuna taa za kuongoza magari tu, haishauriwi wewe mtumia Zebra kuvuka bila tahadhari yoyote, unatakiwa utazame je, gari zimekata ndipo unavuka au at least gari iwe mbali sana. Ila sio unavuka halafu unapunguza speed kabisa unatembea kama mgonjwa ukitegemea Zebra itakulinda, uashangaa mtu amepita na wewe mazima miguu juu kichwa chini.

Tuwe makini tuchukue tahadhari.
 
Twende hivi
 
Katiba mpya yenye mantiki ni muhimu!
Hizo fomu polisi anazojaza makosa, kuwe na vipengele vinavyompa dereva uchaguzi, wa ama anakubaliana na makosa yaliyoelezwa na polisi, hivyo ndani ya siku 14 awe amelipa ada ya kosa, au hakubaliani na makosa anayoshutumiwa hivyo baada ya siku 14 aende mahakama fulani iliyo karibu na eneo la tukio.

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Kama kuna wanachopaswa kukagua, ni hali ya hayo magurudumu au chochote kama kiko katika hali salama au hatarishi na sio mwaka.

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Kama kuna wanachopaswa kukagua, ni hali ya hayo magurudumu au chochote kama kiko katika hali salama au hatarishi na sio mwaka.

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
Gurudumu hutengenezwa kwa kutumia mpira ambao hutokana na utomvu wa miti, jinsi unavyopigwa na mvua na jua mpira hupotezwa ulaini wake na kuanza kukauka kisha unakatika. Wataalamu wanaotengeneza magurudumu hukadiria muda linaloweza kuishi kabla ya kukatika na muda huo huandikwa kwenye gurudumu ili litambulike kirahisi.
Hapa Tanzania kuna mijitu mitundu isiyojali maisha ya wengine, mijitu hii hutumia vifaa maalumu kuchonga mifereji iliyokwisha kwenye gurudumu wakisahau kuwa wanapunguza unene wa gurudumu hivyo linaweza kupasuka wakati wowote endapo litajazwa upepo kiwango chake.
 
 
Itoshe kusema mtoa mada ni mpumbavu na limbukeni..inamaana wewe unaakili nyingi kulikodunia maana zebra duniani kote ipo hivyo ni lazima upunguze mwendo unakimbia unawahi wapi? Hiyo zebra ya kijani na nyekundu wwka kijijini kwenu uhai ni muhimu kuliko haya magari
 
Hongkong kwenye zebra karibu zote kuna taa ya kuongoza watu wakati wa kuvuka (kama ilivyo Mlimani city pale), kwa bongo taa za namna hiyo zipo lakini nyingi zimewekwa kwenye makutano ya barabara...
Nchi zilizoendelea unakuta watu wengi wanasubiri taa yao nao waukesha upo sahihi Hong Kong kwa zile bara bara pana bila Zebra tusingevuka...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…