It's a law of nature. Mwenye nacho huongezewa. Asiyekuwa nacho, basi anaweza kunyang'anywa hata kidogo alichobahatika kuwa nacho ili achukue mwenye nacho kingi tayari...
Mwinyi anapewa zawadi ya gari aina ya Germany Technology Mercedes Benz na serikali na siyo Mama Samia Suluhu Hassani...
Inashangaza kidogo kwa sababu kiongozi mstaafu kama Mwinyi mwenye privileges na marupurupu kibao na mwenye familia nzuri yenye watoto wenye nyadhifa kubwakubwa na uwezo Mkubwa wa kiuchumi ktk jamii, anashindwaje kujinunulia yeye mwenyewe gari atakalo kwa mahitaji yake kwa gharama zake toka ktk fedha nyingi anazolipwa na serikali wakati wote...?
It doesn't make any sense at all, ... right...?
Mama Samia Suluhu Hassani, Rais wa JMT umeanza kuboronga mapema sana. Unaanza kulewa madaraka mapema sana. Unaanza kuanza kuyatumia madaraka yako ya Urais vibaya mapema sana...!
I am afraid to say that, this is very dangerous move to your presidency...
Nakuhakikishia kuwa, unaweza kuishia kuwa Rais wa hovyo sana pengine kuliko hata Mwendazake Pombe Magufuli...!!
LABDA UNASAHAU HARAKA SANA....
Kumbuka, ni wiki jana tu umetoka Mwanza kwenye sherehe za Mei Mosi. Wafanyakazi waliitaka serikali yako ingalau iwaongezee mshahara ingalau hata Shilingi 50,000 tu kwa kila mfanyakazi. Ulijitetea vizuri, ukaeleweka na wakasema watakuvumilia hadi mwakani sawasawa na ombi lako...
Aidha kumbuka jana tu pia ulikusanya walioitwa "wazee wa Dar". Wakaiomba serikali yako unayoingoza ifanye vitu vidogo kadhaa vinavyohitaji fedha...
"Malkia wa maneno matamu" ukajitetea vizuri sana kwa maneno yako matamu kwelikweli huku ukisingizia hali mbaya ya uchumi wa nchi kama sababu...
Ukawaomba wakupe muda ili ujipange na kuona hali itakuwaje. Wazee wale kwa nilivyowatazama nyuso zao, ni kama walikuelewa na wakakupa " benefit of doubt..."
Lakini leo katika hali ya kushangaza unaamua kumzawadia fedha za wazee na wafanyakazi hawahawa wa nchi hii Mzee Ally H. Mwinyi uliyoiita "zawadi ya birthday" gari aina ya Mercedes Benz yenye thamani ya kiasi cha fedha za kitanzania kati ya 900,000,000 hadi 6,900,000,000 (bilioni 6.9)....!!
Are you really serious Madam President..?
Labda Madam President wewe na watu wako mnadhani Watanzania ni wajinga sana, hawajui gharama za magari hayo kama ni mapya. Ngoja tukueleze...
Binafsi niliposikia tu unachotaka kufanya kwa Mwinyi, haraka haraka nimetembelea soko la aina hii ya magari mapya mtandaoni, nimeshangaa kwa sababu bei yake ni kubwa sana..
Mercedes Benzi ya bei ndogo kabisa kwa kuzingatia muundo na toleo ni USD 400,000 sawa na Tshs. 920,000,000...!!
Ya bei ya juu kabisa ni USD 3,000,000 sawa na Tshs 6, 900,000,000 (bilioni 6.9..!!!)
Hapa chini ni baadhi ya picha ya magari haya..
View attachment 1779132View attachment 1779134
Hivi unadhani kuna sababu gani ya Watanzania kuendelea kuamini kuwa wewe mama kama kiongozi wa nchi hii unakwenda kufanya tofauti na aliyekutangulia nawe kwa bahati tu umejikuta ni Rais wa nchi hii...?
It's a wrong decision at a wrong time...
Achana na hii kitu. Hizo fedha unazoziona hapo siyo zako. Ni fedha za Watanzania zaidi ya 60,000,000. Tafadhali usuanze kupagawa mapema hivi, utaharibikiwa. Tumia busara na hekima kuzitumia fedha hizo ili kila Mtanzania aone impact yake..
Unapata wapi ujasiri wa kumzawadia mtu mmoja Tshs. 900,000,000 (huku tayari akiwa fedha zake nyingi tu) kati kati ya kundi kubwa la wananchi unaowaongoza ambao zaidi 30% wanaishi katikati ya umasikini uliotopea...??
View attachment 1779225
View attachment 1779135
View attachment 1779136
View attachment 1779137
View attachment 1779223