Somali Bantus walikataliwa Somalia, UN waliomba warudishwe kwao Tanzania

Somali Bantus walikataliwa Somalia, UN waliomba warudishwe kwao Tanzania

Hii iwe fundisho kwa yale mitafuna mirungi inatoka bongo na kenya eti inaenda kwenye hiyo nchi kumpigania Mungu wao, wajue kuwa huko hakuna Mungu bali ni watu wa aguzi na wenye roho ngumu. Wabaki bongo waijenge nchi yao wasidanganywe wataenda kuteswa
 
Somalia kuna Wabantu ambao walifika huko wengi kwa Utumwa, maisha yao yalikuwa magumu kuanzia mwanzo Wasomali hawakuwahi kuwakubali na wamekataliwa kata kata na Msomali yoyote aliyejaribu ku-intermarry na Mbantu alitengwa na jamii ya Wasomali.

Hali ilikuwa mbaya kwa Wabantu Somalia hadi UN iliwaombea hifadhi Tanzania wakarudishwa Mkoani Tanga wengi tu wengine walipewa hifadhi USA.

Kwa mujibu wa UN hawa Wabantu wa Somalia walichukuliwa kama Watumwa karne ya 20 na walitokea jamii ya Wazigua, Wazaramo, Wayao, Wamakua pamoja na wengine, fikiria miaka yote hiyo lkn bado hawakubaliki nchini Somalia, …

Tuwakubali na kuwapa hifadhi, uraia. Hawa ni ndugu zetu.
 
Miska ya 1992 waliletwa Tanga kwa meli, waliwekewa mahema nje ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa mpaka utaratibu wa kuwapeleka Handeni ulipokamilika.

Huko Handeni ndiyo sehemu wanawekwa wenye migogoro ya ardhi, sasa hivi Wamasai wa Ngorongoro wanapelekwa huko.
Handeni ndio liberia ya bongo
 
Huu ni uongo wa wazi.Wasomali hawa wenye asili ya Nchi za Tanzania na Msumbiji walikwenda kutafuta makazi kama wahamiaji wengine.Waliondoka Somalia mwaka 1991 baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe ndani ya Somalia.
Wasomali hawa hawabaguliwi huko Somalia na wameoana na kuzaa na jamii walizozikuta.
Kuna wapemba walikimbilia Somalia 1992 baada ya vurugu za Zanzibar.Wapo wanaishi mpaka leo na wameoana na wenyeji wa huko .Kwanini hawa wapemba wasibaguliwe.
Wanyamwezi,wanyasa na wamakua waliohamia Zanzibar nao walikuwa watumwa?Au walihamia kutafuta makazi na riziki?Abeid Amani Karume alikuwa mtumwa?Kwani hakuwa na asili ya Zanzibar!
Jiulize kwanini wapemba walikimbilia Mogadishu Somalia na sio Mombasa Kenya?
 
Vurugu za 1992? [emoji15]
 
Maswali ya msingi kuulizana hapa ni haya yafuatayo:
1. Nani alikuwa anafanya biashara hiyo ya watumwa ?
2. Kwanini biashara ya utumwa isitawi kwenye jamii ambayo watu wake ni washika dini sana ?
 
Back
Top Bottom