Soma ujifunze: Jinsi kijiwe changu kilivyosababisha mtu akalizwa 2M na tapeli leo

Soma ujifunze: Jinsi kijiwe changu kilivyosababisha mtu akalizwa 2M na tapeli leo

Boda boda pengine kapata kwa mkopo au kujibana mpaka kakonda..leo anaibiwa mchana kweupe..akitoka hapo usishangae na yeye anakuwa katili ... ..maana machungu yake..
Bora watu kama akina Mshana Jr wamsaidie aisee
 
Mh hawa watu ni hatari.

Nilikua nashinda kijiwe kimoja hivi cha kuuza maua. Siku hiyo akaja jamaa akauliza bei ya maua akatajiwa akasema atakuja kesho yake, alitaka maua ya zaidi ya laki 2.

Kesho akaja huku akiwa amekodi kirikuu kabisa, basi akatoa 20 kama tip ya vijana kumbebea maua. Tumemaliza akasema inabidi twende naye kwake ili tumshushie, tukakubali. Pesa ya maua akasema anaenda kuitoa benki Mlimani City.

Njiani akamwambia dereva wa kirikuu ampe laki 4 akamtumie mkewe akifik Mlimani akishatoa pesa atamrudishia. Dereva akajibu ana laki 2 tu, mshua wa maua akajibu ana laki jamaa akasema agewe tu hiyo hiyo.

Akaomba simu ya mshua wa maua ili atumie kuandika namba pembeni, mshua akatoa. Simu ilikua Hauwei Y6 Pro (at that time ilikua ni bonge la simu). Alivyogewa akashuka akaingia money shop akarudi tukaendelea na safari. Simu hajarudisha hapo

Kisha ikaja mada ya video ya mfanyakazi akimkanyaga mtoto na abuse kibao, mada ilivyopamba moto dereva kirikuu akasema halafu ninayo kwenye simu, mnunua maua akasema hebu nione. Akagewa simu akaangalia kisha akabaki nayo pia. Hii ilikua Tecno sikumbuki aina gani.

Tulivyofika Mlimani jamaa akashuka, akaingia ndani mule watu tukawa nje tunamsubiri. Baada ya muda kupita mshua wa maua akasema ebwana tuingie ndani tumshtue kua muda unaenda, jamaa alisema anaingia CRDB. Wakaingia, baada ya muda wanatoka wanasema mshkaji hayupo.

Kwa jinsi alivyo nadhifu na mchangamfu kumuwazia utapeli haikua rahisi, mshua wa maua akasema pigeni namba yangu, tunapiga simu haipatikani tukajaribu na ya dereva kirikuu ikawa haipatikani.

Jibu tukawa tushapata. Mshua wa maua anataka kumpiga dereva kirikuu akisema kashirikiana na yule bwana. Mwisho kila mtu akaamini kua ndiyo kashalizwa. Dereva kirikuu akasema hapa hapandi mtu gari langu maua yenu nayatupa. Katika ile 20 tukampa 5 ndiyo akakubali kuturudisha kijiweni.
Hahaha
Bonge la Picha
 
Back
Top Bottom