Chief-Mkwawa
Platinum Member
- May 25, 2011
- 31,559
- 42,179
Duos 2 unayoizungumzia ni ipi mkuu?
Wakubwa naomba mnijulishe brand ya smartphone yoyote ibayouzwa chini ya laki.
Kitu Tecno na oking 45,000 Tu
yenye cortex a9 1.2ghz dual core icheki link hii
Samsung Galaxy S Duos 2 S7582 - Full phone specifications
mkuu mkwawa, simu yangu p5 tayari imegoma. nimereset lkn wapi. na zile assistant program zote sizioni.
vipi nikijikim kwa hizo huwei zinazotangazwa na tigo?
1. je nikinunua zinaweza kuwa connected na line nyingine? kuna moja nilinunua ukiconect net na line nyingine haikubali hadi tigo japo ilikuwa duo's.
2. vipi kuhusu hizo zinazotangazwa na Airtel? zipi nzuri zikishindanishwa na za tigo?
kwa hali ilivyo, ulimwengu wa digital hauepukiki.
Samahani kazi yahiyo cortex kwny simu nini
cortex ni jina la series ya processor za arm. unapoongelea proceesor ndio mfanyakazi wa simu kila kitu kuanzia ukiangalia video, ukifungua application, ukipiga picha na hata ukiingia internet ni processor inayofanikisha hivyo vitu. sababu hii cortex ni series ina maana zipo nyingi kuna kuanzia
cortex A5
cortex A7
cortex A8
cortex A9
cortex A12
cortex A15
cortex A17
hizo ndio cortex maarufu.
pia hizi series za processor za cortex ni open source mtu yoyote anaweza kuzitumia
Samahani, nimekuwa "mvivu" kidogo kuendelea na utafiti kutokana ka muongozo ulioweka hapo juu. Ningeweza ingia kwenye mitandao na kufanya utafiti zaidi, ila sababu wewe ni mtaalam zaidi wa simu basi ngoja tu nikuulize: Ukitoa hizo processor za arm (cortex), kuna aina nyingine ya processor za simu na kwa sasa simu ambayo ina speed kubwa kabisa ina processor speed kiasi gani? ASANTE.
Vipi kuhusu hizi simu za clone?
Mkuu mim natumia huawei y 220 unaweza ukanipa sifa zake na huwa inasumbua fb pmj na watsup kwenye kudownload
arm ndio pekee kama vile kwa pc x86 ndio pekee. ila nimeeleza hapo juu kuwa ni open source hivyo watengeneza processor za simu wanazitumia na kumodify wanavyotaka.
cortex yenye speed kuliko zote kwa sasa ni cortex a15, ila soon tunategemea cortex za 64bit ambazo zitakuwa na speed zaidi.
hii cortex 15 qualcom wameimodify wakaipa power zaidi na kuiita krait.
hivyo kukujibu swali lako processor ya simu yenye speed zaidi ni ile yenye cortex a15 au krait. hizi hapa chini ndio chip zenye hii processor ambazo ni latest.
1.snapdragon 800/801/805 ndio yenye speed zaidi iliyotengenezwa na qualcom
2.exynos 5 octa ndio yenye speed zaidi ya samsung
3. tegra k1 ndio yenye speed zaidi nvidia
4. MT6795 hii ni ya mediatek wamejitahidi pia
5.kirin 920 hii ya huawei
ila overall naipa snapdragon 805 kama king wa processor za simu
update
processor zote hapo juu zinakuja kwenye configuration ya quadcore (4) au octacore(8) na clock speed 2ghz hadi 2.5ghz