Skendo za Unyanyasaji wa kingono kwa Watoto, waumini 520,000 wajitenga na kanisa Katoliki Ujerumani kwa mwaka

Skendo za Unyanyasaji wa kingono kwa Watoto, waumini 520,000 wajitenga na kanisa Katoliki Ujerumani kwa mwaka

Mukulu wa Bakulu

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2014
Posts
4,051
Reaction score
12,954
Kutokana na skendo za Unyanyasaji wa kingono kwa Watoto, zaidi ya waumini 520,000 walitangaza kuachana na kanisa katoliki kwa mwaka 2022, hili ni ongezeko la 44% ukilinganisha na waliojitenga na kanisa mwaka 2021 ambao walikua 360,000.

Kwa ujumla kwa mwaka 2022 waaumini zaidi ya 900,000 kutoka madhehebu ya kiprotestant na katoliki walitangaza kuachana na madhehebu yao na kujitangaza kua hawana dini.

Kwa takwimu, 52.7% ya wajerumani hujitangaza wakristo, 37.8% wasio na dini yoyote na 9% mchanganyiko wa madhehebu na dini mbali mbali na kati yao 5% ni waislamu wengi wao wakiwa ni wahamiaji kutoka Bosnia na Uturuki.

Watu wengine wanasema watu hao hawaachani na kanisa bali wanakimbia michango na kodi za kanisa ambazo hukatwa kwenye mishahara yao ama mapato yao kati ya 8% na 9% ya mapato ya muumini.

Soma zaidi.

Soma zaidi
 
Sasa kama michango ipo mpaka ulaya huku afrika kuna haja gani ya kukimbia michango? Wale wanaohama kutoka ukatoliki wako sahihi na ni asili kuhamwa kwa kanisa hilo kongwe duniani kama alivyoha kaasisi martin luther
 
Uzuri haya mambo ni ya hiyari. Hakuna wa kumlazimisha mtu kwenda Kanisani. Na ifahamike pia maendeleo ya sayansi na teknolojia Ulaya yameleta athari nyingi kwenye jamii yao.

Na mojawapo ya hizo athari, ni hii ya kuwafanya watu kuwa busy zaidi kutafuta pesa. Hivyo binafsi sioni kama kuna tatizo.
 
Back
Top Bottom