Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 9,140
- 15,963
Hili soko ni la muda mrefu tena tangu baada ya uhuru, na lipo katikati ya jiji mita chache tu toka ilipo stand kubwa ya mabasi, lakini haliendani kabisa na sura ya jiji.
Muundo wa soko ni wa kizamani kuanzia nje hadi ndani ambapo vizimba ni vidogo vidogo na wafanyabiashara wengine wamejijengea wanavyojuwa wenyewe ndani ya Soko hilo.
Jiji la Arusha limekuwa likikusanya mapato miaka yote lakini hakuna uboreshaji au upanuzi wa soko hilo kuwa la kisasa ili liweze endana na hadhi ya jiji.
Soko hili limekuwa kikitembelewa na watalii na hata kununua bidhaa humo sokoni.
Jiji kama Dar es Salaam masoko yake yanaendana sana na hadhi ya jiji hilo mfano wa soko kuu kisutu, soko la kariakoo, Machinga complex.
Masoko karibia yote Arusha yapo katika Muundo wa vibanda vibanda na sio muundo wa jengo la soko
Ni vizuri halmashauri ya jiji la Arusha kwa kutumia mapato yake ya ndani kufanya ujenzi wa soko kubwa na wenye hadhi unaoendana na jiji hili la kitalii na sio kusubiri kuambiwa toka juu .
mpangilio wa soko kuu kwa ndani
Soko kuu kwa nje