Smartphone za Oppo na Vivo zipo underrated sana. Wana vyuma vina camera iPhone yoyote haiweki mguu!

Hii TZ imefika kweli au ndo mpaka uagize nje
Wafanyanyabiashara waoga sana kuleta simu za Oppo, Vivo, Tecno, Huawei za bei kubwa.

Wanajua Mtanzania kutoa Mil 1 anunue Vivo bora akanunue iPhone 13 base used.

Kwahiyo tukienda madukani tunakutana na zile za bei ya kati.

Kama mtu unaweza kujiripua unaagiza. Kuna kipindi tuliagiza Huawei ilikua poa tatizo gharama za kutuma nazo juu, nakumbuka ilikua 80,000 hivi.
 
Tuanzie hapa kwanza,flagship mnamaanisha nini?
 
Tuanzie hapa kwanza,flagship mnamaanisha nini?
Ili unielewe kirahisi chukua huu mtiriko:

1. Toyota Prado V8 - Flagship

2. Toyota Harrier - Mid-range

3. Toyota IST - Low-range

Flagship ni bidhaa ya kampuni yoyote iliyo na ubora wa hali ya juu kabisa, yani ukiitoa hiyo bidhaa hakuna nyingine yenye kiwango kuizidi hiyo.
 
Hapa ukiiotea S24 used ndiyo kabisaa unakuwa umeula balaa, maana kwanza inakuwa imebakiza 6 years of major OS updates...

Unyama mwingi mwaisa.
 
Better kuagiza tu nje
 
Nimekuelewa vizur sana,shukran
 
Siwafundishi tena, Ukiteswa na bando, Huo ni uzembe wako, kwa halotel Pata GB2 kwa 3000, Gb3 kwa 4000, GB5 kwa 5000, Gb7 kwa 7000, Gb10 kwa 10000, Gb15 kwa 14,000, Gb20 kwa 19,000, Gb25 kwa 23000 na Gb30 kwa 26000 tu mwezi mzima. 0618370992.
 
Unachosema ni sahihi. Mimi ni team HUAWEI.
August hii nimevuta huawei p30 pro ambayo ni flagship ya 2019 sina habari kwa miaka 5 ijayo
 
Price ya 22 na 23 zinaweza kucheza kwenye sh ngapi.
1. Boxed
2. Unboxed(second hand n.k)
 
Nilikua natafuta tu S23U naona bei bado za moto. Tuone hadi January ikiisha.

Mi nikinunua S23U navuka nayo 4 years aisee.
23u inamwonekano mzuti sana betri kubwa. Ni kama unatumia note series. Kio kikubwa n.k. bei inasemaje hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…