Huyu ni msanii mkubwa sana, anaye heshimika kwenye anga za rap&hiphop music na ni kati ya wanamuziki wachache sana waliobaki ukiachilia mbali wale waliokwisha tangulia mbele za haki kama tupac& biggy.
Nyie mnaodai snoop ni mzee, mnajua kati ya Jayz na Snoop nani mzee?
Kwa wasio mfahamu, huyu ni kati ya wasanii wenye washabiki wengi sana duniani, na wala clouds hawajakosea kumleta na hii kazi clouds wala hawajaanza jana, kifupi wanaijua kuliko mnavyofikili nyinyi.
Ukisema clouds hawana hela ndiomana wanamleta msanii aliyechuja si kweli, kwani waliwaleta G unit, rick ross na wengine wengi tu wakiwa bado kwenye peak, mkumbuke hawa international artist mara nyingi ratiba zao zinakuwa finyu sana, tena hasa kwa sisi wa dunia ya tatu, kama tulivyoona kwa criss brown au hata Diamond kwa sasa.
Kama hamuamini njooni hiyo tarehe 5 pale leaders muone hilo shangwe lake.
Nyie wa zama hizi za akina meek mill,sijui Tyga mjue tu wanamuki sasa hivi hakuna, umebakia ujanja ujanja tu kama vile bongo ku survive.😀