Somo kwa Watoto wetu,vilaza waliopata fursa na vijana mnaochipukia!

funaku

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Posts
39,468
Reaction score
31,952
Somo hili nalileta kwenu kwa ujumla yaani lina cut across kada zote zinazotakiwa kuhudumia jamii na pia jamii yenyewe inayotakiwa kuhudumiwa.

MOSI:
Lazima mjitambue kwamba ninyin ni watanzania na utambulisho wenu daima uatakuwa ni utanzania.Utanzania ni muunhaniko wa makabila mengi ikiwemo wabantu ,wahamiaji wa zamani lakini wameunganishwa na lugha ya kiswahili.
kimsingi watanzania hawana dini wala kabila na hivyo siku zote tujitambulishe kwa utanzania wetu.

PILI
Nchi hii ni nchi mama yenye historia ya kuwa na binadamu wa kale,ikisadikiwa na kuaminiwa kuwa uwanadamu umeanzia hapa kwetu.hivyo baraka za kiuwadanamu tunazo kutokana na tafiti za kisayansi na ushahidi wa mabaki mbalimbali.

TATU
Nnchi hii kwa muktadha wake haiwezi kuacha kutamaniwa na watu kutoka nje hivyo itabidi kutoka jasho la damu kuilinda vilivyo na kulinda values zake .

NNE
Nchi hii imefikiwa na Tawala nyingi za kibabe yaani dola korofi za karne na karne lakini haikuwahi kuwa koloni kamili yaani ilishindikana ...hivyo inabidi kumantain statua hiyo.Ila ni muhimu kujua kuwa watakuja tena na tena.

TANO
Wapo wakongwe waliowahi kuipambania nchi hii hadi leo na walifanikiwa kwa kiasi flani ,wengine wameshatangulia mbele ya haki na wachache wapo.tunapaswa kujifunza madahaifu yao na hivyo kuboresha pale walipoishia.

SITA
Nchi hii ipo katika eneo la kimkakati kati ya pande mbili hasimu duniani yaani mashariki na Magharibi...ili uifiiie mashariki kikamilifu lazima Upitie Tanzania hivyo yoyote anayeishika magjaribi kikamilifu lazima atafute njia ya kuifikia mashariki kiurahisi.yoyote anayeitafuata kaskazini au kusini mwa Afrika kiuchumi lazima apitie Tanzania.

SABA
Wapo maadui au marafiki wakubwa ambao inapaswa kuendana nao kwa uangalifu mkubwa ili nchi hii iendelee kuishi .maadui hao na marafiki hao ni pamoja na Urusi,Marekani,Uchina,Uingereza na India na UAE.
Hawa ni maadui na ni marafiki kulingana na nyakati na mandhari ya hali ya mambo.

NANE
Tunayo sera muhimu sana ambayo ilibuniwa na waasisi wetu wa Taifa hususani mwalimu Nyerere.yaani Sisi hatufungamani na yoyote tunaenda na yule ambaye anaendana na maslahi yetu.SERA HII NI YA KIPEKEE na inapaswa kuenziwa.

TISA
Dunia ya leo imeendelea sana katika teknolojia na imefanikisha mawasiliano kwa haraka...lakini haimaanishi mawasiliano ya haraka kuwa ndio mawasiliano sahihi.bado hulka,aina ya mawasiliano na ujumbe wa mawasiliamo ni ule ule ...hivyo tusijipagawawishe na urahisi wa mawasiliano bali tuuchuje ujumbe uliowasilishwa .Watu walishawahi kuwasiliana kwa njia tofauti na wakafanya makubwa sana .

KUMI
Wewe kama kijana namzalendo hakikisha unaweka maslahi ya nchi mbele kabla ya lolote lile.
Usipoweka maslahi ya nchi mbele...nchi haitokuwepo na wewe hutakuwepo pia.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!
 
Imeeleweka. Tunangoja watambuzi na wachambuzi waseme nasi tuone wanachosema kama sio kusikia.
 
Back
Top Bottom