Skendo ya Bashe na sukari ni kubwa kuliko, isiache ipite bila uwajibikaji.

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Ukiyasikiliza maelezo ya Bashe katika tuhuma za maamuzi na kutolewa vibali vya biashara ya kuingiza sukari yana walakini mwingi na kuacha maswali zaidi
1. Ni kweli Bashe anayo mamlaka ya kujifanyia maamuzi tu kwamba nchi ina dharura ya upungufu wa sukari yanayompa mamlaka ya kutofuata taratibu za manunuzi wakati huo ?
Kama waziri anayo mamlaka hayo inabidi yaondolewe au yawekewe utaratibu maalumu usioacha mashaka, sio sahihi kumpa waziri mmoja mamlaka makubwa hivyo.

2.Kwa nini wakati huo Bashe anafanya haya maamuzi ya kwamba nchi ina uhaba wa sukari na vuwanda vya sukari vimeshindwa kuingiza sukari kutoka nje hivyo kuhitajika maamuzi ya dharura wizara yake ya Kilimo au ya biashara haikuwa inatoa taarifa rasmi kwa umma?
Je, Bashe alipeleka taarifa rasmi kwenye kamati husika za bunge kuhusu jambo hilo?

3.Kwa nini viwanda vyote vya sukari vilishindwa kuingiza hata kilo moja ya sukari kadri ya vibali vyao walivyoomba na kupewa? Huku sio sawa na kula njama za kuhujumu uchumi na hivyo kuhitajika kuwajibishwa mahakamani kwa makosa ya uhujumu uchumi?

Yani Bashe anasema viwanda vyote vilishindwa kuingiza sukari hata kilo moja ikabidi wizara wachukie taratibu nyingine halafu inaisha tu hivyo?! Hivi ndivyo biashara ya sukari inavyosimamiwa na wizara yake kwamba hakuna uwajibikaji?
 
Mada za udadisi wa kutumia akili kama hizi utaona hapa JF hazina msisimko wowote ule!

Hiyo ni moja ya sababu nchi yetu inadhalilishwa kuwa nchi ya 'MAITI'.

Leo 'MAITI' wapo kwenye ushangiliaji wa ujio wa mgeni toka CHADEMA kwenda CCM!
 
Yani Bashe anasema viwanda vyote vilishindwa kuingiza sukari hata kilo moja ikabidi wizara wachukie taratibu nyingine halafu inaisha tu hivyo?! Hivi ndivyo biashara ya sukari inavyosimamiwa na wizara yake kwamba hakuna uwajibikaji?
Katika miaka ya hivi karibuni, najaribu kujikumbusha angalau mfano mmoja tu wa kiongozi "kuwajibika".
Sipati mfano hata mmoja.

Kwa hiyo, matukio ya namna hii yamekuwa ni kama mazoea tu. Watu watajadili na kupiga vikelele siku moja mbili hivi huko vijiweni, halafu mambo yanaendelea kama kawaida.
CCM na serikali yake wamekwisha tambua vizuri sana tabia hizi za waTanzania. Sasa wamekuwa hawana hofu tena ya nini kitatokea baada ya mkasa wowote unaojitokeza na wananchi wakajuwa nini kimefanyika.
Chukulia kelele za Bandari zilivyokuwa, na jinsi serikali ilivyo uchukulia na kuendelea na kazi zake kama hakuna lolote lililosemwa.

Kwa hiyo sasa imekuwa ni mazoea, hawastuki tena.

Binafsi naamini hili la sukari siyo swala la Bashe kujichukulia uamzi. Bashe alikuwa anatimiza tu yaliyo amriwa yafanyike.
Swala hilo limeshamalizwa na Spika.

Kulipeleka shauri mahakamani. Nani ataifanya/isimamia hiyo kazi? Hii kidogo italiendeleza kuwemo akilini mwa wananchi (maiti).

Inabidi niulizepia: Mwenyekiti Mbowe siku hizi anasemekana anafanya mikutano mingi (ya chopa). Tunajulishwa uwepo wa mikutano hii, na mara moja moja tunaonyeshwa 'nyomi'. Lakini hatusikii huyu mwenyekiti huzungumzia mambo gani kwenye mikutano hii! Siyo vyombo vya habari, au hata huku mitandaoni tunasoma ajenda anazowapelekea wananchi huko kwenye mikutano yake. Hii ni kwa bahati mbaya, au ni jambo mahsusi lililo tengenezwa liwe hivyo? Ningetegemea baadhi ya maswala kama hili la sukari linge elezwa vizuri ili wananchi walielewe ipasavyo; pamoja na kwamba wao ni "maiti".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…