SMZ: Kuna ongezeko la uhamiaji holela wa watoto kutoka Tanzania Bara kuja Zanzibar

SMZ: Kuna ongezeko la uhamiaji holela wa watoto kutoka Tanzania Bara kuja Zanzibar

Amesema mwaka jana watoto 66 waligunduliwa mitaani baada ya kuingia Zanzibar kwa njia zisizo halali kutoka Tanzania Bara.

Kama ni hivi huwa sielewi maana ya muungano kabisa🤔🤔
NILIPO SEMA HUMU KUWA HUU MUUNGANO NI WAKIANITHI NI KAMA NDOA HARAMU ZA JINSIA MOJA MKANIONA MJINGA
 
Lakini, wazenji huwa wanatuonaje sisi?

Bagamoyo kule kuna wahamiaji haramu wengi tu kutoka Zanzibar lakini sisi hatusemi

Tunakiongozi mkuu kutoka huko, sisi huku tusemeje?
 
Zanzibar na uamsho waliktaa muungano waziwazi wakaitwa magaidi na kupewa kesi wengine walikaa miaka 7 na wengine walikufa kwa huo muungano wenu mnao uona Leo haufai. Sasa wabongo mna double standards za wazi na za kinafki tu kwa maana kitu kikiwanufaisha mnakaa kimya ila kikianza kula kwenu ndio mnashtuka usingizi wa kinafki
 
Hawana taratibu za ku deal na watoto wa mitaani ? Kama hawana basi wafanye wawe nazo na kama zipo basi wazifuate...

Kama issue ni umasikini na hizi Serikali zote mbili zimekuwa na uongozi ule ule tangia uhuru basi ni kwamba wamefeli sehemu fulani.
 
Serikali inapata hasara sana kila mwaka kuwarejesha wahamiaji haramu tanganyika
 
Serikali ya Zanzibar imesema kuna ongezeko la uhamiaji holela wa watoto kutoka Tanzania Bara kwenda Zanzibar unaochangiwa na umaskini na unyanyasaji.

Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Zanzibar, Abeida Rashid ametoa kauli hiyo wakati wa mazungumzo ya kitaifa ya kushughulikia uhamiaji haramu na kuimarisha ulinzi wa wahamiaji wanaoishi katika mazingira hatarishi Tanzania.

Amesema mwaka jana watoto 66 waligunduliwa mitaani baada ya kuingia Zanzibar kwa njia zisizo halali kutoka Tanzania Bara.
“Kuanzia Januari hadi mwezi huu, tuliwakuta 19 ambao wamepelekwa kwenye nyumba salama ambako wanapata mafunzo muhimu ili kujikimu,” amesema.

Chanzo: The Citizen Tanzania
Njia zisizo halali.
Asante
 
hakuna shida ni sehemu ya muungano, watoto wameona mbali, kuna asali nyingi imetoka huku imeenda kule, wacha waifate hukohuko shekhe, ushanifaham eeh
 
Umewahi kuona wanatoa ufadhili wa kwenda kusoma Uarabuni? waarabu wenyewe wanasoma Uingereza wengi
Ufadhili wa masomo huonekana wapi ambako hakuna scholarship za arabuni!?.. nimekuuliza hakuna shule arabuni!?..nyinyi watanganyika mnaizidi nchi gani ya kiarabu kitaaluma/elimu?
 
Muungano wa ajabu sana, huku Tanganyika wahamihaji haramu kutoka visiwani mpaka wanashika hatamu!
 
Back
Top Bottom