SOMO LA BURE: Namna ya kuagiza bidhaa kutoka CHINA kwa ajili ya biashara (jumla) Kupitia Mtandao alibaba kwa kutumia simu yako

Acha nikae karibu na huu uzi...Kuna la kujifunza kwa wale ambao bado hatuja jipata.
 
Vitu kama laptops, computer displqy unaweza safirisha kwa meli na inakuwa kwa cbm!?
Kampuni nyingi za bongo laptop, simu,Ipad wanatoza kwa PC siyo cbm.
Mfano smart phone (simu janja)PC Moja ni usd20, laptop USD 50, Ipad USD 30 bei hii iwe unasafirisha Kwa meli au ndege. Lakini phone accessories ndiyo zinatozwa Kwa CBM
 
mkuu, hivi nawasialiana au najiunga vipi na hawa shipping agents kama Silent ocean,? Ili niwatumie
Ingia Insta page ya silent utakuta mawasiliano yao chati nao Kwa whatsup, watakutumia address zao za china inakuwa kama business card, supplier akikuuliza do you have a shipping agent in china? Unamjibu ndiyo harafu unamtumia hiyo business card kama ilivyo, Kwa hiyo baada ya wewe kulipia mzigo ndiyo anaupeleka kwenye warehouse za silent zilizopo china.

Supplier akifikisha mzigo wako atapewa risti inayothibitisha kuwa mzigo wako umepokelewa na silent ocean atakutumia kwenye page ya Alibaba mliyokuwa mnachati naye wakati wa manunuzi .
 
unafuata bandarini mwenyewe au unaletewa ulipo?
Mzigo ukifika utapokea ujumbe kwenye simu yako kuwa mzigo umeshawasili na kukutaka ufanye malipo na baada ya hapo unaenda kwenye warehous(godown) la kampuni uliyosafirishia kuchukua mzigo wako ukiwa na nakala za risti za malipo na risti ile uliyotumiwa na supplier alipofikisha mzigo wako(rist ya mzigo kupokelewa china kwenye godown unaonyesha kwa kutumia simu yako kama uliyotumiwa na supplier)
 
Uzi poa sana kaka, ziko site nyingine zenye bei chini ya Alibaba kama 1688, Pinduoduo n.k

Kwa products zenye quality uhakika, mtu anaweza check taobao.

Tatzo la site nyingi zenye bei nzuri, zina tumia kichina tupu..so uta hitaji translator….

Lakini kwa kuanzia, hapo si pabaya….

Mtu ukijimudu pia ni vyema ukafika china mwenyewe….kule utakuta pia baadhi ya bidhaa bei ni hata nusu ya hizi za alibaba na sites nyingine… issue n upatkanaji wa masoko….wabongo wengi hawatoi code….


Pia masoko yako mbali mbali sana….so uta hitaji mtu wa kukuguide….mimi niliemda kichwa kichwa, nikapoteza mwezi mzima hola….ila round 2 ikabidi nipate mchina, mambo ndo nika yafurahia.

Tukaze wakuu….ukimaster hizo site, unaweza save pakubwa sana, ukicompare na kununua hapa bongo.

NB: Zipo baadhi ya products tayar wachina wana agents bongo…so ukienda hawato kuuzia…. Ni vyema kujua pia hilo, usije fata hewa.

Tuendelee peana nondo.
 
Ubarikiwe sana kiongozi kwa bandiko hili
 
Mkuu unaonekana uko legend mwaga Michele kidogo au tuje inbox
 
Nilinunua mzigo wa 1. 2M ila almost mzigo wa 600,000 ni substandard na overpriced kwa bei niliyonunulia. Ingawa kwa kulazimisha nitauza hivyohivyo kurudisha gharama ila hela yangu imelala.
Huu mzigo uliokuwa sawa unaenda vizuri. Suppliers wengine wakengefu. Suppliers wasio wa Aliexpress na Alibaba ni wazuri zaidi.

Niliagiza uko sababu MOQ ni ndogo, nilikuwa nataka vitu vidogo ambavyo kwingine mpaka niagize pisi nyingi.
 
Pole sana bingwa, ndio unazidi kukomaa kadri unavyoumia ndio unaimarika, utakua bora zaidi kadri unavyosonga.
 
Huu uzi mzuri sana.

Ila naomba kufahamishwa VIP KWA WALIO MKOANI MAPEMBELO CARGO wanatuletea mpaka huku au utaratibu upoje??
 
Mzigo wa kilo 10 niliambiwa laki 9, je imekaaje wakuu hii kampuni ya dhl
 
Asante kwa hii experience yako mkuu
 
Asante sana mkuu kwa uzi mzuri
nilichojifunza kumbe ata akina sisi wa kujitafuta na ka 2M tunaweza piga biashara za china na mambo yakaenda baada ya mwaka ukawa ngazi nyingine 😀 thanks again
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…