Sokomoko la zawadi ya gari ya Rais mstaafu Mwinyi

Sokomoko la zawadi ya gari ya Rais mstaafu Mwinyi

Mimi furaha yangu ningeona mechi ya mtani hata mambo ya BENZ nisingehoji,si unajua (sisi) wananchi wa kawaida tunaridhika kwa vitu vidogo vidogo.

Kazingua kwenye mechi ya mtani ili wapeane MABENZ. Pesa yangu ya kiingilio sijui itarudi vipi, wametoa tamko tu TFF, serikali ipo wapi?
 
Kuna ile BMW aliyokuwa anatumia Magufuli tena siku alipoenda kumuona kikwete akiwa kafiwa na Kakake ni bei gani vile
 
Kwl tumekosewa sana tu..hiyo pesa bora wangejenga sanamu ya makufuri wetu pale chato tungewaelewa...mkurugenzi unanunua gari mirioni mia tano ihiiiiiiiiiiii...porisi embu njooni kabura sijaharibu pereka ndani...hii pesa utaitapika Rc wa hapa uko wapi? Hebu erezea nirikutuma kushangaa wanawake au kazi? Na wewe nimekutumbuaaaaaa.....ndugu zangu ni razima tuereze ukwl au nasema uongo ndg zangu?....Pumzika Mwamba.
 
kiongozi mstaafu kama Mwinyi mwenye privileges na marupurupu kibao na mwenye familia nzuri yenye watoto wenye nyadhifa kubwakubwa na uwezo Mkubwa wa kiuchumi ktk jamii, anashindwaje kujinunulia yeye mwenyewe gari atakalo kwa mahitaji yake kwa gharama zake toka ktk fedha nyingi anazolipwa na serikali wakati wote...?
Rais mstaafu hutunzwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za nchi.
 
Kwa hiyo na wewe ulitaka Mzee Ruksa apewe IST?
Mtu mmoja alipata kusema "maskini wana roho mbaya sana!!"
Unadhani kuwa nina mawazo ya kimasikini siyo? Huwezi kutumia mali ya mtu mwingine kutamba nayo huku ukijitapa kuwa wewe ni tajiri kumbe ni mwizi na masikini wa akili tu...!!

Nisingeweza kusema Samia Suluhu ampe zawadi gani baba yake kwa sababu hayo ni mambo yake binafsi...

Inashitusha kusikia kuwa "serikali inamzawadia Mzee Mwinyi zawadi ya Birthday" Gari aina ya Mercedes Benz kwa gharama ya kodi zetu. Ingekuwa Madam Samia toka kwenye pochi yake ndiye anampa, kusingekuwa na mjadala...!!

Kama ni "serikali" inampa, straight hizo ni fedha zetu walipa Kodi...

Hii siyo sahihi hata kama iñgekuwa RAV4 ya mwaka 1998...

Huyu mzee tayari tunamgharamia kwa kumpa privileges & marupurupu kibao tu kama kodi zetu...

It's very unfair kuchukua kiasi kikubwa cha fedha kama hiki kumpa mtu yuleyule wakati kuna wananchi mahali wanahitaji 50,000,000 tu wapate zahaanati ya kijiji na kuokoa maisha ya maelfu ya watoto na kinamama...

This is selfishness of the highest order...
 
Sio kwamba mama anahofu ya kutoungwa mkono na baadhi ya watu so anachofanya nikujaribu kuwavuta upande wake?

Ebu tuendelee kufikiri kwanini Serikali itoe zawadi yenye thamani kubwa namna iyo
 
Back
Top Bottom