SMS gani ukiandikiwa na mtu unakereka

SMS gani ukiandikiwa na mtu unakereka

Wale wajinga wa "ile pesa tuma kwenye namba hii".
Nazichukia hiz texts balaa.
Screenshot_20241109_174812_Messages.jpg
 
1.Wale wa X badala ya S
2.Namba mpya "Guess mimi ni nani ?"
3.Namba mpya inakutafuta badala ya kujitambulisha inasubiri uanze kuuliza wewe nani..Huwa siulizi..Mambo ni mengi sana unapata namba ya mtu unamtafuta unategemea aanze kukuuliza wewe nani serious?
Acha tukae kimya mpaka utakapoona inafaa wewe kujitambulisha.Tutapeana salamu kawaida kabisa lakini sitakuuliza wewe ni nani.Never.
4....."Nisave XYZ uone status zangu nina biashara"..Which biashara??,How???
Unauza bhangi inbox ??? Husemi aina ya biashara wengine hatuview status mara nyingi hivyo na hatupost..Biashara ambazo hazina maelezo yoyote yanayoeleweka.
5.Wanaoweka "H" kila mwisho wa neno
Mf "Mamboh ,vipih,ukoh poah"
Unatamani umwambie "Huko shule ulienda kusomea ujinga" 🤣🤣
 
Wajinga wengi. Asilimia kubwa kwenye jamii wanaandika hivyo (x baadala ya s), tena kwa mwandiko mbovu wa kukatakata.

Unakuta mtu anatumia smartphone, tena kajiunga kifurushi cha mwezi mzima cha SMS nyingi ambazo hata atumie kwa fujo vipi, SMS haziishi. Cha ajabu anaandika kwa mkato unafikiri kajiunga kifurushi cha SMS 10.

Mijitu dizaini hiyo huwa sijibu SMS zao, halafu napata lawama kwamba nina dharau.
 
Kuna jamaa alikuwa hajui kusoma na kuandika lakini alinunua simu akawa anjaribu kukariri SMS za jamaa mmoja, katika harakati za kukariri aliambulia neno 'vp' siku iliyofuata alimchatisha demu wake kwa kutumia neno alliloliiga bila kujua kuwa alishalisahau, aliandika PV badala y VP akawa kibonzo mtaani.
 
Kuna manzi flan ilikuwa akikutumia message ukaijibu, kinafatia kizinga Cha maana😂 nlchukiaga sana kuona message zake yule manz
 
Kuna baadhi ya watu wanekerwa na SMS wanazoandikiwa na ndugu, jamaa, marafiki, wapenzi (mademu)nk.

Kuna rafiki yangu anakerwa na SMS zenye herufi 'X' inayokaa badala ya 'S' mfano mtu anaandika xamia xuluhu (samia suluhu), kuna jamaa mwingine anachukia SMS zenye tarakimu/namba mfano 2taonana (tutaonana).

Binafsi nilishamfukuza mke wangu wa ndoa baada ya kunifowadia SMS iliyoishia kwa kusema "tuma ujumbe huu kwa watu kumi (10), usipofanya hivyo hutaona uso wa bwana".

Wewe hupendi ujumbe wa namba gani? Sema.
Ya kirungu wakati mwenyewe hali hoi bin taabani
 
Back
Top Bottom