Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Kwa hakika Tanzania na watanzania tuna kila sababu ya kujivunia uimara ,weledi ,uzalendo ,utayari, ushupavu, umadhubuti,umakini na uhodari wa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama. Msione watu wanalala kwa usalama huku milango wakiwa wameweka tu misumari kama komeo na kuamka wakiwa salama wao na mali zao.
Uhodari na umakini wa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama ndio unatufanya watanzania tuamke salama sisi na mali zetu, kusafiri usiku kucha kupita milima na mabonde, tambarare na kona zote bila shida wala wasiwasi ya aina yoyote ile ya kutekwa. Watu kukesha bar wakiuza na kunywa pombe na wengine wakiangalia mipira mpaka usiku sana ,huku wengine wakikesha katika nyumba za ibada huku milango ikiwa wazi au imerudishiwa tu kuzuia baridi isiingie ndani.
Tuna tembea muda wowote tutakao kwa sababu tuna askari shupavu ,tuna majeshi imara na viongozi hodari na makini wanaongoza vyombo hivi chini ya Uongozi na maelekezo ya Mama yetu na Rais wetu mpendwa Daktari Samia Suluhu Hasssan.
Kumbukeni tunapokuwa tumelala sisi majumbani mwetu ,vyombo vyetu vinakuwa macho na vikitembea na kufanya doria usiku kucha ,huku vikipambana na kukabiliana na vitisho vyote kwa usalama wetu. Tupo salama kwa sababu ya jasho,machozi na Damu ya askari wetu waliojitolea kutulinda watanzania.
Kumbukeni kuna askari wetu inafikia wakati wanapata ulemavu wa kudumu na wengine wanafia kazini katika mapambano ya kulinda Taifa letu dhidi ya wahalifu na majambazi. Lakini wanaobakia wanaendelea na kazi ya kutulinda kwa moyo wote bila kukata tamaa wala kukatishwa tamaa japo wamepoteza wenzao katika mapambano.
Watanzania tuna kila sababu ya kuvipongeza,kuvitia moyo ,kuviunga mkono na kuvipatia ushirikiano mkubwa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kwa kutoa taarifa za muhimu kila iwezekanavyo kwa maslahi mapana ya usalama wa Taifa letu. Natambua changamoto huwa hazikosekani katika suala zima la kulinda Raia na mali zao. kwa sababu unakuwa unapambana na watu wenye akili na ujuzi wa kila aina na wenye kila aina ya utaalamu wanaoutumia katika kufanya uhalifu.
Watanzania tuwe na imani kuwa matukio yaliyotokea hapa Nchini ya watu kutoweka na kutopatikana mpaka sasa , yanaendelea kushughulikiwa vyema na kwa ushirikiano mkubwa sana wa idara zetu zote za ulinzi na usalama,.kuhakikisha kuwa wote waliopotea wanapatikana wakiwa hai na salama , lakini pia kukomesha Vitendo vyote vya kihalifu vinavyotokea na kufanyika Nchini.
Watanzania tuendelee kulinda amani yetu na kamwe na katu tusikubali kuharibu amani ya Nchi yetu ambayo ndio msingi wa maendeleo ya Taifa letu.pasipo amani na utulivu hakuna habari za biashara,wala michezo,wala siasa majukwaani,wala kusoma kwa amani kwa wanafunzi wetu,wala kujishughulisha vizuri kwa shughuli za kiuchumi,kijamii n.k
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.