Uchaguzi 2020 Slogan ya Hapa kazi tu ni bora kuliko za vyama vingine ni rahisi kuielewa na ilisaidia CCM kushinda

Uchaguzi 2020 Slogan ya Hapa kazi tu ni bora kuliko za vyama vingine ni rahisi kuielewa na ilisaidia CCM kushinda

Hakika wizi wa kura unawaumiza watu flan flan .katka iman yangu ukitenda dhambi na ukagundua hii ni dhambi unafanya majuto kamili na una ungama.kama dhambi ni wizi au uharbifu flan unatakiwa urudishevulicho iba na Kama ni dhuluma au uharbifu flan Iunatakiwa ufidie gharama.sasa Kama uko dhuluma watu uka pora ushindi wao ukaiba kura.ukawaua na kuwapiga wanao lalamika ukitaka kutubu utaratibu ukoje ?naomba msaada hapo ili tusaudie watu flani flani hawana Aman kabisa.
 
Tunakaribia kumaliza mwezi toka mlipotudhulumu haki yetu ya kuchagua, hatuoni hiyo kazi mnayosema zaidi ya kutupandishia bei ya saruji na sasa wakuu wenu wameanza kukimbizana na wauzaji kama walivyofanya kwenye sukari
Mlijidhulumu wenyewe kwa sera zenu zisizochagulika na zisizo na mashiko wala maslahi mapana ya taifa. Tangu lini raia wazalendo wakachagua machafuko na maandamano halafu wakaacha amani & maendeleo???
 
Mlijidhulumu wenyewe kwa sera zenu zisizochagulika na zisizo na mashiko wala maslahi mapana ya taifa. Tangu lini raia wazalendo wakachagua machafuko na maandamano halafu wakaacha amani & maendeleo???
kwahiyo malipo yetu ni kupandishiwa bei ya saruji?
 
CCM at its highest stupidity again pamoja na kuwa na viongozi wenye PhD wengi kuliko nchi yoyote duniani! Hapa kazi tu ni kauli mbiu ya kijinga kwa sababu haina time factor ambayo ni muhimu kisayansi: work = load x distance x time ndo maana Miradi mingi ya Awamu hii inatajwa tu (haionekani) au haikamiliki na wateuliwa wamefanya kauli mbiu yenu kuwa wimbo wa taifa. Mfano mmoja tosha: SGR inatakiwa ifike Uvinza na Mwanza kupitia Dodoma na Tabora na imeanza kujengwa mwanzoni mwa Awamu hii lakini hata Morogoro haijulikani itafika lini. Wakati wa Nyerere tulikuwa na kauli mbiu: Linalowezekana Leo Lisingoje Kesho, hii kisayansi inaeleweka na kukubalika maana ina time element. Kama kauli mbiu ya CCM ingekuwa: Hapa Kazi Tu Sasa au Leo, mngeeleweka na SGR ingekuwa inaelekea Mwanza toka Tabora, Stiegler's Gorge ingekuwa inajaza maji, madege yangekuwa yanaruka, Chato Airport ingekuwa imekamilika na Burigi National Park ingekuwa inajaa watalii. Kauli mbiu za ACT Wazalendo na CHADEMA ni sahihi kabisa kwa sababu kuna wakulima wengi wenye kipato kikubwa kuliko mfanyakazi yeyote wa kuajiriwa na wakulima hawa walioendelea ndo wanaweza kuchangia maendeleo. Arusha, Moshi, Mwanza, Tanga nk ni miji iliyoendelea siku nyingi kwa mchango wa wakulima wa Kahawa, Pamba na Mkonge. Tukiwa hapahapa na ng'ombe zetu na wake zetu wengi na watoto wetu lukuki tukangoja wazungu walioendelea waje watujengee reli, Ikulu, Shule, barabara nk. Wasukuma (chapa ng'ombe) Wana ng'ombe wengi mpaka mahari inafika ng'ombe 40 lakini nyumba zao zimekandikwa kwa kinyesi cha haohao ng'ombe na kuezekwa kwa nyasi huku wanafamilia wote wakilalia ngozi ya ng'ombe. Kule Ulaya Manor houses (nyumba za wakulima) zilizojengwa na wakulima wenyewe ni nzuri sana kuliko hayo mabox (highrise) ya mijini tunayoyaona na kujigamba kuwa ndo maendeleo. Maendeleo yana Chama siyo cha CCM!
Wewe ni tofauti sana na BAVICHA wengi -- possibly, uko hatua za juu katika political maturity. Why? Kwa sababu unakiri wazi serikali ya JPM imefanya wonders kwa miradi mikubwa sana ya maendeleo. Unajua kilichomkosesha kura Mr Mzungu ni pale alipowahadaa raia kwamba JPM hakufanya lolote la maendeleo, ilhali wananchi wanamchora tuu na kumlia taimu. Nadhani ungegombea wewe, nani ajuaye, things could have been a little bit more encouraging in the ballot box. Nashauri 2025 Twende na Swela!!!
 
Ili kushinda uchaguzi slogan huwa pia na mchango mkubwa

Slogan mfano us ACT wazaledo ya Kazi na Bata ilikuwa hata haileweki inalenga nani Mkulima,mfanyabiashara,machinga ,wavuvi,, wafugaji, au wafanyakazi? Ukiingalia ililenga wafanyakazi wa serikali tu ambao idadi yao ni laki nne tu sio jamii nzima ya watanzania

Ukija slogan ya Chadema ya maendeleo ya watu sip vitu imekaa kivituko na haieleweki kirahisi unatakiwa kuwa na Phd kuielewa sababu watu wanahitaji vitu mfano barabara, hospitali, shule nk wewe unasema sio yanatakiwa maedeleo ya watu. Watu wanajiuliza hayo maendeleo ya watu Yakoje? Toeni mifano mna wabunge wenu Chadema wamekaa miaka kumi hadi kumi na tano bungeni ni maendeleo yepi ya watu waliyoleta majimboni mwao tuone mfano kuwa yanafananaje? Unakuta hakuna wabunge wa Chadema hawakupeleka maendeleo ya vitu wala ya watu miaka yote waliyokaa bungeni. Hivyo hiyo Slogan ilichangia pia wananchi kuwanyima kura chadema sababu ilikosa ushahidi wa walichofanya nyuma cha maendeleo ya Watu

CCM slogan ya hapa kazi tu ilibeba ushahidi wa vitu vilivyofanyiiwa kazi Barabara,reli,mashule,vituo vya afya, umeme nk pia slogan hiyo ni nyeyekevu kuwa tupeni kura tukafanye kazi sio tukafanye kazi na kula bata kama ile ya ACT wazalendo ya kazi na bata!!!

Hii Slogan ya Hapa kazi tu ni vizuri iwekwe hadi kwenye nembo ya CCM iwe ya kudumu
Slogan haikuisadia CCM kushinda. Ni mapolisi!
 
Unachokizungumza ni kweli kabisa.

Slogan au Kauli mbiu ina nafasi kubwa sana ya kumbeba mgombea ili watu wamuelewe na wamkubali pia.

Fikiria Mh Jakaya M Kikwete alitumia "Hali Mpya, Nguvu Mpya na Kasi Kubwa"

Mh Dkt. John Pombe Maguuli alitumia "Hapa Kazi Tu"

Sasa njoo kwa ACT, CUF, TLP, NCCR MAGEUZI, CHADEMA nk...UTACHEKAAA!

Kuna vitu huwa vinachangia mgombea kushinda;
1. Muonekano au sifa za mgombea mwenyewe, Je, mgombea anauzika kwa wananchi? Kuna wagombea hata uwabebe vipi huwa hawabebeki kirahisi maana wamejaa makandokando mengi na udhaiu mwingi.

2. Slogan au Kauli Mbiu au MOTTO. Mgombea anatumia msimamo gani kuwashawishi watu ili wakupe dhamana.

3. Budget au Bajeti ya kampeni. Utafiti unaonesha kwamba ili mgombea agombee nafasi ya Rais na ashinde nin lazima awe amejipanga kwenye bajeti ya kampeni zake. Bajeti hiyo ni lazima iwe sawa na Pato la Taifa la mwezi mmoja. Sasa piga mahesabu, pato la mwezi la Tanzania ni Bilioni ngapi, baada ya hapo fuatilia bajeti ya kampeni ya CCM ni Tsh ngapi, na ACT, CHADEMA, TLP, CHAUMA, NCCR MAGEUZI nk.

Kampeni inahitaji matangazo ya mitandaoni na ya kubandikwa kwenye mitaa. Kwa mujibu wa TRA mabango ya wagombea wote ya kunandikwa mitraani yanalipiwa, Je, Tundu Lissu, na Benard Membe mwaka huu walibandika mabango mangapi? Wakati huo huo Mgombea wa CCM ukifuatilia bajeti ya mabango yake ya mitaani ni zaidi ya Bilioni moja.

Njoo kwenye bajeti ya kulipia vyombo vya habari vya kumtangaza mgombea kama Redio, TV, Magazeti, Online medias nk

Njoo bajeti ya usafiri na malazi na idadi ya watu wa kukupigia kampeni maana ukitembea mgombea pekee yako hakika hutaweza, La sivyo uwe kama mgombea wa CHAUMA na mambo ya UBWABWA (haahahhahha).

Moja ya vilivyompa ushindi Barrack Obama ni kuchangiwa michango mingi kwa wadau wake wa Democratic, hata Hillary Clinton, na hata Joe Biden pia.

4. SERA, ILANI, AHADI, unasema ukishinda utafanya nini kwa Taifa. ACT Wazalendo wametoa ILANI ya uchaguzi katikati ya kampeni, kweli mtashinda? Wakati huo huo CHADEMA wamekuja na sera mbovu za ajabu sana.

5. Watu gani wapo nyuma yako, na ni aina gani ya watu wanaoku support? Watu gani wanakusemea vizuri ili ushinde? Tundun Lissu anasemewa na Askofu Bagonza, Mwamakula, na Ponda ambao hata dini zao zimewakana wazi, mbaya zaidi Ponda anasema kuwa Waislamu wote wapo upande wa Tundu Lissu. Hii ni akili kweli? Tundu Lissu hakujifunza tu kwa Edward Lowassa mwaka 2015 aliposema hii i zamu ya Walutheri? Hii kauli ilichangia kumpiga Lowassa maana alionekana wazi anaeneza udini na ataleta udini. Tanzania siyo nchi ya kidini, Tanzania haiongozwi kidini au kikabila au kikanda au kimila.

6.
7.
8.
Yapo mambo mengi sana, mimi nimeahngia kidogo tu
 
Msijibaraguze hoja iliyopo mezani ni wapi mlizipeleka zile 74b za Mabeberu...wenyewe wanataka maelezo ya kina.
Tunakaribia kumaliza mwezi toka mlipotudhulumu haki yetu ya kuchagua, hatuoni hiyo kazi mnayosema zaidi ya kutupandishia bei ya saruji na sasa wakuu wenu wameanza kukimbizana na wauzaji kama walivyofanya kwenye sukari
Wewe uko nchi gani? fuatilia vyombo vya habari ujue yaliyojiri au kama vipi tembelea kurasa za twitter na instagram za OWT - Ofisi ya Waziri Mkuu Tanzania.

Sidhani kama mfuko wa saruji unazidi 17,000. Ni kati ya 15,000 - 17,000.

Lakini pia jana Mh Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameanya kikao kupitia Video Conferencing na Wakuu wa Mikoa yote Tanzania kukagua na kuhakikisha saruji haipendi bei na bei yake inakuwa kama awali kabla ya uchaguzi maana hakuna ongezeko la kodi.

Hayo mengine muwe mnaongea baada ya kuhakikisha kuwa yana ukweli ili tusipotoshe umma wa watanzania.
 
Back
Top Bottom