Uchaguzi 2020 Sokoine, Mbeya: Magufuli asema Tulia amemsumbua sana kwa ajili ya maendeleo ya Mbeya, amuomba Joseph "Sugu" Mbilinyi kura

Uchaguzi 2020 Sokoine, Mbeya: Magufuli asema Tulia amemsumbua sana kwa ajili ya maendeleo ya Mbeya, amuomba Joseph "Sugu" Mbilinyi kura

We kweli kilaza! piga hesabu kwa watu 10000 kwa malipo ya 5000 ni sh ngapi ? Utawalipa ! Endeeleeni kuweweseka.
Hivi huu ujinga wenu mpaka lini? hujui kama wanafunzi wamefuatwa na mabasi vyuoni? hujui wanafunzi wamevalishwa mafulana na makofia ya kijani? hata hujui jiji kulikuwa na maagizo kwamba lazima wafanyakazi wote waende uwanjani? Hujui kama watu wamesombwa kutoka majimboni vijijini huko? wenye CCM wanajua nguvu wanayoitumia kujaza watu, hata hukumsikiliza maam Maria Nyerere?
 
Leo Dkt. Magufuli anaendelea na kampeni katika mkoa wa Mbeya

Uwanja umefurika wananchi wa itikadi mbalimbali na bendera zao hakika siasa siyo Uadui.

Viongozi mbalimbali wanaendelea kuwasili hapa uwanjani.

=========

View attachment 1585551
MAGUFULI: Mwaka 2015 tulipita hapa kuwaomba kura wana-Mbeya, mlitusikiliza na natambua nilipata kura nyingi sana Mbeya lakini kwa mbunge aliyekuwa wa CCM mkasema hapana, mkanichagulia pia baadhi ya madiwani lakini mkanichagulia wabunge katika maeneo ya Mbeya, Mkanichagulia Kyela, Chunya na maeneo mengine.

Hapa mjini mkasema hapana, niseme kwa dhati, nilisikitika lakini sikuwachukia na nikaja nikaambiwa kwamba, kushindwa kwa CCM katika jiji hili la Mbeya ilitokana na ugomvi wa wana-CCM wenyewe.

Nilichofanya ndugu zangu na nataka niwaeleze hapa leo, kutaka kuhakikisha kwamba Mbeya haipotei kwenye ramani, nilimtafuta mwanamama mmoja msomi aliyekuwa akiitwa Dr. Tulia nikamteua kuwa mbunge kwamba yale yatakayokuwa kuwa yanajitokeza kwa ajili ya Mbeya angalau yawe na msemaji.

Nilipomteua Dr. Tulia kuwa mbunge na ndiye mbunge mmoja wa kwanza niliyemteua, alipoingia bungeni akateuliwa pia kwa nyota aliyokuwa nayo, akateuliwa kuwa naibu spika wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania.




Amefanya kazi zote zilizotakiwa kufanywa na mbunge wa Mbeya, napenda leo kusema kwa hadhara hii Tulia nikushukuru sana kwa sababu ulinisumbua sana kwa ajili ya maendeleo ya Mbeya na kwa sababu leo umekuja mwenyewe na kwa vile sitakuteua tena kwa viti maalum, nimekuleta kwa wazazi wako, dada zako, kaka zako, wazee wako wakusulubu wewe kwa ajili ya kazi zako nzuri.

Nina matumaini makubwa kwa hadhara hii, tofauti zilizopo miongoni mwa wana-Mbeya mtaniletea Dr. Tulia Ackson awe mbunge wa hapa.

Ninayasema haya kwa sababu pamonja na kwamba hakutuchagua hapa Mbeya mjini tuliendelea kufanya kazi kwa manufaa ya wana-Mbeya wote kwa sababu ninafahamu maendeleo hayana chama.

===
MBEYA: MAGUFULI AMUOMBA KURA SUGU

Mgombea Urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM amewaomba kura watu wote, akiwemo Joseph Mbilinyi, mbunge wa Mbeya mjini aliyemaliza muda wake maarufu kama Sugu

Ameyasema hayo alipokuwa Mbeya kwenye mkutano wa kampeni anazoziendeleza kuelekea uchhaguzi mkuu Oktoba 2020

Amesema maendeleo hakuna vyama, dhamira yake ni kuibadilisha Mbeya kabla muda wake haujaisha, ili liwe jiji la mfano kitaifa na kimataifa
Anaemuamini Magufuli akapimwe akili
 
Wakati picha zikianza kurushwa chunguza utofauti wa sehemu foreground, middle ground na background.

Utajua CCM ni wepi, Wapitaji na wapi na Wasio interest ed ni wepi?
You are very observant,there is a clear line separating Truth and A Lie.
 
Wana Mbeya msichague huyu Mama mpiga makofi. Hana lolote.

Kama Magufuli anampenda sana, basi atumie muda huu uliobaki kumpangia kazi nyingine yoyote maana uwezo huo wa kugawagawa na kuhonga vyeo anao
 
Kuna neno limetumika kumuomba "Sugu" kura Leo limeniacha hoi.
Kweli kampeni sio mchezo wallah!
 
Tunaambiwa na tunaonaga watu wanaletwa na mabasi na maroli lakini Mbeya sasa watakuwa wameletwa na treni maana iti isi tuu machi. Tathimi inaonyesha wamefunika kanda ya ziwa hata wale wa Kigoma wanafuata. CCM imeenda mbali hata kuwanunu wenye maduka, mamalishe na wachuuzi wote wako barabarani, wamenunuliwa wapo uwanjani jamani kwanza ni hatari kuwa na msongamano mkubwa hivi unaweza kusababisha watu kuumia bure.
Vile vile CCM imevuka mipaka kwani viongozi wote wa makanisa na misikiti hapa mbeya na waumini wao wamenunuliwa wote na CCM kibya zaidi watu wenyeumri mkubwa pia wamekuja kwa wingi kitu ambacho kuwanunua hawa si vizuri kwani wengine ni wazee sana si wangewaacha wapumzike.
Nasikia ununuaji umevuka kiwango hadi wapiga kura tutanunuliwa, kimsingi tumefika bei acha tu maana viongozi wengi wa upinzani walianza kuunga mkono kitambo nasi tunawafuata
 
Tatizo ni nini..?
JamiiForums1767593501.jpg
 
Naona leo kaenda na adabu... angeleta zile message za wasipochagua CCM hataleta maendeleo ndio angejua kuwa hajui.
 
Back
Top Bottom