Soma ujifunze: Jinsi kijiwe changu kilivyosababisha mtu akalizwa 2M na tapeli leo

Wakuu habarini za Mda Huu, Nina Kisa kimoja leo kama mnavyojua baada ya kumaliza Chuo Basi tunavyosubiri milioni Basi tunatafuta Buku.

Jana majira ya saa 4 Asubuhi nikiwa katika kijiwe changu cha kuchimba mchanga mgumu alitokea mteja mmoja aliyekua kavalia nadhifu sana akiwa ameshuka bodaboda kama abiria, kutokana na njaa niliyonayo ilibidi nimfate haraka nikijua labda Ni boss anaejenga apartment hapa mjini Basi amekuja kuchukua mchanga angalau trip 10.

Nikweli niliongeanae akasema anataka mchanga trip 4, na Bahati Nzuri kulikua na gari kubwa inamaliza kubeba mchanga trip ya mwisho Basi wakakubaliana na dereva ambebee mchanga wake Huku Mimi nikiongezewa dau toka 60000-70000 kwa trip.

Vijana walianza kupakia mchanga kwa kasi sana, Huku boss akiwa pembeni Kuna bucha akiagiza Nyama kg1 na baada ya hapo alimuomba pikipiki yule boda aliyekuja nae( ambae walionekana kuchangamkiana) Ili boss apeleke mboga nyumbani fasta sana Huku akidai atest isije ikawa kasahau kuendeshea.

Vijana wa kazi walimaliza kazi Huku tukimsubiri boss apande mbele Ili Twende location turudi kupakia tena, tulisubiri kwa Nusu saa Hakuna mtu, tukasema labda anasubr iive ale lakini mbaka sa 6 Hakuna mtu, tukamuuliza dereva boda kwani ulimtoa wapi huyo mtu, akadai walijuana Jana yake na alimtembeza Jana yake kutwa Huku akiwekewa mafuta ya 30,000.

Tulimuiliza unakujua kwake? Alijibu nilimpeleka sehem akanionyesha nyumba yake kwa mbali, tulimwambia aende lakini ALIPEWA JIBU kua hawamjui mtu huyo. Kijana alianza kuona mkojo unauma, kiungwana nilimuonesha choo.

ALISEMA amenunua pikipiki shilingi milioni 2 na Laki 3, wiki iliyopita, alionekana kuchanganyikiwa sana, Kuna mengi ya kujifunza. Kuhusu mchanga ilibidi tupeleke sehemu Yakwanza Huku bei ikishuka hadi 50,000.

Wanajf, usimuamini mtu KIZEMBE KIZEMBE. Bola Wali Nyama kuliko Walimwengu.
Karibuni kwa mchanga mgumu songea.

0738853634
Daaa!!! Hii kwa kweli niya mwaka. Lakini siku zote usikubali kumpa mtu chombo chako cha moto, hata kama ni ndugu yako. The best thing mwambie "twende nikupeleke"
 
Mwaka jana alipita jomba mmoja hapo ofisini kwangu mida ya jioni sana akidai yeye ana PC mupyaaa kaifanyia ma namna gani kaichomoa Bandarini ila sasa namna ya kuitoa getini imekuwa msala, walinzi wanataka mgao.

Kuna dogo mmoja aliwahi nijia kuniuliza kama nina pc au ninamfahamu jamaa anaeuza kwa bei nzuri nimuelekeze akanunue, dogo nikamkol akaja nikamueleza ilivyo akakubali. Sasa yule jomba sijui aliniona zuzu kiasi gani akanambia bro wewe niamini tu, nipe kwanza elfu 60 hiyo nyingine utanimalizia nikileta mzigo mi nikamjibu tu short n clear, sina pesa subiri nikuunganishe na mhitaji. Dogo nikawa nimeshampanga nikamwambia asimpe yule jamaa hata mia bila kuniconsult kwanza.

Kesho yake dogo akawasiliana na mchizi, akaambiwa njoo geti namba 5 utanikuta, dogo akalamba kibati mpaka getini akakutana na mchizi, jamaa akamchombeza ampe kwanza elfu 60 akawahonge walinzi atoke na mzigo, dogo akatoa, yule jamaa sijui aliingia geti gani akatokea geti gani, mimi nipo zangu ofisini, dogo ananipigia. Bro hivi fulani una namba yake nyingine? Nikamuuliza, vipi kwani akanijibu hapatikani na wala hamuoni, nikamuuliza umempa hela? Akanijibu ndio, nikamwambia basi ushaliwa we unatoaje pesa bila kukitia mkononi kitu, nilikwambia mapemaa nilikuwa na nia yangu ukaniona fala. Hiyo kumbuka ni saa 5 asubuh ananipigia kumbe kawekwa tangu saa 2 kasoro, alipoona imeisha ikambid arudi tu hostel kwake, mpaka leo hakuna cha pc wala nin
 
Mkuu hatari, Mkuu Ni fundi mzur wa PC?
 
Mh hawa watu ni hatari.

Nilikua nashinda kijiwe kimoja hivi cha kuuza maua. Siku hiyo akaja jamaa akauliza bei ya maua akatajiwa akasema atakuja kesho yake, alitaka maua ya zaidi ya laki 2.

Kesho akaja huku akiwa amekodi kirikuu kabisa, basi akatoa 20 kama tip ya vijana kumbebea maua. Tumemaliza akasema inabidi twende naye kwake ili tumshushie, tukakubali. Pesa ya maua akasema anaenda kuitoa benki Mlimani City.

Njiani akamwambia dereva wa kirikuu ampe laki 4 akamtumie mkewe akifik Mlimani akishatoa pesa atamrudishia. Dereva akajibu ana laki 2 tu, mshua wa maua akajibu ana laki jamaa akasema agewe tu hiyo hiyo.

Akaomba simu ya mshua wa maua ili atumie kuandika namba pembeni, mshua akatoa. Simu ilikua Hauwei Y6 Pro (at that time ilikua ni bonge la simu). Alivyogewa akashuka akaingia money shop akarudi tukaendelea na safari. Simu hajarudisha hapo

Kisha ikaja mada ya video ya mfanyakazi akimkanyaga mtoto na abuse kibao, mada ilivyopamba moto dereva kirikuu akasema halafu ninayo kwenye simu, mnunua maua akasema hebu nione. Akagewa simu akaangalia kisha akabaki nayo pia. Hii ilikua Tecno sikumbuki aina gani.

Tulivyofika Mlimani jamaa akashuka, akaingia ndani mule watu tukawa nje tunamsubiri. Baada ya muda kupita mshua wa maua akasema ebwana tuingie ndani tumshtue kua muda unaenda, jamaa alisema anaingia CRDB. Wakaingia, baada ya muda wanatoka wanasema mshkaji hayupo.

Kwa jinsi alivyo nadhifu na mchangamfu kumuwazia utapeli haikua rahisi, mshua wa maua akasema pigeni namba yangu, tunapiga simu haipatikani tukajaribu na ya dereva kirikuu ikawa haipatikani.

Jibu tukawa tushapata. Mshua wa maua anataka kumpiga dereva kirikuu akisema kashirikiana na yule bwana. Mwisho kila mtu akaamini kua ndiyo kashalizwa. Dereva kirikuu akasema hapa hapandi mtu gari langu maua yenu nayatupa. Katika ile 20 tukampa 5 ndiyo akakubali kuturudisha kijiweni.
Mshua wa maua[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
[emoji23][emoji23][emoji23]Nacheka Kama mazuri! Pole Sana!
 
Back
Top Bottom