Somo kwa wastaafu: Pesa za pensheni siyo za kufanyia biashara kama unataka kuishi Maisha marefu

Somo kwa wastaafu: Pesa za pensheni siyo za kufanyia biashara kama unataka kuishi Maisha marefu

Usiombe Hela za kustaafu zimeisha ukawa na uzee usio na Hela ndipo utajua utajua ndoa ilidumu kwa upendo au pesa.

Kwa kizazi hiki cha siku za mwisho ukiwa huna hela mke na watoto wataungana kukunyanyasa kwa kuambiwa ulimaliza Hela kwa wanawake na ulevi.
 
Kama unawaongelea Wastaafu wa miaka ya nyuma ambao walikuwa wanapewa kiinua mgongo chote sawa, ila hawa wa Kikokotoo cha 33% hawezi kupata fedha nyingi hivyo kwa Mkupuo.
===================

Ila hoja yako ina make sense

Nimeona Mkuu King Kong III ameshauri vyema.

Kama huna abcd za biashara mpya ni vyema kutokujiingiza kichwa kichwa kuepusha risks za kupoteza mtaji wako.

Lakini kingine, ni vyema Mtumishi kujitahidi kujenga Nyumba yako wakati ukiwa kazini kuepusha kutumia fedha zako za pension kujengea.

Pia ni muhimu kuwekeza iwe Biashara ya Kiwanda cha Mkate/Kilimo/Biashara ya Ujenzi ukiwa kazini. Sio una staafu ndiyo unahangaika na biashara wakati huna ufahamu wowote

Kuna mtu mmoja aliwahi kusema hela ya Pension ni hela ya kustarehe kabla hujafa.

Ulikuwa unatamani kwenda South Africa kutalii unaenda.

Ulikuwa hujawahi kwenda Zanzibar na Lushoto unaenda.

Ulikuwa hujaoa, basi unaoa at your own risk😜
 
Bi mkubwa alivyopata hela akajifanya mkulima wa matikiti akakutana na tapeli hapo same anaitwa Heriel Mbaga mke wake ni mwalimu hapo same,Akatapeliwa akili imemkaa sawa.Kilichomsaidia hela nyingine aliweka Fixed.Ingepigwa yote.
 
Huruma kweli, matapeli watu wabaya kweli,
 
uzi wa kibabe sana, biashara za kufanya uzeeni ni kujitafutia kufa huku unalalama muda wote mdomo umeuchama
Halafu wale wazee wanoko ofisin ndio Huwa yanakuta Kama malipizi.
Pana Mzee alikua boss dar kawafukuzisha kazi watu wengi plus kuwachafulia mafaili wengine alistaafu akilipwa M 250 Leo ana kaanga chips mbagala ***** zimeisha alidhani akistaafu atalamba teuzi acheni unoko makazini maisha yanaendelea tu hata baada ya kustaafu.
Nataka nikamtafute nimpongeze kwa kufungua kijiwe Cha chips.
Unoko plus ndumba Leo unauza chips
 
Fanya biashara ujanani upate hasara ikupe uzoefu ili ya kustaafia uwe umejifunza kutorudia kosa
 
Halafu wale wazee wanoko ofisin ndio Huwa yanakuta Kama malipizi.
Pana Mzee alikua boss dar kawafukuzisha kazi watu wengi plus kuwachafulia mafaili wengine alistaafu akilipwa M 250 Leo ana kaanga chips mbagala ***** zimeisha alidhani akistaafu atalamba teuzi acheni unoko makazini maisha yanaendelea tu hata baada ya kustaafu.
Nataka nikamtafute nimpongeze kwa kufungua kijiwe Cha chips.
Unoko plus ndumba Leo unauza chips
Nimecheka kama mazuri, atalamba teuzi sio
 
Nimecheka kama mazuri,atalamba teuzi sio
Teuzi awape nani hawana connection, Washamba tu wengi wao wametokea bush na wazazi wao hawakuwahi fanya kazi Serikali wakauona msoto wa wazazi wao waliopigika kwa uzalendo baada ya kustaafu.

Kazi zenyewe za kupita unawafanyia mabaya wenzio kisa madaraka wanachoka vibaya
 
Bi mkubwa alivyopata hela akajifanya mkulima wa matikiti akakutana na tapeli hapo same anaitwa Heriel Mbaga mke wake ni mwalimu hapo same,Akatapeliwa akili imemkaa sawa.Kilichomsaidia hela nyingine aliweka Fixed.Ingepigwa yote.
Heriel Mbaga mke wake ni mwalimu hapo same
 
Bi mkubwa alivyopata hela akajifanya mkulima wa matikiti akakutana na tapeli hapo same anaitwa Heriel Mbaga mke wake ni mwalimu hapo same,Akatapeliwa akili imemkaa sawa.Kilichomsaidia hela nyingine aliweka Fixed.Ingepigwa yote.
Mbona kama unashangilia?au alikuwa haambiliki?
 
Lete Maneno.....
By JK Wa Msoga Chalinze Pwani Tanzania

JK Alisema Mwayangumwangu
 
Watu hawana huruma na wastaafu, huwapa michongo ya pesa wanaishia kufa kwa pressure. Ukistaafu idea nyingi sana unaletewa na ndugu.

Pana mstaafu alipata milion 250. Shemeji yake akamwambia tufate pikipiki China ukileta kwa jumla pesa ipo, akampa pesa shemeji yake akalala nazo kona China, hadi wa leo hata kama alirudi nchini kimya kimya siri yake.

Pana mstaafu aliambiwa trekta zinalipa akapigiwa hesabu na motivator akaingia dukani akachukua trekta mbili mpya kwa milion 90 leo zipo juu ya mawe zinaliwa na kitu, amekosa pesa za kununua spea.

Mwingine aliambiwa daladala zinalipa akazinunua akaishia kushinda stand anahesabu tripu Kila ikipita. Ukistaafu achana na biashara, nunua bond au weka fixed nje ya nchi mfano Canada, USA au zile stable country ule gawio kila baada ya muda, umeshindwa sana jenga chumba sebule chumba sebule gombana na wapangaji maisha yasonge.

Kisha tafuta shamba mikoani acha familia mjini weka kasikilize sauti za ndege tu porini unalima kilimo kisicho cha biashara ili kufanya mazoezi tu utafika miaka 100, pia kaa mbali kabisa na hawa mitume na manabii watakufilisi.

Pana mama yupo kitandani mwaka sasa anaumwa, aliambiwa biashara fulani inalipa alikuwa na nyumba zake 4 alijinyima akiwa kazini kujenga, akaingia bank akazikopea milion 200 baada ya muda biashara ikawa hasara bank wanataka hela zao.

Bora upoteze pesa ujanani una nguvu kuliko kupoteza uzeeni, zikienda zimeenda.
Ndiyo upumbavu wao hao amefanya kazi almost atleast 30 year bila kufanya biashara baada ya miaka 60 eti ndiyo anataka kufanya biashara! Idiot watumwa hao
 
Back
Top Bottom