Mimi kama muhaya, nshomile kutoka Uhayani Republic, imenibidi niingie chimbo kuleta maelezo kamili juu ya hii vita ya Israel na palestina ambayo kuna watu wanadhani Gaza inapigwa kwa bahati mbaya. Ukisoma maandiko ya agano la Kale (Old Testament) katika biblia na vitabu vya kiyahudi Torah na Tanakh. Utagundua kuwa Gaza ilitakiwa kubondwa tangu enzi na enzi kwa mujibu wa maandiko. Vita vya Israel na Palestina, vinaanza tangu enzi za zama za Wafilisti na Wana wa Israel, na chanzo kikuu cha vita ya waisraeli na wafilisti kugombana ilikuwa ni kwa sababu ya Ardhi, Rasilimali, na Ngome, na vita hivyo havikuwa na chanzo maalumu bali kugombania Ardhi na rasilimali. Vita vya hawa jamaa vimeorodheshwa kama ifuatavyo;
1. Vita ya Israel na Wafilisti ikiongozwa na Eli na watoto wake.
Ukisoma 1 Samwel 4:1-3, utaona namna vita vilipigwa baina ya wafilisti na waisraeli.
English
Kiswahili
UFAFANUZI: Miaka hiyo Eli na wanawawe, waliingia vitani na wafilisti, vita vikapigwa kweli kweli. Waisraeli wakiongozwa na Eli na wanawawe wawili wakashindwa vita. Watoto wakiume wa Eli ambao walikuwa mashujaa wakauwawa na wafilisti, Sababu za kushindwa kwa Eli ni kutokuwa na Imani thabiti. Vita vikaendelea kwa miaka mingi, waisraeli wakiendelea kuchezea kichapo. Mpaka ufalme wa Sauli.
2. MFALME SAULI, MWANAE JONATHAN na WAFILISTI
Baada ya muda mrefu, utawala wa Mfalme Sauli ukaingia. Vita bado vikaendelea kupigwa balabala baina ya waisraeli na Wafilisti; katika kitabu cha 1 Samwel mlango wa 14-15 tunaona.
1 Samwel 14:47-52
UFAFANUZI: Sauli na mwanaye wa kiume Jonathan waliendelea kupigana vita dhidi ya wafilisti. Na wakawa wanashinda kwa sababu walikuwa wanamtumikia Mungu. Vita viliendelea mpaka badae akaibuka Goliath.
3. DAUDI, GOLIATH na WAFILISTI
Katika kitabu cha 1 Samwel 17:1-53 Daudi ambaye alikuwa mchungaji wa mifugo anaonekana kwenda vitani kuwasalimia kaka zake, ndipo akamuoka Goliath ambaye ni mfilisti akiwadhiaki ndugu zake katika uwanja huo wa vita.
UFAFANUZI: Vita iliisha kwa daudi kuwa mshindi, na badae baada ya kifo cha mfalme Sauli, kwa mujibu wa unabii wa Samwel ilitakiwa Daudi ndio arithi ufalme huo kutokana na watoto wa Sauli wote kuuwawa vitani na wafilisti. David anafanikiwa kuwa mfalme ya Yuda, na badae biblia inaeleza David alikuwa nguli wa Vita, katika enzi za ufalme wake alizikunguta falme za Wafilisti vibaya mno na kufanikiwa kuteka maeneo yote ya Israel na kuziunganisha tawala zote kuwa chini yake, na Yerusalemu ndio ukawa mji mkuu. Tokea hapo wafilisti wakawa wanakula kichapo tu. Baada ya kifo cha Mfalme Daudi, mwanawe Sulemani alimrithi kwenye kiti cha enzi. Sulemani akawa mfalme wa tatu wa Israeli na akatawala kwa muda mrefu. Anajulikana kwa hekima yake, utajiri, na kwa kujenga Hekalu la Kwanza huko Yerusalemu. Utawala wa Sulemani mara nyingi huonekana kama kipindi cha ufanisi mkubwa katika historia ya Israeli.
4. UNABII WA AMOS dhidi ya GAZA na NCHI JIRANI.
Angalia maandiko ya Biblia hapo chini namna Nabii Amos anavyoishutumu Gaza kwa udhalimu wake na kuitabiria kuwa Gaza na Jirani yeyote atakaye endelea na ujinga ujinga basi atapokea kichapo kikali.
Ukisoma kitabu cha Amosi 1:6-8 (Amos 1:6-8)
English
View attachment 2786092
Kiswahili
UFAFANUZI: Amosi analaani mji wa Gaza kwa vitendo vyake vya zamani, hususani kwa kuteka jamii nzima na kuziuza kwa Edomu. Unabii huo unatabiri adhabu ya Mungu kwa namna ya adhabu ya moto (sijui ndio haya mabomu) juu ya kuta na ngome za jiji hilo kama adhabu matendo yao. Hii ni sehemu ya mfululizo wa unabii katika Amosi 1 unaozungumzia mataifa mbalimbali jirani, ukigusia udhalimu na vitendo vyao viovu na kadhia watakayokumbana nayo kutokana na mipango yao dhidi ya Israel. Ndio maana mwaka 1948 Israel ilizikunguta nchi zote za kiarabu zilizoungana kumshambulia hapa nazungumzia Misri, Lebanon, Syria, na zote zilizoshiriki katika vita hile ya mwaka 1948 inayoitwa Israel-Arab war. Unabii bado unaendelea.
5. MFALME HEZEKIA kuwatandika wafilisti na kuchukua eneo la GAZA
Vile vile ukisoma tena kitabu cha; 2 Wafalme 18:8 (2 Kings 18:8)
English
Kiswahili
UFAFANUZI: Mstari huu ni sehemu ya simulizi la kihistoria la Mfalme Hezekia wa utawala wa Yuda na kampeni zake za kijeshi. Inataja kutekwa kwa eneo la Wafilisti, na eneo la mji wa Gaza, na Mfalme Hezekia. Muktadha mpana wa tukio hili ni kwamba Mfalme Hezekia wa Yuda alitafuta kuimarisha na kulinda ufalme wake. Gaza ulikuwa mji katika eneo la Wafilisti, ambao walikuwa adui wa muda mrefu wa Waisraeli na Wayuda. Kampeni ya kijeshi ya Mfalme Hezekia katika eneo hilo, ambayo ilijumuisha Gaza, inaweza kuwa sehemu ya juhudi pana za kulinda mipaka ya ufalme wake na kudhibiti udhibiti wa eneo hilo. Sababu maalum au vitendo vilivyosababisha kampeni hii hazijaelezewa kwa kina katika maandishi ya kibiblia.
6. SAMSON na GAZA
Vilevile tunaona kwenye kitabu cha waamuzi wafilisti wa mji wa Gaza wakipokea kichapo kutoka kwa Samson, baada ya kupata mwanamke katika mji huo.
Waamuzi 16:1-4 (Judges 16:1-4)
English
Kiswahili
UFAFANUZI: Mstari huu ni sehemu ya hadithi ya Samsoni, mmoja wa Waamuzi wa Israeli, na inasimulia ziara yake katika jiji la Gaza. Waamuzi 16, inatajwa kwamba Samsoni alienda Gaza, na huko akamwona kahaba. Akiwa Gaza, alijihusisha na matukio mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kubeba milango ya jiji hadi juu ya kilima. Matendo yake huko Gaza ni sehemu ya simulizi kubwa zaidi la maisha ya Samsoni na kukutana kwake na Wafilisti, ambao walikuwa maadui wa Waisraeli wakati huo. Safari ya mwisho ya Samsoni lilifanyika huko Gaza. Alifia huko Gaza, karibu na mahali alipokuwa ametekwa na Wafilisti. Kifo cha Samsoni kinafafanuliwa katika Waamuzi 16:21-30, ambapo aliangusha hekalu la mungu wa Wafilisti Dagoni, akiwaua Wafilisti wengi, akiwemo na yeye mwenyewe, katika mchakato huo.
HITIMISHO: Mji wa kale wa Gaza ulikuwa katika eneo linalolingana na sehemu ya Gaza ya hivi leo. Kwa maelfu ya miaka, jiji na mazingira yake yamekumbwa na mabadiliko na maendeleo mengi, lakini marejeo ya kibiblia ya Gaza kwa ujumla yanarejelea mji wa kihistoria na eneo pana zaidi la mji huo mkongwe. Gaza ya leo iko katika eneo la linalosemekana ndio lililokuwa jiji la kale la Gaza, na miunganisho ya kihistoria na maandiko ya Biblia inasalia katika muktadha huo wa kijiografia kuwa Gaza ya leo ndio Gaza ya Kale.
Wafilisti wa nyakati za kale si sawa na Wapalestina wa leo. Neno "Wafilisti" linarejelea watu wa kale walioishi katika eneo la Kanaani, ambalo liko karibu na eneo la Israeli ya kisasa na maeneo ya Palestina, na vile vile sehemu za Gaza ya leo, maeneo haya waliishi wafilisti. Walitajwa katika Biblia ya Kiebrania na walijulikana kwa migogoro yao ya muda mrefu na Waisraeli wa kale.
Wapalestina wa kisasa ni wakazi wenye asilimia ya Kiarabu wanaoishi katika eneo hilo linalojumuisha Ukingo wa Magharibi (West Bank), Ukanda wa Gaza (Gaza strip), na sehemu za Israeli. Neno "Wapalestina" kimsingi linamaanisha wakazi wa Kiarabu wa maeneo haya. Ingawa majina yanafanana kwa kiasi fulani kutokana na eneo la kijiografia, mazingira ya kihistoria na kiutamaduni ya Wafilisti na Wapalestina wa kisasa ni tofauti. Wafilisti walikoma kuwepo kama watu wanaotambulika zamani, jamii yao ilipotea, wakati Wapalestina wa kisasa ni watu tofauti wenye historia na utambulisho wao wa kiarabu.