Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Mkuu Samaritan, kiukweli Baba wa Taifa iliwahi kutuusia, "umasikini mbaya kabisa ni umasikini wa mawazo!".Hiyo ni nzuri sana, watu wengi huwa wanalalamika kwamba wana mawazo mazuri ila tatizo ni mtaji, huu utakua ni ufumbuzi wa hilo tatizo.
Angalizo, pawe na wataalamu wa kupima na kuangalia uhalisia na utekelezaji wa hayo mawazo kabla watu hawajavunja vibubu kurushia akiba zao huko.
Thanks mkuu Pasco
Kiukweli kabisa, Watanzania wapo wengi wenye good bussiness ideas tatozo ni mitaji!.
Juzi nilikuwa Mtwara, huwezi amini, all major suppliers ni makampuni ya Kenya na Afrika Kusini, kisa suplies wetu wa hapa hawana capacity!, japo sikubahatika kuona hata tangazo moja la zabuni kwenye magezeti yetu, kila kitu ni online!, huwezi amini, hata maji ya kunywa, japo ni haya haya ya Kilimanjaro, supplier ni Mkenya!.
Juzi wameleta malori 200 kubeba mabomba ya gesi, Mtwara na Lindi, hakuna madereva!. Nimeshuhudia baadhi ya mabasi ya abiria wa mikoani ya Youtong madereva ni Wachina!.
Mradi wa mabasi yaendayo kasi, umetangaza tenda ya kutafuta kampuni ya uendeshaji mradi huo, mtashangaa kukuta ni kampuni ya kigeni simply because sisi hatuwezi!.
Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana, CMCA, italisimamia hili!.
Pasco.