Somo kwa wastaafu: Pesa za pensheni siyo za kufanyia biashara kama unataka kuishi Maisha marefu

Somo kwa wastaafu: Pesa za pensheni siyo za kufanyia biashara kama unataka kuishi Maisha marefu

bongo dili

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2015
Posts
12,350
Reaction score
25,180
Watu hawana huruma na wastaafu, huwapa michongo ya pesa wanaishia kufa kwa pressure. Ukistaafu idea nyingi sana unaletewa na ndugu.

Pana mstaafu alipata milion 250. Shemeji yake akamwambia tufate pikipiki China ukileta kwa jumla pesa ipo, akampa pesa shemeji yake akalala nazo kona China, hadi wa leo hata kama alirudi nchini kimya kimya siri yake.

Pana mstaafu aliambiwa trekta zinalipa akapigiwa hesabu na motivator akaingia dukani akachukua trekta mbili mpya kwa milion 90 leo zipo juu ya mawe zinaliwa na kitu, amekosa pesa za kununua spea.

Mwingine aliambiwa daladala zinalipa akazinunua akaishia kushinda stand anahesabu tripu Kila ikipita. Ukistaafu achana na biashara, nunua bond au weka fixed nje ya nchi mfano Canada, USA au zile stable country ule gawio kila baada ya muda, umeshindwa sana jenga chumba sebule chumba sebule gombana na wapangaji maisha yasonge.

Kisha tafuta shamba mikoani acha familia mjini weka kasikilize sauti za ndege tu porini unalima kilimo kisicho cha biashara ili kufanya mazoezi tu utafika miaka 100, pia kaa mbali kabisa na hawa mitume na manabii watakufilisi.

Pana mama yupo kitandani mwaka sasa anaumwa, aliambiwa biashara fulani inalipa alikuwa na nyumba zake 4 alijinyima akiwa kazini kujenga, akaingia bank akazikopea milion 200 baada ya muda biashara ikawa hasara bank wanataka hela zao.

Bora upoteze pesa ujanani una nguvu kuliko kupoteza uzeeni, zikienda zimeenda.
 
Huyo alienunua trekta alifanya maamuzi sahihi.
Inawezekana alikosea tu location, nunua tela jembe na mashine ya kupukucha unafanyanya kazi misimu yote kiangazi unabeba hata matofali, msimu wa mvua unalima msimu wa kuvuna unapukucha.

Matunzo ya trekta na spea zake ni bei za kawaida sana, usiseme spea zimemshinda kamuulize ni changamoto gani imemfanya azi paki.

Ni vizuri hiyo biashara angeianza kabla ya kustaafu ili ajue changamoto zake mapema wala asingepaki.
 
'.....akapigiwa hesabu na motivator....'

'....mwingine aliambiwa daladala zinalipa akazinunua akaishia kushinda stand anahesabu tripu Kila ikipita.....'

🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Imenilazimu tu kucheka lakini sio kwamba nina furaha, hapana!
Ukipigiwa hesabu kwa siku unalaza laki si unaona maisha ndo haya zikianza story za makonda hesabu haiendi lazima ushinde stand unahesabu tripu
 
Ni kutuliza akili tu.. sio kila anachofanya mwenzio na kutoboa nawe utatoboa.. kuna watu wametoboa kwenye daladala, majumba ya kupangisha, trekta, kilimo na kadhalika.

Shida wastaafu ni kuweka mzigo woote kwa mara moja, hali hicho kitu hawajawahi kukifanya hata kidogo, hana hata abc zake, ye anatupa mzigo, na si wastaafu tu, kuna wengine huwa wanapata mzigo wa ghafla vuup, milioni 100 hii hapa, analeta masihara anabaki buku mfukoni hana.

Mpaka unastaafu, hujawahi fanya biashara, kosa hilo.
 
Huyo alienunua trekta alifanya maamuzi sahihi.
Inawezekana alikosea tu location, nunua tela jembe na mshinde ya kupukucha unafanyanya kazi misimu yote kiangazi unabeba hata matofali, msimu wa mvua unalima msimu wa kuvuna unapukucha.

matunzo ya trekta na spea zake ni bei za kawaida sana, usiseme spea zimemshinda kamuulize ni changamoto gani imemfanya azi paki.

Ni vizuri hiyo biashara angeianza kabla ya kustaaf ili ajue changamoto zake mapema wala asingepaki
Biashara Sio kwa ajili ya Kila mtu, uzeeni Sio wakati wa kujifunza biashara.
Hela za kustaafu ni sawa na pesa ya mkopo, pesa ya rambi rambi, za michango ya kikundi, pesa ya ada.
Kutoboa na pesa hizi kwenye biashara wengi wamefeli
 
Sijui wanakutwaga na nini mwingine alitapeliwa na hawa wa mtandano ila yeye alikuwa katumia kiasi.

Kwanza hazimalizagi hata miaka miwili. Kifupi hakuna pesa nyingi ukiishika huwa haitoshi bora kuwekeza kwenye nyumba za kupangisha kama ulivyosema au kula tu😁
 
Ni kutuliza akili tu.. sio kila anachofanya mwenzio na kutoboa nawe utatoboa.. kuna watu wametoboa kwenye daladala, majumba ya kupangisha, trekta, kilimo na kadhalika.

Shida wastaafu ni kuweka mzigo woote kwa mara mojq, hqli hicho kitu hawajawahi kukifanya hata kidogo, hana hata abc zake, ye anatupa mzigo, na si wastaafu tu, kuna wengine huwa wanapata mzigo wa ghafla vuup, milioni 100 hii hapa, analeta masihara anabaki buku mfukoni hana.

Mpaka unastaafu, hujawahi fanya biashara, kosa hilo.
Biasharaa Haina adabu hata wazoefu wanaliwa kichwa Chali.
Pana mtu aliingiza viroba vya billion moja kwa hela ya mkopo baada ya mzigo kujaa store, kesho Serikali ikapiga marufuku ya viroba, jamaa alitafuta kamba Hela ya watu itarudije
 
Huyo alienunua trekta alifanya maamuzi sahihi.
Inawezekana alikosea tu location, nunua tela jembe na mshinde ya kupukucha unafanyanya kazi misimu yote kiangazi unabeba hata matofali, msimu wa mvua unalima msimu wa kuvuna unapukucha.

matunzo ya trekta na spea zake ni bei za kawaida sana, usiseme spea zimemshinda kamuulize ni changamoto gani imemfanya azi paki.

Ni vizuri hiyo biashara angeianza kabla ya kustaaf ili ajue changamoto zake mapema wala asingepaki
Sijui kwa Nini alichukua trekta 2.... Angeanza na moja kwanza aone upepo inakwendaje... Watu hawana huruma na pesa za wenzao...
 
Wengi wanavamia biashara bila kuwa na knowledge.

Zingatia vitu vitatu ukitaka kuanzisha biashara.

1. Capital
2. Market
3. Knowledge.

-Usianzishe Biashara ukiwa na msingi penenge, hautaifanya kisawasawa.
-Tafuta soko la uhakika ndipo udumbukize pesa, usifanye biashara ambayo soko hauna utatupa hela
-Hapa ndipo watu wengi wanafeli, wakiona mangi au muha kafungua duka na wao wanavamia.
 
Back
Top Bottom