Uchaguzi 2020 Slogan ya Hapa kazi tu ni bora kuliko za vyama vingine ni rahisi kuielewa na ilisaidia CCM kushinda

Uchaguzi 2020 Slogan ya Hapa kazi tu ni bora kuliko za vyama vingine ni rahisi kuielewa na ilisaidia CCM kushinda

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Posts
36,902
Reaction score
52,001
Ili kushinda uchaguzi slogan huwa pia na mchango mkubwa

Slogan mfano us ACT wazaledo ya Kazi na Bata ilikuwa hata haileweki inalenga nani Mkulima,mfanyabiashara,machinga ,wavuvi,, wafugaji, au wafanyakazi? Ukiingalia ililenga wafanyakazi wa serikali tu ambao idadi yao ni laki nne tu sio jamii nzima ya watanzania

Ukija slogan ya Chadema ya maendeleo ya watu sip vitu imekaa kivituko na haieleweki kirahisi unatakiwa kuwa na Phd kuielewa sababu watu wanahitaji vitu mfano barabara, hospitali, shule nk wewe unasema sio yanatakiwa maedeleo ya watu. Watu wanajiuliza hayo maendeleo ya watu Yakoje? Toeni mifano mna wabunge wenu Chadema wamekaa miaka kumi hadi kumi na tano bungeni ni maendeleo yepi ya watu waliyoleta majimboni mwao tuone mfano kuwa yanafananaje? Unakuta hakuna wabunge wa Chadema hawakupeleka maendeleo ya vitu wala ya watu miaka yote waliyokaa bungeni. Hivyo hiyo Slogan ilichangia pia wananchi kuwanyima kura chadema sababu ilikosa ushahidi wa walichofanya nyuma cha maendeleo ya Watu

CCM slogan ya hapa kazi tu ilibeba ushahidi wa vitu vilivyofanyiiwa kazi Barabara,reli,mashule,vituo vya afya, umeme nk pia slogan hiyo ni nyeyekevu kuwa tupeni kura tukafanye kazi sio tukafanye kazi na kula bata kama ile ya ACT wazalendo ya kazi na bata!!!

Hii Slogan ya Hapa kazi tu ni vizuri iwekwe hadi kwenye nembo ya CCM iwe ya kudumu
 
Na imeandikwa kwenye Kitabu Kitakatifu, kwa wale wanaoamini uwepo wa Mungu, akiongoza maisha ya binadamu.
2 Wathesalonike 3:10 Kwa kuwa hata wakati ule tulipokuwapo kwenu tuliwaagiza neno hili, kwamba ikiwa mtu hataki kufanya kazi, basi, asile chakula.
 
Mahojiano kati ya Mwandishi na mbunge mkongwe wa Chadema aliyekaa miaka kumi

MWANDISHI:Mheshimiwa mbunge chama chenu hakitaki maendeleo ya vitu tuonyeshe chochote ulichofanya icha maendeleo ya watu miaka yote uliyokaa bungeni? Kama hujapeleka yawe maendeleo ya vitu au ya watu kwa nini unagombea tena?

MBUNGE:Wewe mwandishi umetumwa na CCM
 
CCM at its highest stupidity again pamoja na kuwa na viongozi wenye PhD wengi kuliko nchi yoyote duniani! Hapa kazi tu ni kauli mbiu ya kijinga kwa sababu haina time factor ambayo ni muhimu kisayansi: work = load x distance x time ndo maana Miradi mingi ya Awamu hii inatajwa tu (haionekani) au haikamiliki na wateuliwa wamefanya kauli mbiu yenu kuwa wimbo wa taifa.

Mfano mmoja tosha: SGR inatakiwa ifike Uvinza na Mwanza kupitia Dodoma na Tabora na imeanza kujengwa mwanzoni mwa Awamu hii lakini hata Morogoro haijulikani itafika lini. Wakati wa Nyerere tulikuwa na kauli mbiu: Linalowezekana Leo Lisingoje Kesho, hii kisayansi inaeleweka na kukubalika maana ina time element. Kama kauli mbiu ya CCM ingekuwa: Hapa Kazi Tu Sasa au Leo, mngeeleweka na SGR ingekuwa inaelekea Mwanza toka Tabora, Stiegler's Gorge ingekuwa inajaza maji, madege yangekuwa yanaruka, Chato Airport ingekuwa imekamilika na Burigi National Park ingekuwa inajaa watalii. Kauli mbiu za ACT Wazalendo na CHADEMA ni sahihi kabisa kwa sababu kuna wakulima wengi wenye kipato kikubwa kuliko mfanyakazi yeyote wa kuajiriwa na wakulima hawa walioendelea ndo wanaweza kuchangia maendeleo. Arusha, Moshi, Mwanza, Tanga nk ni miji iliyoendelea siku nyingi kwa mchango wa wakulima wa Kahawa, Pamba na Mkonge.

Tukiwa hapahapa na ng'ombe zetu na wake zetu wengi na watoto wetu lukuki tukangoja wazungu walioendelea waje watujengee reli, Ikulu, Shule, barabara nk. Wasukuma (chapa ng'ombe) Wana ng'ombe wengi mpaka mahari inafika ng'ombe 40 lakini nyumba zao zimekandikwa kwa kinyesi cha haohao ng'ombe na kuezekwa kwa nyasi huku wanafamilia wote wakilalia ngozi ya ng'ombe. Kule Ulaya Manor houses (nyumba za wakulima) zilizojengwa na wakulima wenyewe ni nzuri sana kuliko hayo mabox (highrise) ya mijini tunayoyaona na kujigamba kuwa ndo maendeleo. Maendeleo yana Chama siyo cha CCM!
 
Kulikuwa na wachumia tumbo tu hakukuwa na mpinzani
 
Eti “ccm kushinda”. Yani munajitahidi kweli kuwaingizia wananchi hiyo hali ya kuona kuwa ccm imeshinda kwa kuleta hoja za kitoto kabisa ili tu kujaribu ku “normalize” upumbavu.
 
Eti “slogan” ya “hapa kazi tu” ndo imewapa ushindi!😂

Slogan? Stupid kabisa.
 
Munatumia nguvu nyingi mno kuyafanya mambo ya kijinga na ya kipumbavu, yaonekane kuwa ni mambo ya kawaida kabisa!
 
Kuna watu tangu January mpaka Desemba ni thread za kipuuzi tu. Si bora uanzishe thread za Kubet?
 
Nilikuwa naandika na kufuta oansasa nineshindwa kuposti chochote
 
umenkumbusha upuuzi walikua wanaongea, sjui fly over hazina kazi, yaani kwa kifupi niwaone wanavuka pale ubungo hawataamini mawe watakayopata
 
Msijibaraguze hoja iliyopo mezani ni wapi mlizipeleka zile 74b za Mabeberu...wenyewe wanataka maelezo ya kina.
 
Tunakaribia kumaliza mwezi toka mlipotudhulumu haki yetu ya kuchagua, hatuoni hiyo kazi mnayosema zaidi ya kutupandishia bei ya saruji na sasa wakuu wenu wameanza kukimbizana na wauzaji kama walivyofanya kwenye sukari
 
Back
Top Bottom