SMS gani ukiandikiwa na mtu unakereka

Vifupisho vya kivivu mfano mamb, vp, gd (mambo,vipi, good)
Kubadili herufi mfano xx, xhule, xim (sisi, shule, simu)
Herufi kubwa tupu bila sababu
Alama za uandishi pahala siyo pake mfano ndiyo...!!!!, Wapi???
Kuongeza herufi za mwisho mfano badooo, sokoniii, kakaa
Maneno fulani fulani mfano best, kipenzi, nk
Mtu kuandika kwa lafudhi anayoongea mfano taadhali, apana, nk

Kinachokera kuliko ni mambo yote hayo yakifanywa na dume zima
 
Kuna mmoja juzi kana na mapya, eti ananiandikia " VP qaqa" akimaanisha 'vipi kaka'.
Aise nilimlamba makofi mpaka akiniahidi kuwa hatarudia kuandika vile tena.

Kila mama amkanye mwanae kabla sijamkanya mwenyewe.
 
Yeye: Oi inakuaje kijana?
Mimi: Safi tu, inakuaje kijana?
Yeye: Fresh
Ukimya wa dakika 10
Yeye: Niambie kijana mishe zinaendaje

Huu ujinga siwezi jibu hata iweje, toa salamu mambo yaishe. Maongezi mengine kama ni ya muhimu piga simu. Unataka nianze kuelezea jinsi mambo-issues zangu zinavyoendelea kwenye meseji for what?
 
Hahahah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…