Siyo siri, miradi mikubwa kama SGR, inaota nyasi. Hali ni ngumu!

Siyo siri, miradi mikubwa kama SGR, inaota nyasi. Hali ni ngumu!

Wewe ni lofa sana kamanda. Yaani ni nyumbu kabisa, unasahau hata ulichoandika sekunde moja tu.
Soma vizuri uelewe.
Naona mmeulizwa na member humu kama mnamfahamu Membe na mnaruka kimanga!
Kwa mtu mwenye akili ameshawaweka kwenye bahasha stahiki.
 
Labda ratiba ya mradi Kwa sasa inawapasa kufanya kazi kipande toka buguruni mpaka pugu ndo maana hapo chini ya daraja panaota nyasi, ingekuwa juu ya daraja kuna nondo zimeachwa wazi bila ya zege kumwagwa Kwa mda mrefu hapo ingeacha maswali mengi zaidi..
 
Hilo la nyasi ni akili yako imekutuma hivyo. Hoja ni kuwa gazeti la serikali limechapisha front page picha inayoonyesha sehemu ambayo ujenzi wake umesimama muda mrefu sana sasa. Hata huko kuota nyasi ni kuashiria kuwa hakuna kinachofanyika hapo muda mrefu. Ulishaona wapi mahali watu wanapaganyaga kila siku pakaota nyasi?
Ujenzi umesimama kwani ujenzi wa SGR unafanyika kwa kilomita zote 500 at once?
 
Asante mkuu ingalau wewe unaweza kudiscuss kwa kutumia akili.
Najiuliza
-hapo unapoiona picha nguzo ndio imefika na taruma la zege haliendelei
-hapo unaona ni bado hapa mjini DSM(na kazi haiendelei)
-kwenye picha hata kibarua haonekani
-Kwa nyasi tunazoziona hakuna gari ya kifusi, zege, kokoto wala mchanga iliyopita hapo muda mrefu

Ni vema basi tungepata toka Daily News picha za kule kunakoendelea kujengwa ili tuione hiyo 75% ya maendeleo.
Poleni sana kwa speculations zenu!
Kwa taarifa yako kuanzia stesheni (mwanzo wa mradi) hadi Ilala (umbali wa km 2.5) treni inapita juu (via duct). Kwenye umbali huo (2.5km) tayari nguzo zote zimeshajengwa na kukamilika. Juu ya hizo nguzo zinalazwa beams ambazo hupachikwa (zaidi ya 70% ya beams zote kwenye eneo hilo zimeshawekwa). Beam hizo zinatengenezwa ndani ya kambi ya Ilala (Njoo ndani ya kambi ya Ilala uone kama beams hazitengenezwi). Katika eneo hilo almost kazi ya zege imebaki kidogo sana ndiyo maana huoni magari ya zege yakikimbizana.
Kuhusu magari ya kifusi inabidi nicheke kwanza😁😁😁!! Kifusi kinatumika kwenye ujenzi wa tuta (embankment), sasa kifusi cha nini katika eneo hilo wakati treni inapita juu? Acha ukilaza.
Hata hivyo maeneo ya mbele kama Vingunguti, Banana, nk. ambapo treni inapita chini hivyo tuta (embankment) kujengwa, elewa kwamba ujenzi wa tuta haufanyiki wakati wa mvua. Kusisitiza ujenzi wa tuta wakati mvua inanyesha ni kudhihirisha tena kwamba wewe ni KILAZA MKUBWA wa mambo ya uhandisi ujenzi.
Mambo ya Ngoswe mwachie Ngoswe! Halafu watu wenye nongwa kama nyie ndio mtakao kuwa wa kwanza kwa kiherehere kupanda treni reli itakapokamilika.
 
Huu mradi,tuombe ukamilike,Ni mradi mzuri Sana kwakweli,sisi wakulima mazao yet yatapata usafiri wa uhakika
 
Poleni sana kwa speculations zenu!
Kwa taarifa yako kuanzia stesheni (mwanzo wa mradi) hadi Ilala (umbali wa km 2.5) treni inapita juu (via duct). Kwenye umbali huo (2.5km) tayari nguzo zote zimeshajengwa na kukamilika. Juu ya hizo nguzo zinalazwa beams ambazo hupachikwa (zaidi ya 70% ya beams zote kwenye eneo hilo zimeshawekwa). Beam hizo zinatengenezwa ndani ya kambi ya Ilala (Njoo ndani ya kambi ya Ilala uone kama beams hazitengenezwi). Katika eneo hilo almost kazi ya zege imebaki kidogo sana ndiyo maana huoni magari ya zege yakikimbizana.
Kuhusu magari ya kifusi inabidi nicheke kwanza😁😁😁!! Kifusi kinatumika kwenye ujenzi wa tuta (embankment), sasa kifusi cha nini wakati treni inapita juu? Acha ukilaza.
Hata hivyo maeneo ya mbele kama Vingunguti, Banana, nk. ambapo treni inapita chini hivyo tuta (embankment) kujengwa, ujenzi wa tuta haufanyiki wakati wa mvua. Kusisitiza ujenzi wa tuta wakati mvua inanyesha ni kudhihirisha tena kwamba wewe ni KILAZA MKUBWA wa mambo ya uhandisi ujenzi.
Mambo ya Ngoswe mwachie Ngoswe! Halafu watu wenye nongwa kama nyie ndio mtakao kuwa wa kwanza kwa kiherehere kupanda treni reli itakapokamilika.
Ingalau pamoja na makandokando we umeeleza kitu.
Tupia kapicha kama Daily News basi.
Si wote twaweza kuja Ilala.
Habari za kodi zetu na matumizi yake ni muhimu kuyaelezea.
 
Back
Top Bottom