Soma unaweza jifunza kitu: Jinsi graduate nilivyopoteza 1.8M niliyoitafuta kwa jasho

Mie niliibiwa kwenye daladala 6.4 M mwezi uliopita tena ya Ofisi,nikitembea nahisi moyo unachomoka nikikaa nahisi hivyo hivyo ni mateso ambayo sijawi kuyapitia toka kuzaliwa kwangu.
Duuh pole mkuu
 
We jamaa tukio Hilo linakwambia wewe bado sio mjasiriamali so inakubidi ujifunze ujasiriamali, inabidii uwende kidogo kidogo kwa hiyo pesa ulitakiwa kabla hujakusanya kufikia yote hiyo ungekuwa unaizungusha kwenye biashara ndogo ndogo na kuachana na hivyo vibarua na kubakia na tution center kabla hujakusanya yote hiyo. Boda boda ungenunua kwa hela ya kutokujichosha.
 
Pole sana mkuu umepoteza pikipiki ila nguvu, akili na maarifa bado unayo so usife moyo ndugu
Shukran
Nimekuelewa, lkn unamaana nngeachana na shuguli zote zilizonipa hiyo ela then nibaki na moja?
 
Mie niliibiwa kwenye daladala 6.4 M mwezi uliopita tena ya Ofisi,nikitembea nahisi moyo unachomoka nikikaa nahisi hivyo hivyo ni mateso ambayo sijawi kuyapitia toka kuzaliwa kwangu.
Pole Sana Mungu akupe nguvu subira pia! Upate zingine zaidi ya hizo kwa njia nyepesi ambayo haukuitegemea! Kwa Mungu hakuna kubwa amini hivyo
 
Dunia nzuri Ila wanadamu wengi hawaaminiki, unajua saa yingine ukifikiria Ndungai alivyoSEMA vijana hawaaminiki tunakebehi Ila Ni ukweli kabisa, imagine mkasa Kama wa huyu bwana mdogo....Alie muamini kijana mwezake na kumpatia Akira ya boda, kilichotokea, vijana wengi wako hivyo.....hawana mitaji Ila wakisaidika tu watakuzunga na watakuacha njia panda
 
Pole sana mkuu najua inauma ila hakuna namna jipange kwa staili nyingine kikubwa uhai
 
Kumbe nilikuwa sahihu kumpokonya chombo yule jamaa, ila haya mambo ndiyo maana watu wanarogwa.
 
Haya ni mapito mkuu, muhimu uhai. Mwaka 2017 nilitapeliwa 10M Njombe, hapa nilidanganywa kwa ajili ya kilimo cha viazi lakini hela ikaliwa na sikupata chochote, na 2.2M na ndugu yangu wa karibu ambayo nilimtumia akanunulie shamba la miti lakini shamba sikupata mpaka muda huu naandika hapa.
Katika dunia ya sasa muamini Baba/Mama yako tu ndicho nilichofundishwa kupitia hii kadhia. Mungu ni mwema bado napambana mdogo mdogo na imebaki historia tu
 
Muamini Baba na Mama??? Kwenye pesa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…