Soko kuu Arusha halina hadhi ya kuitwa soko kuu

Well said! Arusha imetengwa sana kwenye maendeleo hasa miundo mbinu. Imagine mkoa wenye vitega uchumi vya kutosha halafu miundo mbinu ni yaajabu kabisa. Bus station za Arusha zinasikitisha. Inabidi serikali ikumbuke Arusha katika hili, irudishe fadhila
Jiji linapata Sana hela kupitia kwa wafanyabiashara, utalii, madini lakini miundombinu ni mibovu hakuna mfano wake
 
Well said! Arusha imetengwa sana kwenye maendeleo hasa miundo mbinu. Imagine mkoa wenye vitega uchumi vya kutosha halafu miundo mbinu ni yaajabu kabisa. Bus station za Arusha zinasikitisha. Inabidi serikali ikumbuke Arusha katika hili, irudishe fadhila
Jiji linapata Sana hela kupitia kwa wafanyabiashara, utalii, madini lakini miundombinu ni mibovu
 
Hili soko ni la muda mrefu tena tangu baada ya uhuru, na lipo katikati ya jiji mita chache tu toka ilipo stand kubwa ya mabasi, lakini haliendani kabisa na sura ya jiji.

Muundo wa soko ni wa kizamani kuanzia nje hadi ndani ambapo vizimba ni vidogo vidogo na wafanyabiashara wengine wamejijengea wanavyojuwa wenyewe ndani ya Soko hilo.

Jiji la Arusha limekuwa likikusanya mapato miaka yote lakini hakuna uboreshaji au upanuzi wa soko hilo kuwa la kisasa ili liweze endana na hadhi ya jiji.

Soko hili limekuwa kikitembelewa na watalii na hata kununua bidhaa humo sokoni.

Jiji kama Dar es Salaam masoko yake yanaendana sana na hadhi ya jiji hilo mfano wa soko kuu kisutu, soko la kariakoo, Machinga complex.

Masoko karibia yote Arusha yapo katika Muundo wa vibanda vibanda na sio muundo wa jengo la soko

Ni vizuri halmashauri ya jiji la Arusha kwa kutumia mapato yake ya ndani kufanya ujenzi wa soko kubwa na wenye hadhi unaoendana na jiji hili la kitalii na sio kusubiri kuambiwa toka juu .

mpangilio wa soko kuu kwa ndani

View attachment 2069594
View attachment 2069617

Unatakiwa tu ujue maana ya "neno soko kuu" haihusiani na quality.
 
Screenshot_20220105-095707.png
 
Jiji linapata Sana hela kupitia kwa wafanyabiashara, utalii, madini lakini miundombinu ni mibovu hakuna
Mbona sisi wenyewe tupo peace sana na Arusha yetu. Mmesikia tukipiga kelele kuwa tunashida na Soko jingine au Stand, au kama ni Hiace ndogo kwani zinashida gani. HEBU MTUACHE NA CHUGA YETU, Wooooi!!
 
Ni wavivu hao zile hotel ni wachache wanapata pesa ukabila uko mbele bado hawajastaarabika
Ila wao ndo wa kwanza kusoma na kuelimika ama elimu haijawasaidia.ujue mareale alipishana na jk nyerere. Huyu mjanja msomi alimtangulia new York Ila yeye alienda kuomba Uhuru wa kaskazini sema huyu ambaye hakusoma alienda kuomba Uhuru wa tanganyika na hao hao ndo wanaojidai kuwa walimchangia nauli.
Ila wao wakashindwa kutumia nauli zao wamtangulie kuomba Uhuru. Wangetufanya Kama Kenyatta alivyowafanya wakenya.
Yaani ardhi yenye rutuba wangejimilikisha wao kwanza na marafiki zao.
 
Masoko ya Magomeni, Kisutu, Chato,Lushoto, Morogoro na sasa Kariakoo nk yamejengwa na wenyeji au kodi.za nchi nzima?
Mwendakuzimu hakuleta mradi wote mkubwa Arusha kwa sababu alizozijua mwenyewe
 
Huo mkoa unahitaji nusra ya Mungu. Masoko yote mawili (Soko kuu na soko la kilombero) ni aibu tupu. Hiyo bus stand ndio usiseme. Mji unakuwa, lakini miundo mbinu ipo vilevile. Usiende Sheikh Amri Abeid, ndio kabisa. Nadhani tangu enzi za kocha Mwamwaja (Meneja wa Uwanja zamani) uwanja haujafanyiwa ukarabati wowote. Arusha bado ni manispaa.
 
jiji manake sio miundombinu mkuu ingekua hivyo morogoro ingeshalikua jiji siku nyingi... Arusha imetengwa sana na serikali kwa upande wa huduma za kijamii lakini haizuii ukweli Arusha ndio mji uliochangamka nyuma ya dar
 
Mkuu, labda hiyo ni definition ya kibongobongo. Lakini, tofauti kubwa ya Manispaa na jiji ni Miundo mbinu. Babati haiwezi kufananishwa na Arusha kwa sababu ya miundo mbinu.

Nakubaliana na wewe kwamba Arusha ilitengwa kwa sababu za kisiasa, lakini hata pale ambapo mkoa ulikuwa na viongozi wa CCM (mfano marehemu Mrema) hakuna cha maana kilichofanyika.

Sasa hivi jiji lipo chini ya CCM, ngoja tuone kama kutakuwa na mabadiliko yoyote.
 
Kituo cha abiria hapo Kilombero utacheka utadhani sio Jiji kabisaa...yaani hawafikiri kuweka mazingira bora kwa Wananchi wao ni kukusanya fedha za ushuru na Leseni na kujenga fremu za kupangisha mtaani..
 
Mkuu, labda hiyo ni definition ya kibongobongo. Lakini, tofauti kubwa ya Manispaa na jiji ni Miundo mbinu. Babati haiwezi kufananishwa na Arusha kwa sababu ya miundo mbinu.

Nakubaliana na wewe kwamba Arusha ilitengwa kwa sababu za kisiasa, lakini hata pale ambapo mkoa ulikuwa na viongozi wa CCM (mfano marehemu Mrema) hakuna cha maana kilichofanyika.

Sasa hivi jiji lipo chini ya CCM, ngoja tuone kama kutakuwa na mabadiliko yoyote.
Kwa hiyo Arusha ilipewa hadhi ya jiji kwa miundombinu gani iliyokua nayo kipindi kile??
Naomba source ya definition yako ya jiji mkuu?
Jiji ni hadhi mji unayofikia baada ya kufika uwezo wa kujitegemea kiuchumi boss pamoja na idadi kubwa ya watu ndani ya mipaka yake.
Na kwa takwimu Arusha ndio halmashauri ya jiji ya pili kwa idadi kubwa ya watu nyuma ya dar.. Kumbuka Mwanza imemegwa kuwa nyamagana na ilemela kuwa manispaa inayojitegemea kwahiyo kwenye mgao wa fedha wanachkua kila halmashauri kivyake na angalia jinsi miundombinu mwanza inavyojengwa kwa kasi sasa majiji yote yanayofuatia yamepitwa na Arusha kwa idadi ya watu
Sasa baada ya hapo ni jukumu la serikali kuu kuimarisha yale majiji yake ambayo ndio sehemu kwenye watu wengi na mzunguko mkubwa wa fedha na uwekezaji
Kwahio Serikali haijafanya uendelezaji wowote wa msingi kwa miundombinu ya jiji la Arusha hasa Stendi, masoko na viwanja vya mpira lakini bado halizuii Arusha kuwa moja ya miji yenye mchango mkubwa zaidi for Reference nenda kwenye official website ya tra
 
Mkuu, labda hiyo ni definition ya kibongobongo. Lakini, tofauti kubwa ya Manispaa na jiji ni Miundo mbinu. Babati haiwezi kufananishwa na Arusha kwa sababu ya miundo mbinu.

Nakubaliana na wewe kwamba Arusha ilitengwa kwa sababu za kisiasa, lakini hata pale ambapo mkoa ulikuwa na viongozi wa CCM (mfano marehemu Mrema) hakuna cha maana kilichofanyika.

Sasa hivi jiji lipo chini ya CCM, ngoja tuone kama kutakuwa na mabadiliko yoyote.
Kama tungekua na utawala wa kujitegemea Arusha kungekua na lami hadi kwenye vichochoro lakini makusanyo yote yanaenda serikali kuu
Na hasa kwa vile serikali inautambua Arusha kama mji wa tatu nyuma ya Dar na Mwanza tulitegemea serikali kuu iboreshe japo masoko hasa baada ya tra kuingilia asilimia kubwa ya mapato ya halmashauri hivi sasa halmashauri hazina pesa hadi mabango ya matangazo yanakusanywa na tra...ni aibu Arusha taa za barabarani tunashindwa hadi na monduli, masoko mabovu stendi ya daladala ni aibu tupu stendi kubwa hata korogwe wanatupita
Ukweli usipingika Arusha ilinyimwa pesa ya maendeleo kwa makusudi na miradi mikubwa yote iliyopo ilisainiwa enzi za jk kama wa maji, tengeru sakina na tscp ambayo ndio imefanya Arusha kidogo kuwa na barabara za hadhi otherwise Arusha tumesuswa kwa mda sana
 
Masoko ya Magomeni, Kisutu, Chato,Lushoto, Morogoro na sasa Kariakoo nk yamejengwa na wenyeji au kodi.za nchi nzima?
Mwendakuzimu hakuleta mradi wote mkubwa Arusha kwa sababu alizozijua mwenyewe
Well Said
 
Siasa za CCM za ajabu sana. Hii nchi haiwezi kuja kuendelea kwa namna hii. Eti kaskazini ni ngome ya upinzani kwahiyo imetengwa.

Hasa kipindi kile cha mwendakuzimu ndio kabisa hata yeye kukanyaga kaskazini alikuwa hataki kusikia.
Nyie si mnapesa wachapa kazi kuliko race yoyote hapa Tanzania, jengeni soko lenu na stendi yenu.
 
Kama tungekua na utawala wa kujitegemea Arusha kungekua na lami hadi kwenye vichochoro lakini makusanyo yote yanaenda serikali kuu
Na hasa kwa vile serikali inautambua Arusha kama mji wa tatu nyuma ya Dar na Mwanza tulitegemea serikali kuu iboreshe japo masoko hasa baada ya tra kuingilia asilimia kubwa ya mapato ya halmashauri hivi sasa halmashauri hazina pesa hadi mabango ya matangazo yanakusanywa na tra...ni aibu Arusha taa za barabarani tunashindwa hadi na monduli, masoko mabovu stendi ya daladala ni aibu tupu stendi kubwa hata korogwe wanatupita
Ukweli usipingika Arusha ilinyimwa pesa ya maendeleo kwa makusudi na miradi mikubwa yote iliyopo ilisainiwa enzi za jk kama wa maji, tengeru sakina na tscp ambayo ndio imefanya Arusha kidogo kuwa na barabara za hadhi otherwise Arusha tumesuswa kwa mda sana
Kumbe unafahamu Arusha hakuna kitu lkn huwa unajifanya hujui.
 
Back
Top Bottom