Siyo siri, miradi mikubwa kama SGR, inaota nyasi. Hali ni ngumu!

Wewe ni lofa sana kamanda. Yaani ni nyumbu kabisa, unasahau hata ulichoandika sekunde moja tu.
Soma vizuri uelewe.
Naona mmeulizwa na member humu kama mnamfahamu Membe na mnaruka kimanga!
Kwa mtu mwenye akili ameshawaweka kwenye bahasha stahiki.
 
Labda ratiba ya mradi Kwa sasa inawapasa kufanya kazi kipande toka buguruni mpaka pugu ndo maana hapo chini ya daraja panaota nyasi, ingekuwa juu ya daraja kuna nondo zimeachwa wazi bila ya zege kumwagwa Kwa mda mrefu hapo ingeacha maswali mengi zaidi..
 
Ujenzi umesimama kwani ujenzi wa SGR unafanyika kwa kilomita zote 500 at once?
 
Poleni sana kwa speculations zenu!
Kwa taarifa yako kuanzia stesheni (mwanzo wa mradi) hadi Ilala (umbali wa km 2.5) treni inapita juu (via duct). Kwenye umbali huo (2.5km) tayari nguzo zote zimeshajengwa na kukamilika. Juu ya hizo nguzo zinalazwa beams ambazo hupachikwa (zaidi ya 70% ya beams zote kwenye eneo hilo zimeshawekwa). Beam hizo zinatengenezwa ndani ya kambi ya Ilala (Njoo ndani ya kambi ya Ilala uone kama beams hazitengenezwi). Katika eneo hilo almost kazi ya zege imebaki kidogo sana ndiyo maana huoni magari ya zege yakikimbizana.
Kuhusu magari ya kifusi inabidi nicheke kwanza😁😁😁!! Kifusi kinatumika kwenye ujenzi wa tuta (embankment), sasa kifusi cha nini katika eneo hilo wakati treni inapita juu? Acha ukilaza.
Hata hivyo maeneo ya mbele kama Vingunguti, Banana, nk. ambapo treni inapita chini hivyo tuta (embankment) kujengwa, elewa kwamba ujenzi wa tuta haufanyiki wakati wa mvua. Kusisitiza ujenzi wa tuta wakati mvua inanyesha ni kudhihirisha tena kwamba wewe ni KILAZA MKUBWA wa mambo ya uhandisi ujenzi.
Mambo ya Ngoswe mwachie Ngoswe! Halafu watu wenye nongwa kama nyie ndio mtakao kuwa wa kwanza kwa kiherehere kupanda treni reli itakapokamilika.
 
Huu mradi,tuombe ukamilike,Ni mradi mzuri Sana kwakweli,sisi wakulima mazao yet yatapata usafiri wa uhakika
 
Ingalau pamoja na makandokando we umeeleza kitu.
Tupia kapicha kama Daily News basi.
Si wote twaweza kuja Ilala.
Habari za kodi zetu na matumizi yake ni muhimu kuyaelezea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…