Somo kutoka Urusi: Ili Taifa lipate mafanikio lazima kuwe na "consistency" kwa viongozi wa wandamizi na nguli

Acheni kukaririshwa mambo ya ajabu. Hiyo mifumo nani anaii oparate.
Brother soma historia hakuna Taifa limewahi kuinuka bila kuwa na kiongoza au viongozi shupavu. Hao US, Britain sijui German na wengine. Wapo hapo kwa sababu wapo viongozi shupavu waliwahi kuwapata, wakafanya makubwa. Endeleeni lidanganyana eti mifumo.
Hao wenye mifumo mbona wanacharuana kila mwaka. Si waache hiyo mifumo iwaongoze.
 
Tunae kapitain joji mkuchika nguli wa mifumo ya kimkakati ya taifa..
Nakubaliana na wewe. Tunatakiwa angalau kwa miaka 10 hadi 15 tunakuwa na watu wa aina yake ndani ya Serikali na katika level hizo
 
Umeandika unazi na umekurupuka.
 
Mkuu habari za kweli unadhani utazipata wapi? Zile za west unasemaq zinapropaganda,hata za upande wa pili hazikosi propaganda pia,na hiyo ni moja ya principle za vita,hutakiwi kuripoti ukweli unaoendelea kwenye uwanja wa mapambano,warusi wamechinjwa sana Ukraine lakini wao hawezi wakakutangazia wamevipa maagizo vyombo vyao vya habari nini cha kuandika,shusheni jazba ukweli mtaujua baadae.
 
Mpaka hapo tumeiahaendelea maendeleo gani unataka? Kilaq kaya Ina choo chake,waqtu wanamwamko wa kuwapeleka watoto shule,ufaulu umeongezeka mashuleni,sasa wewe unataka nini? au unataka turushe rocket yenye satellite kwenda anga za juu ndo uamini kwamba sisi watanzania tumeendelea?
 
Urusi ndio nchi yenye mafanikio zaidi duniani? GDP yake ni ngapi? GDP per capita ni ngapi? HDI yake ipoje? wnanchi wake wana furaha kiasi gani?
acha upumbavu, mkitaka kuongozwa n madikteta nendeni Burundi au Uganda hapo
NANI ALIYEKWAMBIA KUWA NA GDP KUBWA NDIO MAFANIKIO?,HATA DADA SAMIA ATAKUFA ATAKUACHA MJINGA,
 
EeeenHeee Heeee!

Na wewe umetokea sayari gani, au makazi yako ni pangoni pasipofikiwa na mwanga wala sauti?

Hata uandishi wenyewe ni wa shida, takwimu unazoweka kama ushahidi ni takataka!

Kwa hiyo kiwango cha elimu yako ndiyo tukichukue kama kielelezo cha maendeleo ya nchi yako uliyonayo kichwani mwako?
 
KAbla ya hi vita uliwahi kujua sarafu ya Urusi inaitwaje? Anyway, kila mtu na fikra zake; i think nchi kama India sasa hivi zinatajirika sana kupitia hu mgogoro, mafuta ya Urusi mengi yanauzwa India kwa bei rahisi halafu India ana process then tunakuja kuuziwa sisi; hebu pia prot graph ya thamani ya pesa ya Urusi ilivyokua kabla ya vita na wakati hu wa vita; mkuu, vita ni biashara. For your information, USA anapenda hi vita iendelee ili baadae aje afanye biashara kubwa sana na Ukraine, zile silaha na pesa hatoi bure, hakunaga kitu cha namna hiyo kwenye hi sayari inayoitwa DUNIA
 
Kambarage alijaribu huo ungangari matokeo yake Nchi ilidondokea kwenye umaskini wa kutumia majani kufulia nguo [emoji1] huo ubabe unaousifia miaka mi2 ijayo utaona kitakachotokea URUSI ktk uchumi na Utawala.
Dunia ya leo ubabe Aina ya urusi au Korea kaskazini haulipi Tena.
 
Sio lazima Hawa manguli wawe ni marais. Hujaipata concept yake. Kuhusu rais Samia kupewa muda mrefu wa kutawala naikataa
Mlitamani kayafa apewe muda wa kutawala bila kikomo na mpumbavu mmoja kiongozi wa mhili ulionajisiwa akaapa eti apende asipende atalazimishwa !!
Leo woteee makanyanga mmoja kalala mazima mwingine hajulikani kalala au kasimama
Mungu kaamua ugomvi.
 
Labda useme wewe. Halafu nina hofu hata hujanielewa pamoja na ujuaji wako. And you can't drag me into what you want to.
Jadili nilichoandika acha ujuaji. Sawa.
Jibu swali....
 
Russia hakuna uzalendo wowote Russia inatawaliwa na kikundi kidogo cha mafisadi wakiongozwa na Putin.Hawataki kuachia madaraka wanajua wakiondoka tu Takukuru ya Urusi inao

Hao wote uliwataja mali zao za mabilioni na pesa mabilioni zimekuwa frozen nchi za Magharibi

Vikwazo wamewekewa wao na familia zao
Ile vita sio Kuwa anapigana na Ukraine la.Yeye kavamia Ukraine kisa aliota kuwa kuna siku Ukraine watakuja mvamia.Hivi mtu unaota tu halafu unaenda fanya uharibifu kama ule Ukraine kweli? Mtu hajakuvamia .Ukraine jeshi ni la wananchi wanapigania nchi yao na wana support ya wananchi wakati Urusi Jeshi linampigania Putin abaki madarakani halina support ya wananchi.Wanampigania mtu mmoja na kikundi cha mafisadi wenzie ma Oligarchs


Alichofanya Urusi kinatakiwa kulaaniwa na kila binadamu mwenye akili timamu si cha kufanya kwenye dunia ya kistaarabu ya sasa
 
Bora madikteta wa live live kabisa kuliko hawa viongozi tunaosema ni wa demokrasia kumbe ni vibaraka tu wa wamagharibi
 
Kukua kwa thamani ya fedha siyo kiashiria pekee cha uchumi kukua,nchi nyingi bado zinauziwa mafuta na Urusi kama vile India uliyoitolea mfano,lakini zipo kwenye mchakato wa kidumu wa kuachana na mafuta na gesi ya Urusi,unajua Urusi walipoivamia nchi ya Georgia hawakuwekewa vikwazo vya uchumi na nchi yoyote,so wakajisahau wakadhani kuivamia Ukraine itakuwa ni jambo rahisi la wiki mbili hivi basi,wauondoe madarakani utawala wA Zelensky na kuacha mtu wanayemtaka wao akiendelea kutawala,lakini wamekutana na hali tofauti,walipojaribu kuiteka Kiev walipata upinzani mkali ambao iliwapelekea kuyarudisha majeshi yao nyuma na kuendelea vita kwenye mikoa yenye bandari,huku vikwazo vya uchumi vikiwakalia kooni,sasa hivi huko kwao Hali si shwari,kama una nugu huko anaweza kukusimulia,manaake vyombo vya habari mmevikataa mnasema vinatangaza propaganda za magharibi.
 
Nadhani tuna source tofauti tofauti sana za inform; ninacho kijua mimi ni kwamba hata USA na baraza lao wanajiuliza kwanini jamaa haichukui Kiev? Kwanini pia hapigi reli, vyanzo vya umeme? Kaviacha tu why? Kwanini hapigi hata jengo la bunge ilihali halina ulinzi kiviile? Why? hayo ni maswali ambayo Ulaya na USA wanajiuliza. Umesema Urusi hakujua kama angepambana na vikwazo? Kaka, kabla hawajarusha bomu hukuziona ziara za Putin kwa rafiki zake China, Cuba na kule Venezuela? Unadhani kwanini wakati anaivamia Georgia kama unavyo sema hakufanya hivyo? Mkuu, CIA, M16, KGB wamekua wanapelelezana miaka na miaka, sio leo, wanajuana siri zao nyingi sana; hata hili la vikwazo walijua hao KGB and this is why Putin alisema mapema kabla hajaanza vita kwamba yeyote atakae rusha risasi kwenda kwake atakipata; hizo statement zilitoka kabla; baada sasa ya kuanza vita, rais wa USA alitamka hadharani kwamba USA na NATO hawata peleka majeshi kule, kwa kufanya hivyo ni kukaribisha vita ya dunia. Statement hizo hazikutoka tu ghafla, wale ni wazungu mkuu, wanapigana wenyewe kwa wenyewe, wana akili, wanafanya utafiti sana kabla ya kushambuliana. Usinambie kwamba kitendo cha Putin kutaka kuuza gesi na mafuta yake kwa pesa ya Urusi kilitokea tu ghafla, they knew it even before. Hushangai hata mataifa ya Kiarabu ambayo ni marafiki wakubwa wa USA ni kama wapo upande wa Urusi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…