Siyo siri, miradi mikubwa kama SGR, inaota nyasi. Hali ni ngumu!

Hapo papo hivyo muda sasa.
 
Jidu La Mabambasi,
... kilichokufikirisha nini wakati taarifa rasmi ya serikali ni kuwa mradi umekamilika kwa 75%?

Tulitangaziwa kuwa phase one ya mradi ingekamilika mwishoni mwa 2018 na tukaambiwa vichwa vya train na mabehewa vimeshaagizwa tayari. Nani ameona kimoja kati ya hivyo?
 
Tusaidiane kumshangaa aisee, maana mijitu mingine hadi inatia hasira, kwani hilo ni jengo linalojengwa kwenye kiwanja kimoja?,watu wengine bhana..

Sio kila mtu ni kipofu au mazezeta kama nyie waimba mapambio. Tatizo lenu hata kumbukumbu hamna. Kama serikali ilitangaza mwaka 2017 kuwa ujenzi wa kipande cha Dar - Morogoro ulikuwa umekamilika kwa 70% (na kuwa kufikia December 2018 kingekuwa kimekilika) iweje leo 2020 May bado mradi umekamilika kwa 75%?
Hivi nyie Mataga mnajielewa kweli?
 
Yeye amezungumzia zile nyasi zilizoota pale chini ya daraja ndio zinaashiria ujenzi kusimama, tujikite kwenye mada yake ya hizo nyasi
 
Yeye amezungumzia zile nyasi zilizoota pale chini ya daraja ndio zinaashiria ujenzi kusimama, tujikite kwenye mada yake ya hizo nyasi

Hilo la nyasi ni akili yako imekutuma hivyo. Hoja ni kuwa gazeti la serikali limechapisha front page picha inayoonyesha sehemu ambayo ujenzi wake umesimama muda mrefu sana sasa. Hata huko kuota nyasi ni kuashiria kuwa hakuna kinachofanyika hapo muda mrefu. Ulishaona wapi mahali watu wanapaganyaga kila siku pakaota nyasi?
 
Kazi inaendelea vizuri tu, station ya Dar ukipita sasa hivi inavutia, wiki jana kwenye kutafuta mkate nimeenda hadi station ya Kidete (mbele ya Kilosa) kwa kufuata reli, huko kote kazi inaendelea kwa kasi.
 
Endelea kuota, ila hata ukiamka baada ya 2025 ujenzi bado utakuwa ni 75%.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…