Soko kuu Arusha halina hadhi ya kuitwa soko kuu

Soko kuu Arusha halina hadhi ya kuitwa soko kuu

Onyesheni huko mnapopaita "pamepangiliwa"
 
Halafu miaka ya nyuma nilikuwa nikiingia huko kuna giza, hivi lile giza la hata saa sita mchana liliisha?
 
Kumbe unafahamu Arusha hakuna kitu lkn huwa unajifanya hujui.
🤣🤣🤣 sio hakuna kitu ila ni nyuma ya dar na mwanza kwa ukubwa wa mji na huo ndio ukweli
lakini pamoja na hayo inapitwa miundombinu hadi na iringa na morogoro 😥
 
Nyie si mnapesa wachapa kazi kuliko race yoyote hapa Tanzania, jengeni soko lenu na stendi yenu.
hizo chuki ndio zinaturudisha nyuma ndugu yangu kitombile
Arusha ndio imebeba taswira ya nchi yetu kwa utalii
zaidi ya asilimia 80 ya watalii wote Tanzania bara wanaenda Arusha
lakini pesa ya makusanyo yao ndio yanajenga vituo vya afya vijijini huko
kama serikali ipo serious na utalii alafu mji wa utalii unakosa stendi ni aibu kwa nchi yetu yote boss
watu wa Arusha sisi tuko sawa na lifestyle yetu hata magari yapaki barabarani sawa tu
ila wageni sasa ndio wanapata kadhia kubwa
na hapa ndipo wanasema adui yako mpende tu
kwa sababu mgeni akija anajua kaja Tanzania na sifa mbovu inaenda kwa nchi
kwa sekta binafsi Arusha wamejitahidi sana kutengeneza hoteli na sehemu za burudani lakini kwa upande wa serikali inasikitisha
Hatuta fika mahali kama taifa kama tukibaguana sisi kwa sisi
 
🤣🤣🤣 sio hakuna kitu ila ni nyuma ya dar na mwanza kwa ukubwa wa mji na huo ndio ukweli
lakini pamoja na hayo inapitwa miundombinu hadi na iringa na morogoro 😥
Hakika wewe ni simba kumbe ukweli ulikuwa unaufahamu alafu unachelewa kusema🤣🤣🤣
 
hizo chuki ndio zinaturudisha nyuma ndugu yangu kitombile
Arusha ndio imebeba taswira ya nchi yetu kwa utalii
zaidi ya asilimia 80 ya watalii wote Tanzania bara wanaenda Arusha
lakini pesa ya makusanyo yao ndio yanajenga vituo vya afya vijijini huko
kama serikali ipo serious na utalii alafu mji wa utalii unakosa stendi ni aibu kwa nchi yetu yote boss
watu wa Arusha sisi tuko sawa na lifestyle yetu hata magari yapaki barabarani sawa tu
ila wageni sasa ndio wanapata kadhia kubwa
na hapa ndipo wanasema adui yako mpende tu
kwa sababu mgeni akija anajua kaja Tanzania na sifa mbovu inaenda kwa nchi
kwa sekta binafsi Arusha wamejitahidi sana kutengeneza hoteli na sehemu za burudani lakini kwa upande wa serikali inasikitisha
Hatuta fika mahali kama taifa kama tukibaguana sisi kwa sisi
Rafiki yangu mdazi, unaijua Serengeti?
 
unataka kusema kuwa watalii wanaoenda serengeti wanapitia mwanza sio Arusha 😥
Musoma wanajenga uwanja wa ndege pia na hoteli za kitalii kwaajili ya mbuga yao ya serengeti sasa kila mtu ale urefu wa kamba yake.
 
Vi hiace vyao ni vipanki. Mwanza tunatoq nje ya mji hizi super roof tunaweka huko bado wako super panki.
Hizi panki mie hapa mza nazikumbuka miaka Ile ya early 1990. Mfano zile za kwenda mabatini ama mwaloni stendi ya zamani ndo zimejazana Arusha
Kwa maelezo yako ni wazi kabisa Arusha umeisikia vijiweni, hapo tu kwenye vi hiace ndo pana ukweli

Afu Arusha bado mji uko local Sana Mana wenyeji ni wengi kuliko wageni
Nakusahisha hapo kwenye Mji, Arusha sio mji bali ni Jiji, Kuna wakaazi wengi sana katika maeneo mengi,
yaani ukiweka hata biashara zako mpaka wajue wewe ni mtu wa wapi.
Acha uwongo, kama hujawahi kufika Arusha kaa kimya tu, hakuna hayo mambo Arusha, watu kibao tu kutoka matabaka na makabila mbali mbali wanafanya biashara zao Arusha bila shida, Nilikaa Arusha miaka minne na sijawahi kuona huu upuuzi.
Arusha stendi kuu ndo usiseme ni uchafu bangi zinanuka kila Kona.
Hujawahi kufika Arusha mkuu, heri ukae kimya tu, Stendi ya Arusha ni ndogo lakini si chafu. Hizo bangi ukizisikia vijiweni usidhani zinavutwa kokote, Stendi ipo kati mjini pale, wanaovuta bangi labda wanaenda kule opposite na uwanja wa karume (kama bado hapajajengwa), hakuna mvuta bangi anavuta bangi kiwazi wazi ma hata huko wanakonunua wakijua una hii tabia hawakuuzii.
Vijana wa Arusha ni wavivu Sana wanategemewa kubebea na Bibi wa kizungu kwa kufuga Rasta.
Hujui kitu kuhusu A town, heri ufunge hilo bakuli mkuu, Vijana wa Arusha ni wavivu ??? acha kuchafua watu wa Arusha, Hao wanaowinda wazungu wapo wachache sana hawafikii hata asilimia 1 ya vijana wa Arusha, ila bado hawa sio vi ben ten vinavyo nunuliwa iphone na kuridhika, hawa ni level nyingine, ndoano zikinasa wanasafiri kwenda kuanza maisha ulaya na kama ni kiuchumi huwa hawapigi hatua bali wanachana msamba.
Mji ambao ukiongea na mtu anataka kujua wewe ni wa wapi.
Haya unayatoa wapi, ni kijiweni au?? Nimekaa Arusha miaka minne na kuzoeana na wana arusha wengi tu, haya mambo katika watu 10 utaokutana nao labda ni 1 tu
Pia Arusha ni ndogo Sana hata nyakato inaizidi basi tu.
We ni mshamba sana mkuu, yaelekea unatumia kitochi kuingia jf, huenda hata huijui google maps
Pia wanapenda Sana kushindanisha Mara mza vs Arusha wako kikenya zaidi.baadaye mtaanza kushindanisha USA river vs ngarenaro ya juu or ya chini
Yale yale tu ya vijiweni, punguza kwenda vijiweni tafuta kazi.
 
Kwa maelezo yako ni wazi kabisa Arusha umeisikia vijiweni, hapo tu kwenye vi hiace ndo pana ukweli

Nakusahisha hapo kwenye Mji, Arusha sio mji bali ni Jiji, Kuna wakaazi wengi sana katika maeneo mengi,

Acha uwongo, kama hujawahi kufika Arusha kaa kimya tu, hakuna hayo mambo Arusha, watu kibao tu kutoka matabaka na makabila mbali mbali wanafanya biashara zao Arusha bila shida, Nilikaa Arusha miaka minne na sijawahi kuona huu upuuzi.

Hujawahi kufika Arusha mkuu, heri ukae kimya tu, Stendi ya Arusha ni ndogo lakini si chafu. Hizo bangi ukizisikia vijiweni usidhani zinavutwa kokote, Stendi ipo kati mjini pale, wanaovuta bangi huwa wanaenda kule opposite na uwanja wa karume, ujui kitu kuhusu Arusha mkuu.

Hujui kitu kuhusu A town, heri ufunge hilo bakuli mkuu, Vijana wa Arusha ni wavivu ??? acha kuchafua watu wa Arusha, Hao wanaowinda wazungu wapo wachache sana hawafikii hata asilimia 1 ya vijana wa Arusha, ila bado hawa sio vi ben ten vinavyo nunuliwa iphone na kuridhika, hawa ni level nyingine, ndoano zikinasa wanasafiri kwenda kuanza maisha ulaya na kama ni kiuchumi huwa hawapigi hatua bali wanachana msamba.

Haya unayatoa wapi, ni kijiweni au?? Nimekaa Arusha miaka minne na kuzoeana na wana arusha wengi tu, haya mambo katika watu 10 utaokutana nao labda ni 1 tu

We ni mshamba sana mkuu, yaelekea unatumia kitochi kuingia jf, huenda hata huijui google maps

Yale yale tu ya vijiweni, punguza kwenda vijiweni tafuta kazi.
🤝🤝🤝🤝
 
Kwahili mkuu ume eleza ukweli Chuga is my home town ila toka madini na utalii vimeyumba mji umeachwa kinyama, masoko yetu hakuna hata moja lina hadhii yote ni machafu, vitu vimepangwa holela holela miundo mbinu hakuna mambo ni hovyo kabisa. Serikali ina bidi iweke jicho kwenye hili tusibishe kutetea vitu ilihali tunaona kabisa mambo sio. Stand nayo ni kama hakuna ila stand ya mkoa utadhania ni kituo cha wilaya flani huko kijiji, gari zina paki kwa shida, eneo dogo, msongamano mkubwa. Kuna haja ya serikali kurenew plan ya huu mji una anza poteza sifa yake.
 
uyu ndugu yangu kitombile hajawahi kufika Arusha msamehe tu ana ule unazi wa kanda ya ziwa😥
hawa watu wanachuki sana na Arusha wanadhani tunashindana nao maskini
Jifariji rafiki yangu kuja kushtuka mji wenu utakuwa kama kilwa kivinje.
 
Hili soko ni la muda mrefu tena tangu baada ya uhuru, na lipo katikati ya jiji mita chache tu toka ilipo stand kubwa ya mabasi, lakini haliendani kabisa na sura ya jiji.

Muundo wa soko ni wa kizamani kuanzia nje hadi ndani ambapo vizimba ni vidogo vidogo na wafanyabiashara wengine wamejijengea wanavyojuwa wenyewe ndani ya Soko hilo.

Jiji la Arusha limekuwa likikusanya mapato miaka yote lakini hakuna uboreshaji au upanuzi wa soko hilo kuwa la kisasa ili liweze endana na hadhi ya jiji.

Soko hili limekuwa kikitembelewa na watalii na hata kununua bidhaa humo sokoni.

Jiji kama Dar es Salaam masoko yake yanaendana sana na hadhi ya jiji hilo mfano wa soko kuu kisutu, soko la kariakoo, Machinga complex.

Masoko karibia yote Arusha yapo katika Muundo wa vibanda vibanda na sio muundo wa jengo la soko

Ni vizuri halmashauri ya jiji la Arusha kwa kutumia mapato yake ya ndani kufanya ujenzi wa soko kubwa na wenye hadhi unaoendana na jiji hili la kitalii na sio kusubiri kuambiwa toka juu .

mpangilio wa soko kuu kwa ndani

View attachment 2069594
View attachment 2069617
Soko kuu kwa nje
Nishawahii kula muuza matunda hapo kimasikhara. Mdada mzuri wa kichaga, nilifikia hotel hapo karibu na stendi Aquiline
 
Haya mambo ya kutegemea serikali ndio kila kitu inachosha na ukweli tunaipa sifa tuu maana haina uwezo huo, naamini watu binafsi wana uwezo wa kujenga soko la maana kuliko hata serikali, tuamke tunaweza kuliko serikali
 
Back
Top Bottom