Soma unaweza jifunza kitu: Jinsi graduate nilivyopoteza 1.8M niliyoitafuta kwa jasho

Pole mm pia iliwahi nitokea 5M ilipotea hivyo hivyo

Sent from my TECNO W4 using JamiiForums mobile app
Mkuu mbaya zaidi kwangu kueleza wenzangu ikawa shida, nikasema nani ataniamini nilikaa nalo moyoni Siku moja nikaamua kuwaeleza wenzangu na manager wangu.
Asee manager aaliwaka vibaya sana na kunitolea kauli ambazo sio nzuri.
Haya mambo kabla hajakukuta unaweza hisi MTU alifanya kusudi na nimejifunza staff wenzio mnacheka nao vizuri ila Siku yakukute ni wewe na Mungu wako.
 
Pole Sana mwanangu yote hayo ni ktk pilika pilika za kijikwamua magraduate mi nakumbuka nshatoaga 1m kwenye biashara iliyokua inantia hasara nikafanya maamuzi ya pupa ikapigwa yote na mshkaji wangu kabisa Yani machimboni huko...

Cha muhimu piga moyo konde na uamke kwa hasira zaidi ya ulizokua nazo kizitafuta
 
Mie niliibiwa kwenye daladala 6.4 M mwezi uliopita tena ya Ofisi,nikitembea nahisi moyo unachomoka nikikaa nahisi hivyo hivyo ni mateso ambayo sijawi kuyapitia toka kuzaliwa kwangu.
Pole sana mkuu ila next time tujitahidi kupunguza risks 6M unapanda daladala? Si bora hata uchukue bajaji ama Uber tusilaumu sana ilikua siku yako tu yakufundishwa na ulimwengu. Pole
 
Kwenye harakati za utafutaji kupoteza ni sehemu ya maisha.

Jambo la msingi ni kupambana kupunguza risk za kupoteza.

Mimi nilifanya kazi za usiku, nikakusanya zaidi ya 1M nikaenda kulima mihogo huku Kibiti. Haikurudi hata 100.

So, ni kawaida tu.
Nini kilitokea mkuu? Nguruwe walofanya ya nini?
 

Pole sanaa ndugu amini usiamini anaekuibaia anakuongezea utajiri, ngoja nikupe short yangu kidogo nipo kwa taasisi ya umma flani basi kuna kazi ikatokea ya kutengeneza madirisha ya ofisi ikatoka kama 2 mil kwaajili ya kazi hiyo. Sasa pale mtaani kuna mwana nilimzoea ana kijiwe chake ni fundi fundi mara nyingi alikuwa ananilalamikia kuhusu kazi basi nikaona nimuunganishe kama kawaida.

Ofisi yetu huwa ina tabia ya kukuamini mtumishi, unapewa hela yote kajingaike nayo nikamkumbuka jamaa nikamuunganisha jamaa akaomba hela robo tatu afuate material nikampa akafuata akarudi na material chache kazi ikaanza. Ebwanaee sujui alipatwa na nini jamaa kanikimbia bwanaee na madirisha sikupata msala ukawa wangu boss wangu haeliwi anataka pesa au madirisha mwaka sasa nimetoka kukopa kwa taasisi moja kwa riba chafu nimelipa madirisha yote jamaa mwaka hajaonekana na wala sijui yuko wapi ila process zote nilifuata mikataba na rb ninayo natembea nayo, Mungu si athumani ipo siku tutakutana kinachoniuma sio kuniibia bali kupotezewa credibility pale ofisini sipewi deal tena. Usikate tamaa hadi leo nalipa deni kwa hiyo taasisi. So usife moyo hatujakatwa mikono
 
Pole sana mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…