Soko la Karume limeungua moto

Wapi nimeandika kuna Zama zimewapenda masikini? Unajiwekea tafsiri zako. Jibu mwenyewe.
Unapo sema zama hizi maana yake kuna zama zile nikumbushe hizo zama ambazo masikini alikula bata
 

Uchumi wa Tanzania thamani yake ni kiasi gani ? Labda tuanzie hapo!
 
Soko la karume si Ni lile la mitumba au sisi wageni twakosea
Ndio hilohilo Tena hilo soko lilianzishwa baada ya mbinde wamachinga walikataa kabisa kuhamia hapo Ila walipohamia watu wakapapenda sababu huduma ya usafiri ilikuwepo na daladala zingine zikawa zinaishia hapo.

Mtu anashika anaingia nyumbani anachagua bidhaa then anasepa. Kiukweli wameumizwa sana Mungu awajalie uvumilivu.

January hii watu wameshusha mzigo mkubwa kwa ajili ya uniform, viatu, mabegi, mashuka ya shule Yani ni hasara kubwa mno.
 
Tulipofikia sasa ,tatizo ni sisi wenyewe wananchi, kuna hatua inabidi tuchukue....

Tuwakatae hawa viongozi kwa vitendo,tukatae hii dhuluma na uonevu wa sasa kwa vitendo.
Hii ndo pointi kuku kuliko zote hapa kwa mwezi huu, uonevu umezidi sana kwa wananchi Wa kawaida, Sahiv inabidi vitendo tu
 
Sawa lakini unafahamu viongozi Wamarekani wanaheshimu katiba sababu wanaogopa wananchi hawataruhusu kunyang'anywa haki zao. Na ukitaka kuhakikisha hili angalia jinsi haki za watu weusi zinavyokuwa ngumu kupatikana ukilinganisha na wazungu wakati wote wapo chini ya katiba na sheria zile zile.
 
Uchumi wa Tanzania thamani yake ni kiasi gani ? Labda tuanzie hapo!
Sasa ndio hapo inasikitisha mtu mmoja au genge la watu wachache kuiba hela nyingi kiasi hicho kwenye nchi maskini na maskini kubakia kulipa hilo deni. Kwenye utawala wake tu nduli Jiwe alikopa zaidi ya trillion 50 na 21 akalamba
 
huenda miongoni mwao wamechoma.
uchunguzi ufanyike mara moja.
kuna wajanja, matapeli, wahuni ambao wanatarajia kuonewa huruma ili walipwe fidia.
 
wenzio kuchomewa moto unafurahia , Nyerere alisema watz hatujapevuka kuimudu siasa ya vyama vingi
Hakuna aliyefurahia. Tatizo watu walishainguza siasa kwa jambo lisilohitaji siasa
 
nashauri hilo soko lihamishiwe Mbezi/Luguruni karibu na stendi ya Maguguli
 
Hiyo sentensi ya mwisho ni ngumu hiyo.kwamb! Tbl walizuiwa kuzima moto?
 
Hivi sisi watanzania ni lini tutaamka kutetea haki zetu. Yaani hawa jamaa wanatupelekesha namna hii alafu bado tunawachekea tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…